Tupige vita kuwanyanyapaa waliopata div zero mashuleni

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
17,080
Reaction score
12,300
Ni kwa muda sasa umekuwepo unyanyapaaji mkubwa kwa watu wanaoshindwa masomo ya sekondari maarufu kama ''div zero''

wanaitwa kila majina ya hovyo kama wamezungusha vilaza na mambo ya ajabu ajabu.

Kwanza sio kweli wanaofeli sekondari basi hawawezi chochote maishani kana kwamba ni ndondocha au mataahira.

Wapo waliofeli kwa kukosa maandalizi mazuri ikiwemo upungufu wa madarasa walimu na vifaa vya kufundishia kama maabara etc.

Sasa kusema fulani kazungusha kana kamba katenda jinai hapana ifike wakati sasa tukatae namna hii ya unyanyapaa na ifike sehemu watoto wakifeli wazazi wawashitaki walimu na wadai fidia. Ni jukumu la mwalimu kumfdundisha mtoto nani dhamana yake.
 
Ila nduguyanguuu kuna watu tumesoma mazingira magumu sana na misuli yatima na kumuomba mungu tukapata angalauuu si haba sasa unataka kuwafunza nini wadogo zetu usitetee ujinga msingi wa kupata zero uliujenga mwenyewe
 
upo sahihi ndg, tuna wazazi na ndg ambao hata sekondari hawajafika na tunatumia busara na hekima zao.mhm tu ni kuwa mtu aliyepata zero bila kujiendeleza asitumike kwenye mambo yanayohitaji elimu kubwa lkn kwenye aspects zingine za maisha bado ni mhm.
 
Wengi waliibia na wengi walifaulu kwa kutumia vibomu kwenye mitihani na paper fake wengine ndio zimewatoa
 
Baba J mwenyewe aliwanyanyapaa,nashangaa huyu amemkumbatia
 
Ila nduguyanguuu kuna watu tumesoma mazingira magumu sana na misuli yatima na kumuomba mungu tukapata angalauuu si haba sasa unataka kuwafunza nini wadogo zetu usitetee ujinga msingi wa kupata zero uliujenga mwenyewe
eti msuli yatima...umenkumbusha mbali jamaa
 
Ni kwa muda sasa umekuwepo unyanyapaaji mkubwa kwa watu wanaoshindwa masomo ya sekondari maarufu kama ''div zero''

wanaitwa kila majina ya hovyo kama wamezungusha vilaza na mambo ya ajabu ajabu.

Kwanza sio kweli wanaofeli sekondari basi hawawezi chochote maishani kana kwamba ni ndondocha au mataahira.

Wapo waliofeli kwa kukosa maandalizi mazuri ikiwemo upungufu wa madarasa walimu na vifaa vya kufundishia kama maabara etc.

Sasa kusema fulani kazungusha kana kamba katenda jinai hapana ifike wakati sasa tukatae namna hii ya unyanyapaa na ifike sehemu watoto wakifeli wazazi wawashitaki walimu na wadai fidia. Ni jukumu la mwalimu kumfdundisha mtoto nani dhamana yake.
Aisee umesema vyema kabisa, tusiwanyanyapae nayo ni matokeo kama matokeo mengine hata Mungu anajua! ila ikitokea matokeo yako hivyo usinunue cheti cha mtu aliyefaulu utaumbuka! Fanya jitihana ktk mambo mengine au hata kurudia masomo/mtihani nayo ni njia nzuri zaidi, kuna watu wengi wamefanya hivyo wakatoboa na kutimiza ndoto zao. Never give up!
 
Yaani poote umenena, lakini ulivyosema kumshitaki mwalimu kwa zero ya mwanafunzi hapo si busara!
Kila lawama ni kwa mwalimu.

Mimi naamini kufaulu kwa Mwanafunzi ni juhudi zake mwanafunzi. Japo asilimia kadhaa ni kwa mwalimu, mzazi na serikali kiujumla!
 
Huyu naye sijui kala maharage ya wapi,watu wanapinga ubashite(ziro) kwa nguvu zote halafu wewe unausapoti.Poor thread.
 
Ni kwa muda sasa umekuwepo unyanyapaaji mkubwa kwa watu wanaoshindwa masomo ya sekondari maarufu kama ''div zero''

wanaitwa kila majina ya hovyo kama wamezungusha vilaza na mambo ya ajabu ajabu.

Kwanza sio kweli wanaofeli sekondari basi hawawezi chochote maishani kana kwamba ni ndondocha au mataahira.

Wapo waliofeli kwa kukosa maandalizi mazuri ikiwemo upungufu wa madarasa walimu na vifaa vya kufundishia kama maabara etc.

Sasa kusema fulani kazungusha kana kamba katenda jinai hapana ifike wakati sasa tukatae namna hii ya unyanyapaa na ifike sehemu watoto wakifeli wazazi wawashitaki walimu na wadai fidia. Ni jukumu la mwalimu kumfdundisha mtoto nani dhamana yake.
Umeanzisha kampeni za kumtetea Bashite au?
 
Kupata 0 sio issue ya kufanya watu wakunyanyapae, tatizo ni unapotaka kudanganya kuwa ulchopata ni kingine, tatizo ni mheshimiwa kuwaita vil.aza. Lakini kushitaki walimu ni ngumu sanalabda kama darasa zima limepata 0 na umewapa walimu environment nzuri ya kufundishia pamoja na vijana wazuri. Bila kuathiri niliyo yaandika kuna wengine wetu ili wajioneshe waliposimama husema wengine vibaya (majivuno).
 
hapana sikubaliani na wewe, jiulize mwaka jana azania ilishika mkia wakati shule inawalimu zaidi ya wale wanaohitajika kitaalamu inakila nyenzo tena iko mita chache kutoka makao makuu ya wizara hapo walimu na maafisa elimu lazima wabebe lawama za kufeli kwa watoto.
 
Aisee umesema vyema kabisa, tusiwanyanyapae nayo ni matokeo kama matokeo mengine hata Mungu anajua! ila ikitokea matokeo yako hivyo usinunue cheti cha mtu aliyefaulu utaumbuka! Fanya jitihana ktk mambo mengine au hata kurudia masomo/mtihani nayo ni njia nzuri zaidi, kuna watu wengi wamefanya hivyo wakatoboa na kutimiza ndoto zao. Never give up!
hebu tizama mitihani ya warudiaji maarufu kama QT 99.9% wanafeli huyohuyo akinunua jina la mtu anafaulu hatujiulizi kuwa hapo kuna dosari? iweje mtoto yuleyule akifanya mtihani kwa jina jingine afaulu na akifanya QT afeli?
 
Wengi waliibia na wengi walifaulu kwa kutumia vibomu kwenye mitihani na paper fake wengine ndio zimewatoa
hao si ndio mnaita degree za chupi? halafu haohao ndio wakwanza kuwacheka wenzao.
 
mkuu makazini utawajua yaani wanakuwa hawana idea kabisa wanapopata challenge even lugha...
 
Back
Top Bottom