miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,815
- 49,031
Habari za asubuhi wapendwa ..
Kuna kesi nimeletewa ni wiki sasa natafakari na kuamua kuwafundisha baadhi yetu wenye tabia kama hizo..
Kesi yenyewe kwa ufupi tu ni kuna wana ndoa wapo kwenye kutoelewana kwa muda sasa kisa mume anatabia ya kuchepuka , ila mke ana rafiki yake wa kike ambaye yeye hajaolewa na ndiyo rafiki yake mkubwa kiasi kwamba hawa wanandoa kama vile wanamtumia katika kusuluhisha matatizo yao... lakini aliyeanzisha ni mwanamke kumtuma rafiki yake kwa mume wake kitu ambacho si kibaya....
Sasa kumbe mume kashaacha madanga yote au kaamua kubeba yote pamoja shoga yake mkubwa, Sasa mke analia haamini kinachoendelea na wala hataki kusikia mume wala rafiki. Nipo naye mtu kamleta kwangu nimsaidie ila naona ana kiu ya pombe anataka kulewa sasa tumekunywa weweee jana akaniambia kiu imeisha sasa tujenge au tubomoe. Nimeshayajenga kwake sasa nikaona nije niwajenge na baadhi yenu humu....
Kuna makosa tunayoyafanya wanawake/wanaume katika kutafuta suluuu. Kutumia rafiki kama njia ya mawasiliano yako.... Unajua unapokuja kwangu kunieleza mambo ya mwenza wako na ukanipa nafasi ya mimi kuonana nae kukujadili automatic sababu umesema mabaya yake kwangu na yeye atasema ubaya wako zaidi na anaweza kutengeneza mazingira ya kuonewa huruma na kitakachotokea ni rehema za Mungu tu.......
Huwa wanasema wewe unamwona wa nini wenzio wanasema watakipata lini? Hujui yupi anayemtamani mkeo au mumeo okey akimaliza kusuluhisha unadhani mawasiliano yanaisha ooh no yanaendelea na watakuwa wameshakukatia A.K.A........sababu adui ukishamjua ni nusu ya ushindi...
Tupunguze kutoa madhaifu ya wake au waume zetu kwa marafiki.. Jamani binadamu tunataka kusikia ubaya zaidi kuliko mazuri ndiyo maana baya moja hufuta mazuri elfu..
Unamwambia mshikaji wako ooh mke wangu ooh mume wangu hivi na vile jamani humo humo kwenye weakness ndiyo tunapochezea .. na ndiyo maana ndoa nyingi wanasalitiwa na watu wa karibu hasa wanaojiita washauri wetu kuweni makini..
NB: Ni bora ukaja huku jf au sehemu yeyote ile ukaomba ushauri usiyemjua akakushauri ukasepa kuliko hao mnawaita mashoga .. pia si marafiki wote wabaya
okey weekeend njema .. Nipo tayari kujibu maswali ...