Tupo katika wakati mbaya sana kwa sasa

Tupo katika wakati mbaya sana kwa sasa

CHIBA One

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2018
Posts
558
Reaction score
2,102
Maisha ya sasa ukiyatazama kichwa kinakuuma, ukifikiria tulikotoka na tunakoelekea hasa kwenye swala la Mahusiano na ndoa. Kupata mtu sahihi imekuwa ni tabu kama kuchimba almasi.

1. Tuna aina ya wanawake wanaopenda zaidi mapenzi ya vitu kuliko hisia (wanapenda kuona magari, gentlemen, zawadi, outing, pesa za wigi, simu nywele, kupangiwa nyumba KWAO HAYA NDIO MAHUSIANO.

2. Baada ya kuona hilo no 1. Tumepata vijana wanaochomekea sana, kuazima magari, na kuning'iniza funguo za magari kwenye suruali ili kuendana na hitaji la wanawake.

3. Tumepata aina ya wanawake wanaopenda zaidi kwenda dinner za kupelekwa na wanaume mahotelini, au hata kwenda kunywa soda ilimradi aonekane anakula bata sehemu kali kali kwenye mitandao.

4. Tumekuwa na wanaume wanaojitutumua kualika mabinti kwenye mahoteli ili kukidhi tamaa za mabinti (Hapa ni igiza tuigize) hakuna future wala uhalisia.

5. Mwanamke anaamua kupanga nyumba lakini pesa zinamuuma kulipa kodi, kwa hyo anatafta wa kulipa kodi, mwingine wa kulipia bili za maji na umeme (haijalishi mume wa mtu). Huyu binti baadaye unamsikia anasema kila mwanaume ni mbwa na hawaoi.

6. Tumekuwa na wanawake ambao ukichukua namba yake sasa, Itabidi utatue matatizo yake pale anapojisikia hata kama hujamtongoza.

7. Tuna wanawake ambao ndoa kwao ni zile make up, bridal shower pictures, makeki yenye ngazi na kucheza mziki kuonyesha mashosti zake kaolewa, baada ya hapo hataki kuacha maisha yake ya zamani, anataka aendelee kwenda kula dinner hotelini kama zamani.

Kwa hayo machache unaweza ukafikiria hao wake tunaowatafta tutawachimba wapi? Hizo ndoa zinazofungwa zitadumu kwa miujiza gani?

Wanadamu wamebadilika sana.
 
Maisha bandia yametawala kwa wanaojiita wasomi.

Ukitaka mke wa kujenga naye familia tafuta hata wauza mchicha, karanga, ndizi hao wanajua nini maana ya maisha na nini maana ya mume, achana na washinda Facebook, Twitter wanaopenda kupiga picha kwenye magorofa wakati kwao ni pangu pakavu.
 
Maisha bandia yametawala kwa wanaojiita wasomi.

Ukitaka mke wa kujenga nae familia tafuta hata wauza mchicha, karanga, ndizi hao wanajua nini maana ya maisha na nini maana ya mume, achana na washinda Facebook, Twitter wanaopenda kupiga picha kwenye magorofa wakati kwao ni pangu pakavu.
Naunga mkono.
 
habari za wanawake ni ndefu mno azina mwisho.

mimi nina rafiki yangu yupo chuo baba engineer mlezi wa ndoa ni baba askofu wa jimbo flan KKT ila mama amedai talaka mali zote wanaenda pasu kwa pasu baba askofu amlesuluisha sana bila mafanikio

baba ni mtu mpole sana ila mke wake alianza kujenga nyumba kwa siri akiofia mume wake atazaa nje watoto hawatapata mali.

kwanini mawazo ya mwanawake walio wengi wanawaza wanaume au mume wake ndo ataanza kufa kabla yake......?
 
Maisha bandia yametawala kwa wanaojiita wasomi.

Ukitaka mke wa kujenga nae familia tafuta hata wauza mchicha, karanga, ndizi hao wanajua nini maana ya maisha na nini maana ya mume, achana na washinda Facebook, Twitter wanaopenda kupiga picha kwenye magorofa wakati kwao ni pangu pakavu.
Naunga mkono hoja.
 
Hyo namba 7 imetamalaki inapelekea ndoa zinadumu miaka miwili chalii. Watu wanaoniboa ni hawa wanaojiita ma celebrities hivi wanaolewaga au kubadili.dini na kuolewa kwa fashion ama? Leo mtu kabadili dini kaitwa Husna sijui Zulekha anafunga ndoa baada ya miezi 6 unasikia ndoa imeisha na ukimuhoji utasikia mm ni Jackline Wolper haitakaa itokee nibadili dini au mm ni Irene uwoya wakati alibadili na shekhe akafukizia ubani kama hawataki laana hawa ni nini?

Watabakia kudanga mpaka nyama za mwili ziwaporomoke maana Mungu hadhihakiwi kwa kiapo chochote kile.
 
Maisha bandia yametawala kwa wanaojiita wasomi.

Ukitaka mke wa kujenga naye familia tafuta hata wauza mchicha,karanga,ndizi hao wanajua nini maana ya maisha na nini maana ya mume, achana na washinda Facebook, Twitter wanaopenda kupiga picha kwenye magorofa wakati kwao ni pangu pakavu
"Mwanangu, hivi unadhani kwanini nilimuoa mama yako wa darasa la saba, wakati mimi ni msomi mkubwa?"

Kwa kutumia kauli hii ya mzee wangu, ndiyo maana kigezo changu cha kwanza kumtafuta mke wa kuoa siyo elimu yake.
 
Hatari sana mkuu maisha yamebadilika sana utandawazi umeshika kasi.
 
Back
Top Bottom