Tusijidanganye Simba hii ni ya kawaida sana, uongozi unaendeshwa kiujanja ujanja, MO tuachie timu yetu

kt the irreplaceable

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
2,363
4,851
Wakuu kwema?

Ukitizima kwa jicho la kiufundi hii timu yetu ya Simba ni timu dhaifu, kweli tutasema tumefuzu hatua ya makundi Klabu Bingwa Africa lakini tumekutana na timu gani? Huwezi kujisifu kwa kupigana na mlevi.

Tazama mechi ya Azam, Singida na Yanga, Simba yetu ikikutana na timu iliyo 'compact' hatutoboi, ukweli usemwe. Tuna wachezaji ambao ni wa kawaida sana, mtu kama Kibu ataifikisha wapi timu?

Aya twende kwenye uongozi, huku ndiyo ujanja ujanja, walikuwa wanajificha kwenye kivuli cha Yanga kufungwa kimataifa. Mpaka sasa kocha mkuu Mgunda hana mkataba, hawajui kama wamuongezee au watafute kocha mpya.

Mpaka sasa anayejiita mwekezaji hajaweka ile pesa shilingi bilioni 20 kama thamani ya hisa ya asilimia 49. Timu inasajili wachezaji wa laki 5 kama akina Kibu itafika wapi? Angalia Yanga wamecheza michezo pungufu ila ndiyo wanaongoza ligi. Halafu kuna mbumbumbu wanasema tutachukua kombe, labda kombe la kahawa.

Mo Dewj tuachie timu yetu, ondoka na huyo dada yako Barbra, wanachama tunataka 20b, hatuwezi kuendelea kuwa mambumbumbu kiasi hiki.
 
Mpaka sasa anayejiita mwekezaji hajaweka ile pesa shilingi bilioni 20 kama thamani ya hisa ya asilimia 49. Timu inasajili wachezaji wa laki 5 kama akina kibu itafika wapi? Angalia yanga wamecheza michezo pungufu ila ndio wanaongoza ligi, alafu kuna mbumbumbu wanasema tutachukua kombe, labda kombe la kahawa.
Ni kweli kabisa ubabaishaji tu mkuu. Sasa nikwambie kitu kaweke bid ya 500B tumpe Mo vihela vyake utupeleke nchi ya ahadi.
 
Wakuu kwema?
Ukitizima kwa jicho la kiufundi hii timu yetu ya simba ni timu dhaifu, well tutasema tumefuzu hatua ya makundi klabu bingwa Africa lakini tumekutana na timu gani? Huwez kujisifu kwa kupigana na mlevi.

Tizama mechi ya Azam, Singida na Yanga, simba yetu ikikutana na timu iliyo compact hatutoboi, ukweli usemwe. Tuna wachezaji ambao ni 'average' sana, mtu kama kibu ataiifikisha wapi timu?

Aya twende kwenye menejinent, huku ndio ujanja ujanja, walikua wanajificha kwenye kivuli cha Yanga kufungwa kimataifa. Mpaka sasa kocha mkuu Mgunda hana mkataba, hawajui kama wamuongezee au watafute kocha mpya.

Mpaka sasa anayejiita mwekezaji hajaweka ile pesa shilingi bilioni 20 kama thamani ya hisa ya asilimia 49. Timu inasajili wachezaji wa laki 5 kama akina kibu itafika wapi? Angalia yanga wamecheza michezo pungufu ila ndio wanaongoza ligi, alafu kuna mbumbumbu wanasema tutachukua kombe, labda kombe la kahawa.

Mo dewj tuachie timu yetu, ondoka na huyo dada yako babra, wanachama tunataka 20b hatuwezi kuendelea kua mambumbumbu kiasi hiki.
Unavyohangaika na Mo!! kama kuku anaetafuta sehemu ya kutagia!! mwana uto mkubwa! ila hongereni kwa kuingia makundi ya walioshindwa!!
 
Wakati mwingne tuwe na shukran wakuu

Kaz wanaoyoifanya Mohamed dewji said bakhresa na ghalib (gsm) n kubwa Sana ndugu zangu

Tuwe na neno la shukrani kwao

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Yani wanajiropokea tu wkt wakiachiwa timu hamna wanachofanya. Sijui wanadhani ni kaz rhs kuendesha club. Mo anajitahid sn na km wanaona anazingua basi waweke hela zao tuone
 
MO AKIWA SIMBA HATA KAMA ANADAIWA NA HAJATOA HATA MIA HADAIWI KITU NA SIMBA MO NDIO ANAIDAI SIMBA. WEWE NI MASKINI KWA AKILI ZAKO UNADHANI PESA YA MO HAITUMIKI SIMBA MDA HUU NINAVYO ANDIKA HII REPLY
 
Wakati wa Usajili Mo Alijitoa.....

Simba Haina wachezaji ndio maana ilihusishwa na wachezaji zaidi ya kumi na ikaishia kuwakosa wooote.

1.Bambala.
2. MANZOKI.
3.Bobosi.
4.Azizi K
5.Adebayor
6
Orodha ni Ndefu sanaaaaa!

WACHEZAJI MIZIGO.
Banda. .................... .Boko
Sackho. ................... .Nyoni.
Okwa. ............... ...Gadiel.
Dejan. ....................... Mwenda.
Kanute. ......................... Kyombo.
(Akpan)
Onyango.
 
Back
Top Bottom