PintoG
JF-Expert Member
- Jun 12, 2017
- 612
- 732
Ukitaka kujua Tanzania miaka 20 ijayo kutakuwa na kugombania rasilimali ya ardhi jaribu kutembea mikoani kwa kuangalia maeneo yaliyokuwa na misitu na vichaka vingi, mikoa kama Tabora,Kigoma,Geita,Kagera nk. maeneo mengi yamevamiwa na watu wameweka makazi, misitu mingi imekatwa hakuna tena mapoli makubwa kama ilivyokuwa zamani. idadi ya watu inaongezeka kwa kasi sanaaa hasa vijijini ambapo ni kawaida kukuta familia ina watoto 5-7 .
Miaka ya 98-2010 palikuwa na campain sana juu ya uzazi wa mpango ,( nakumbuka nyota ya kijani) hii ilisaidia sana familia nyingi kuwa na wastani wa watoto 2-4. lakini kwa sasa serikali na asasi binafsi wamesahau kabisa kuwa population inapanda kwa kasi sana lakini resource zinaendelea kuwa vile vile, na ukienda vijiji watu wengi wanashindwa kumudi mahitaji ya familia kwa sababu watoto wanakuwa wengi sana kuliko uwezo wa wazazi kuwahudumia.matokeo yake watoto wa kike wanazaa mapema na kuleta wajuu nyumbani na kuzidi kukuza familia,elimu pia inakuwa duni na lishe pia.
wito wangu kwa serikali na asasi binafsi waliangalie tena suala la uzazi wa mpango.