Tusichoke Kuyajadili Matatizo Ya Simba

Tusichoke Kuyajadili Matatizo Ya Simba

Mkuu Amavubi kwa hali ilivyo sasa, Simba Sc tunahitaji muujiza zaidi ya ule "ngamia kupenya katka tundu la sindano" ili tuweze kumaliza angalau nafasi ya 4 msimu huu. Ila pamoja na yote hayo tarehe 08/03 ushindi upo palepale.

NB: Bado nipo naomboleza matokeo ya juzi.
 
Last edited by a moderator:
Nimetumia neno wadau nikimaanisha wadau wote wa soka, mwenzenu wiki hii nimechanganyikiwa sana na hii Simba

Nini Kifanyike Jamani, hali hii imekuwa mbaya sana mwaka huu, hatujawahi kufurahi walau mara mbili mfululizo, tukifurahi inafuta sare au kipigo

maoni ya kujenga jamani si ya kubeza, nisije geuka yule shabioki wa Kenya

Simba na Yanga zote zife tu.
 
Mkuu Amavubi kwa hali ilivyo sasa, Simba Sc tunahitaji muujiza zaidi ya ule "ngamia kupenya katka tundu la sindano" ili tuweze kumaliza angalau nafasi ya 4 msimu huu. Ila pamoja na yote hayo tarehe 08/03 ushindi upo palepale.

NB: Bado nipo naomboleza matokeo ya juzi.

Kama tukiamka kuanzia mechi ijayo, hata ubingwa unawezekana, maana kiukweli sio kwamba wa kwanza katuacha saaaaana, ni michezo kama minne, ila nafasi ya tatu na ya nne vinawezekana kabisa!
Simba hata iwe mbovu kiasi gani, Yanga huwa wanakalishwa, Yanga wenyewe wanajua hili halina ubishi.
 
Ndala katuacha pointi 11, tarehe 8/3 tunamfunga zinabaki point 8 ambazo ni kama gemu 3.. tatzo lililopo ni je ndala ataweza poteza mechi 3 na si tushinde zote?! Jibu ni Hapana. Pia timu zilizo nyuma ya Ndala zipo vizuri, Mf. Kagera Sugar ambayo imeshinda mfululizo mechi za karibuni hadi kufika no. 3.

Timu yetu imekosa consistency ndo mana leo tunashinda kesho tunadraw keshokutwa tunafungwa. Eeeh Mungu saidia hili pepo linalotukumba hivi sasa, liwavuruge pia na watesi wetu wote ili tusichekane mtaani.
 
Muache sifa,siku nyingine mkiambiwa timu BOVU msibishe....pili...walipeni mshahara na posho nzuri...Tatu..mkishinda mechi ijayo mshishangilie kabisaaaaaa..
 
ligi siyo simba na yanga mkuu
 
tukubali kuwa na subira hadi vijana watakapokomaa lkn najiuliza tumsubiri messi akomae??

kushangilia ni hulka
 
Mkuu ubingwa ndo basi tena na mechi ambazo zimetukosesha ubingwa ni ile ya Mbeya City na ya Stand united. Sare zile za mwanzo mwanzo nazo zimetucost sana.

Mimi kila mara lawama zangu nazipeleka kwa uongozi, walimwacha Kibadeni akasajili kabla timu haijakomaa akaondolewa, Loga naye alivyokuja akaachwa akasajili kabla hata wachezaji hawatumia akaondolewa, Phiri naye alivyokuja akasajili kabla hata hajatumia wale wachezaji akaondolewa, huyu naye amekuja amekuta wachezaji tayari wapo na analalamika timu haikuandaliwa toka mwanzo kucheza ligi kuu hata akifungwa sababu yake ni kwamba timu hakuiandaa toka mwanzo.

Simba kuna tatizo la muunganiko wa timu, ukiangalia mchezaji mmoja mmoja ni wazuri sana lakini tatizo ni muunganiko, angalia toka ligi ianze tumeshatumia wachezaji zaidi ya ishirini, kwa haraka haraka ni Mapunda, Manyika, yule kipa aliyetoka Mtibwa, Wiliam Lucian, Chollo, Kessy, Baba Ubaya, Shabalala, Banda, Owino, Isihaka, Juuko, Mkude, Kwizera, Kiongera, Tambwe, Mkude, Awadhi, Singano, Kiemba, Chanongo, Miraji Adam, Okwi, Sserunkuma wawili, Hajib, Maguli, yule Messi wa Tanga, Seseme, Kisiga hao niliotaja ni 30 na huenda kuna wengine siwakumbuki, sasa ndani ya mechi 15 unatumia wachezaji 30 pengine na zaidi na sababu ya mejeruhi ni kama wanne tu au watano halafu unatarajia timu iwe na muunganiko wa kueleweka kweli?

