Harusi zimekuwa na gharama sana kuanzia maandlizi hadi kufanikisha. Lakini ndoa ngapi ziko kwenye furaha kama wakati wa Kudate? Baada ya kero basi kuachana huwa ni suluhisho kwa wenzi wote. Gharama mara 2 Kuowa na kuachana (Divorce). Divorce huhusisha mambo ya kisheria kamaspousal support, child custody, child support, distribution of propertyand division of debt. Lakini mambo haya huwa hayapo kuwapo na Uncontested divorce.
Angalia Takwimu za Marekani Mwaka 2008, takribani 40% ya ndoa ziliishia kwenye divorce. Kwa Tanzania ndoa nyingi hudumu kwa miaka 6 na baada ya hapo talaka na kuachana. Takwimu zinaonyesha ni 15% ya ndoa husheherekea 20 years anniversary kwa amani na upendo. Watu wengi huishi kwenye ndoa wakati hakuna ndoa hii ni katika kulinda status quo kuonyesha jamaa wako kwenye ndoa lakini ukweli ndo iliisha vunjika miaka kadhaa nyuma.
Kama unajua kuna kuachana kwanini uingia gharama mara 2? Kuowa na kulewa na kuingia hassles za kuachana?
Kwa wale ambao hamjaowa ama kuoelewa I strongly Urge you NOT to get blinded unto Marriage institution. Cohabitation should be the way forward, Nina Advocate ndoa za mikataba....
Masa
Rev i differ to agree with you in some point
Kwanza kweli kuoa siku hizi imekuwa gharama na asilimia kubwa ya vijana wanaishia kuishi pamoja wanakuwa na watoto bila kuwa kwenye marriage insititutution kutokana na gharama kubwa za kuanza maandalizi ya harusi mpaka harusi yenyewe. Vile vile gharama za mahari nazo kwa makabila imekuwa kama ni kukomoa
Ila swala la kusema cohabitating iwe suluhisho la matatizo ya divorce nyingi zinazotokea naomba nitofautiane na wewe. Ndoa ni insititution ambayo inajengwa na pande mbili zilizokubaliana kuingia kwenye mkataba wa kuishi pamoja. Marriage contract ni pana zaidi ya kusaini vyeti vya ndoa ni makubaliano yanayojengwa na pande mbili ambhazo zimekubaliana kuchukuliana mizigo na kusaidiana na kuishi pamoja till death do them apart. kama Institution inatakiwa ijengwe na pande zote na lazima pande zote ziwe tayyari kukubaliana na masharti ya mkataba huo wa ndoa. Ndoa nyingi zinavunjika kutokana na ama watu wengine wanaoa hawajawa tayari kuachana na mambo yao ila may be umri umemforce kuoa ila bado ana vimada wake ambao hayuko tayari kuachana nao japo anajua yuko kwenye ndoa na alishasema atakaa na mwenza wake kwa maisha yake yote
Wengine wanaoa kwa sababu alimpa mimba mtoto wa mtu na wazazi wamekuja juu hawataki biashara nyingine zaidi ya mtoto wao kuolewa so jamaa anamuoa dada husika kwa sababu hana choice japo kwake hiyo mimba na hata dada mwenyewe ilikuwa bahati mbaya
Wengine wanaoa kufuata mkumbo kuwa rika lake wakiwemo marafiki zake wengi wameoa amebaki peke yake hajaoa japo hayuko tayari kukaa na mke ndani ya nyumba so anaishia kuwa mtu wa baa na kuwa na marafiki anasahau wajibu wake kama mume ndani ya nyumba
Wengine wamelazimishiwa kama kuletewa mke au ile kuambiwa ni lazima umuoe mtoto wa fulani so umemuoa kutimiza ombi la wazazi ila moyoni mwako huyo mke huna mapenzi nae
Wengine mabadiliko ya tabia za wenza ambao tunafunga nao ndoa. Wako wengi sana wanaoficha makucha yao enzi za uchumba na kuja kuyatoa wakati wameshakuw amke na mume ndani ya nyumba
Kero kutoka kwa mwenzako ndani ya nyumba kunakopelekea upande wowote kuingia katika ulezi au kuwa na nyumba ndogo nyingi
Sasa haya yote na mengine mengi ni sababu ya marriage institution kuonekana ya ovyo kwa sasa japo kuna watu na wenza wako na marriage zao zinatimiza even 50 years wanaishi kwa amani japo ugomvi kidogo kidogo upo. Tuipe benefit of doubt bado marriage institution inastahili kuwepo na iendelee na kuwepo na semina na mafunzo ya mara kwa mara kwa wanandoa ili kuweza kuepusha kuiona marriage institution kama kitu kisicho na thamani licha ya umuhimu wake