Makau Js
Member
- May 25, 2017
- 93
- 233
Mwalimu wa somo la kiingereza toka china-Ma Yun a.k.a Jack Ma, Episode ya 1.
Siku moja mwalimu anayefundisha somo la Geography aliwaambia wanafunzi wake kuwa ukitaka kuijua nchi yako ya China vizuri ,inakulazimu usome kwa ufasaha somo langu la Geography.
Pia unatakiwa utengeneza ukaribu wa lugha ya Kiingereza ili uwe balozi mzuri wa taifa letu ,ili mgeni yeyote atakapo kuuliza swali lolote kuhusu nchi yetu umjibu kwa ubora wa ufahamu wako wa lugha ya kiingereza na utajiri wako wa maarifa ya Geography ya china.
Kauli hii ilipenye kwenye masikio ya Ma Yun-Jack Ma,na kwenda nyumbani kwao kuchukua kiasi cha pesa six mao,ambayo ni sawa na USD 2, na kwenda kununua radio ya kusikiliza station zinazo zungumza lugha ya kiingereza kila siku.Wakati huo Jack Ma alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili.
Wazazi wake walikuwa hawana uwezo hata wa kuandika sentensi moja kamilifu ya lugha ya kiingereza kitu ambacho kilileta changamoto kwa mtoto mwenye umri wa miaka 12 mwenye njaa ya kujifunza maarifa na lugha ya kiingereza.
Jack Ma alizaliwa katika mji wa Hangzhou, Zhejiang, China ,sehemu ambayo kuna ziwa ambalo lilikuwa kivutio cha watalii wanaotoka sehemu mbali mbali duniani,Jack Ma alipenda kwenda kushinda kwenye ziwa hilo ili kufanya mazoezi ya kuzungumza lugha ya kiingereza na wageni.
Akiwa na umri wa miaka kumi na mbili Jack Ma alipenda sana kusoma novel za Wuxia -(武俠 yenye maana ‘’Martial Artists ‘’ hii ilimfanya kuwa mtoto mgomvi asiyekubali kuonewa na mtu yeyote yule sababu ya kuwa na mazoezi ya Martial Arts na kuujua mchezo huu kwa ufasaha Zaidi.
Darasani alifanya vyema sana kwenye somo la kiingereza na kutengeneza uadui na somo la hesabu ,alikuwa analichukia somo la hesabu na somo la hesabu lilijua kuwa halipendwi na Jack Ma.
Moja ya taratibu ya nchi ya China miaka ya 1978, iliwalazimu wanafunzi wote wanao taka kujiunga na elimu ya juu kuwa na ulazima wa kufanya vyema somo la hesabu ,ndio unapata nafasi ya kujiunga na elimu ya juu.
Mwaka 1978 watu 5.8 Million waliomba nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu ,ila waliofanikiwa kujiunga vyuo vikuu walikuwa ni watu 402,0000 pekee ,hawa ndio waliokuwa na urafiki na somo la hisabati na kupata nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu .Jack Ma na Martial Arts yake alishindwa sababu hakuwa na urafiki na hesabu.
Baada ya kuomba nafasi za kujiunga na masomo ya elimu ya juu Zaidi ya mara tatu na kushindwa zote ,Professor Yu ,alimuambia Jack Ma, kuwa uwezo wako wa kufaulu somo la hesabu ni mdogo sana,kama ikitokea umefanya vyema somo la hisabati ,naahidi kuandika jina langu kinyume nyume.
Mwenyezi Mungu akitupa uzima na afya tutaendelea kumsoma Mwalimu wa lugha ya Kiingereza toka China fundi wa mchezo wa Martial Arts katika Episode ya Pili.
Darasa:Tumia akili yako kufuata mafundisho;tumia masikio yako kusikiliza maarifa -