Na kama hili swala la kukosa posho kama nalo ni la kweli hali itakuwa mbaya zaidi maana jamaa walioko nyuma yetu wengine tumelingana nao pointi na wengine tumewazidi moja hivyo ikitokea watatu au wanne wameshinda na sisi tukatoa draw au kufungwa maana yake tunarudi nafasi ya nane au ya tisa. Bahati mbaya mechi zinazofuata ni za prisoni ambaye anashika mkia na Yanga ambaye anaongoza hivyo zote ni ngumu. Ni ngumu kushuka daraja lakini safari hii kama wachezaji wasipoamua kupigana ndani ya uwanja hali ni mbaya, viongozi ni kama tayari hawana jipya, kilichobaki ni juhudi za makocha pamoja na wachezaji wenyewe.
 
Muache sifa,siku nyingine mkiambiwa timu BOVU msibishe....pili...walipeni mshahara na posho nzuri...Tatu..mkishinda mechi ijayo mshishangilie kabisaaaaaa..
Kuacha kushangilia wakati timu imeshinda ni ujuha usio kifani.
 
Muache sifa,siku nyingine mkiambiwa timu BOVU msibishe....pili...walipeni mshahara na posho nzuri...Tatu..mkishinda mechi ijayo mshishangilie kabisaaaaaa..

"KUHUSU POSHO"

Kuna mahala nilisoma kuwa Yanga huwalipa wachezaji posho ya 150,000 wakishinda, Azam 130,000 na kwa Simba Sc nusu ya gate collection inayopatikana hupewa wachezaji wagawane..

Mechi za Simba Sc uwanja kujaa na ticket kuwa sold out ni kawaida sana, hii inamaanisha gate collection huwa ni mpunga mrefu.

Mfano.. narudia tena huu ni "mfano", kama kila mtu katka kikosi akakunja 300,000 kwa mechi.. 300,000 mara 30 ni sawa na milioni 9.. ambayo inaweza kuwa mara 3 ya nusu ya gate collection.
 
Mkuu Masuke nimekusoma vyema, cha kufanya sasa ni kuendelea kuvumilia maumivu katika hizi mechi zilizobaki. Ila naamini msimu ujao Simba Sc chini ya Goran Kopunovic itakua imara zaidi.
 
Last edited by a moderator:
tukubali kuwa na subira hadi vijana watakapokomaa lkn najiuliza tumsubiri messi akomae??

Messi ili akomae zaidi anahitaji mtu kama Msuva ambae ata mpush zaid.. tofauti na sasa ambapo anajiachia tu kwa sababu hana mpinzani..
Mf. misimu kama miwili iliyopita pale madrid, di maria alikua kaanza kuzoea na kuzembea zembea, perez akamshusha bale kikosini. Yaliyotokea wote tunayajua, mana bale alikaza di maria akakaza matokeo yake wote tunayajua.. madrid alikomba kila kilicho mbele yake.. Vivyo hivyo kwa huyu Messi anahitaji ushindani wa namna hiyo.
 
Mkuu Masuke nimekusoma vyema, cha kufanya sasa ni kuendelea kuvumilia maumivu katika hizi mechi zilizobaki. Ila naamini msimu ujao Simba Sc chini ya Goran Kopunovic itakua imara zaidi.
Swali ni je ataachwa aendelee kuwepo hadi msimu ujao? Na je mwisho wa ligi hawataondolewa baadhi ya wachezaji na kuletwa wapya? Na wale ambao mikataba yao inaisha je wataongezewa?
 
Last edited by a moderator:
Swali ni je ataachwa aendelee kuwepo hadi msimu ujao? Na je mwisho wa ligi hawataondolewa baadhi ya wachezaji na kuletwa wapya? Na wale ambao mikataba yao inaisha je wataongezewa?

Kwa sasa hebu tuamini kuwa kocha atapewa 2nd chance.. pia promising players kama mkude, ajibu, isihaka, kessy n.k tutaendelea kua nao kwa miaka mingi ijayo.
 
hiyo timu ya copacocacola aliiweza loga timu ilikuwa mbovu zaidi ya hii lakini alitumia mbinu kupata matokeo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom