Tupige kelele sekta ya afya (sauti ya wengi sauti ya Mungu)

LWENYI

JF-Expert Member
Jul 4, 2013
1,784
2,097
Habari ya majukumu wakuu.

Natumai kila mtu anaendelea vyema na majukumu yake na poleni kwa wale wote ambao afya zao zina mushkeri kwa namna mbali mbali Mungu awanyooshee mkono mkarudie hali zenu mapema.

Leo naomba nichangie na mimi mawazo yangu kuhusu sekta hii muhimu ya afya hapa nchini, ili taifa liwe na watu wa kufanya kazi lazima serikali na wananchi wenyewe wawekeze kwenye kulinda na kuboresha afya zao.
Na inapotokea lolote kwa mwananchi kuyumba ki afya naamini pia serikali inawajibika kuchangia kiasi kwa watu hawa kupitia reliefs mbali mbali zinazotakiwa kutolewa katika hospitali za umma hii ni kwasababu wote tunalipa kodi, relief hizi naamini zitakua zenye tija sana ikiwa zitaelekezwa kwenye kwenye dawa, huduma za kulazwa pamoja na vifaa tiba.

Leo naandika haya kuhoji serikali kama je? wanaona ni sahihi kwa hospitali kubwa za serikali kama muhimbili kuwa na viwango vikubwa vya bei ya kitanda kwa mgonjwa aliyelazwa kufikia Kiwango cha shilingi elf 30,000/ kwa siku?= kiwango hiki ni kikubwa sana kwa mwananchi wa kawaida ambaye amepewa rufaa kadhaa kutoka simiyu mpaka kuja kufika muhimbili kwaajili ya kutafuta matibabu tu.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba bei hiyo haijumuishi chakula wala dawa ni gharama za kulala tu, bei inayotozwa na hoteli kubwa tu hapa mjini siku hizi, inafikia mahali hata maiti huzuiliwa kutoka mpaka deni lilipwe, hivi serikali ya wanyonge wa Tanzania hii iko wapi? ikiwa mwanafunzi wa Hosteli mpya za Chuo kikuu analala kwa chini ya shilingi elfu moja kwa siku je? ni halali kwa mgonjwa kulala kwa zaidi ya elf 30 kwa siku?

Maoni yangu, Bei ya kumlaza mgonjwa izingatie yafuatayo
-Gharama za umeme
-Gharama za ufuaji wa mashuka
-Garama za usafi wa wodi
-Gharama za ulinzi

kiwango cha juu kabisa kumlaza mgonjwa kwa siku kulifaa kuwa angalau elf 12 tu kwa siku
serikali izipe ruzuku ya kutosha hospitali zetu ili zisitegemee mapato ya wagonjwa tu kujiendesha hii itapunguza adha hii.

wenu katika kazi,
LWENYI.
-
 
Back
Top Bottom