kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,363
- 17,597
Kila mtu anajua kuwa kila mtu anahitaji kula, kunywa, malazi, mavazi, usafiri, matibabu, na kulipia sherehe za furaha na huzuni kwake, mkewe/mumewe, watoto, ndugu na jamaa zake bila kujali aina ya kazi anayofanya, umri, jinsia, elimu, dini, kabila wala rangi yake. Wafanyakazi wanadai mishahara yao ni midogo lakini bado wako kazini, wafanyabiashara wanadai biashara nguvu lakini wapo na wananchi wanadai vyuma vimekaza mitaani lakini kesho yao inafika.
Je, kuna mbinu gani wafanyakazi wanaitumia kuweza kumudu kuendesha maisha yao kwa siku 30? au waongo wanatuzuga sisi tusio na ajira?
Wananchi mitaani wanamudu vipi kuyaendesha maisha yao ya kila siku? au ni waongo wanatafuta kick tu kwa watawala?
Mbona magari yanatembea, bia na soda zinanywewa, nyumba zinajengwa na watoto wanasoma?
Kuna miujiza gani watu wanaifanya ili mambo yao yaende?