Tusijitoe ufahamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusijitoe ufahamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 26, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,349
  Likes Received: 22,207
  Trophy Points: 280
  NI LAZIMA TUFAHAMU KUWA Mungu ametuumba kwa kusudi maalum.
  Akatupa Jinsia tofauti ili tuweze kuendeleza kizazi chetu na tutimize wajibu na majukumu yanayotukabili siku kwa siku.
  Tunapoamka na kuzna kuitumia vibaya miili yetu na jinsia kwa kigezo kuwa Msondo waliimba wanaume tumeumbwa kuhangaika, wanaume mateso, kwa hiyo najitoa kwenye kundi la wanaume kwa kuogopa majukumu ni kujitoa ufahamu.
  Mungu kwa kuwa alituumba kwa kusudi maalum anajua ni jinsi gani ya kukuwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za kila siku za kimaisha, kula, matibabu, pango la nyumba, karo za shule, fedha ya kujikimu kwa wale wanaotutegemea, na kadhalika vyote Mungu atakupa ukimtegemea, ukijituma kwa bidii na kwa moyo wote.
  mungu aturejeshee ufahamu wetu ambao tumemkabidhi shetani, atupe mwangaza wa dhati wa kujifahamu na kujitambua na kuuheshimu utu wetu na miili yetu, ili tuweze kuitumia vyema na kwa heshima ili wale wanaotuzunguka waone utukufu wa Mungu kupitia miili yetu.
   
 2. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Bujibuji BIG UP Brother!........
   
Loading...