maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Inasikitisha kuona Chuo cha uongozi wa mahakama cha Lushoto kilichokuwa kinaheshimika kwa kutoa wasomi wazuri wa taaluma ya sheria katika ukanda huu wa Afrika Mashariki leo hii kinafikia hatua ya kutoa wafaulu ambao ni theluthi moja ya wanaofanya mitihani.
Kwa mfano mdogo tu, nimegundua kwamba matokeo ya semesta ya kwanza ya mwaka huu kwa kozi za cheti na diploma mwaka wa kwanza ni madudu matupu, waliosupp na disco ziko kibao kiasi kwamba nimeshindwa kuelewa tatizo ni nini? Ni walimu, ni wanafunzi, ni mazingira ya chuo yamebadilika au chuo hakina nyenzo nzuri za kufundishia, kwa maana ya vitabu vya ziada, kiada na rejea.
Kwa kifupi kuna haja kubwa ya wizara ya sheria kuingilia na kutafuta kiini cha mdororo wa chuo hiki kitaaluma badala ya kukaa kimya na kuangalia mambo yakiharibika.