sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 591
- 1,000
Tuungane tena kwenye kuliangalia hili.
Jamaa yangu ni chapombe,bangi na mwasherati aliyekubuhu.Mara kadhaa amekuwa analewa nakulala nje(harudi nyumbani).Tarehe zamshahara haonekani nyumban hadi juhudi zakumtafuta zifanyike.
Mwezi ulopita alinieleza jambo ambalo binafsi nililichukulia Kama sehemu ya mauzauza ya bangi mbichi anazovuta. Alikuja kwangu nakunieleza kuwa marehemu mama yake kamtokea kwenye ndoto na kumsihi aache hizo tabia zaulevi vinginevyo atakufa hivi karibuni.
Baada yakumsikiliza kwa muda nikagundua kuwa jamaa yupo serious. Jamaa anadai kwenye kuota huko aliambiwa na mamayake aokoke kwa maana ya kufuata misingi ya Mungu kupitia dhehebu flani la kikristo.
Jamaa anaishi na mkewe mwaka wa9 saivi na Wana watoto wao wawili.
Mwanzo wa mwezi huu jamaa amekuja kwangu anadai amemshirikisha mkewe juu ya nia yake yakuokoka nakumrudia Mungu Ila mke amekuwa mbogo hataki kusikia jambo Kama hilo.Jamaa na mkewe ni wakatoliki japo tangu alipofunga ndoa hakurudi tena kanisani.
Alivyoamua kuacha hayo Mambo aliamua abadili dhehebu kitu ambacho mkewe hakubaliani nachi na kudai bora jamaa abaki Kwenye tabia zake za awali kuliko kuhama dhehebu.
Mke amesema Kama jamaa atabadili dhehebu basi ndo mwisho wa wao kuishi pamoja.
Jamaa anadai ana wiki3 hajui pombe Wala sigara(bangi)Ila Cha kushangaza haoni furaha ya mkewe zaidi ya visirani vya hapa napale.
Wakuu, mwanamke aliyeteseka miaka mingi kwa tabia mbaya zamumewe anaweza kweli kutaman mumewe aendelee na Mambo maovu kuliko kubadili dhehebu?(sio dini)
Kwangu naona mwanamke alitakiwa kufurahia maamuzi ya mumewe kuacha tabia mbaya kuliko kutizama anaelekea dhehebu gani
Kwa mtazamo wangu wa haraka nahisi huyu mwanamke Kuna namna alikuwa anafaidika kutokana na tabia za ulevi za jamaa.
Je,mnadhani nini kipo nyuma ya msimamo wa huyu mwanamke dhidi ya kuokoka kwa mumewe.
Wasalaam!