Tuongee vizuri; Hii ni sababu kwanini hupati mume/mke

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
7,923
13,402
Salamu waungwana
Mapenzi na mapendo yadumu.

Nisichukue muda wako mwingi, ngoja nikwambie moja ya sababu kwanini haupati mume au mke japo umeweka jitihada nyingi katika hili.

Hivi hujawahi kukutana na mtu yaani mkaelewana kweli kweli na hata kupendana lakini ikatokea tu mkapotezeana yaani mkaachana bila ata kujua kulikoni.

Ndiyo hali hiyo hiyo umemkumbuka uliyekuwa naye katika hali hiyo ee!?, safi. Basi ngoja nikwambie moja ya sababu zinazosababusha hiyo hali. Najua utaishangaa na itakupa hofu kiasi ila isikutishe sana inaweza kuepukika.

Ipo hivi, moja ya sababu watu wengi wanashindwa kupatana na wenza wao wa maisha ni kiwa wanakuwa tayari wamefungamanishwa na uhusiano wa wenza wengine wa maisha. Hapa nimekuchanganya kidogo si ndiyo?, basi usiogope nafafanua;

Ni kwamba watu wengi wanaonekana kuwa wameshaolewa katika ulimwengu wa pili (roho) na hii inasababishwa na wazazi kufunga ndoa wakati mwanamke ni mjamzito. Tambua kuwa kufunga ndia wakati wewe ni mjamzito au mkeo ni mjamzito ni kumuingiza mtoto wenu kwenye ndoa yenu kitu ambacho hakimuhusu kabisa. Mtoto anatakiwa kuzaliwa akiwa huru bila ahadi zenu hizo za shida na raha.

Sasa kama wakati wazazi wako wanafunga ndoa wewe ulikuwa ni ujauzito hii ni sababu kwanini hadi leo hujapata mtu wakukuoa au kumuoa mbali ya kuwepo na kujitokeza watu wenye nia ya kuingia kwenye ndoa na wewe.

Pole sana, najua sasa umepata sababu nyingine katika sababu zako za kwanini hujafanikiwa kuingia kwenye ndoa. Sasa anza kuifanyia kazi. Anza kujikomboa kutoka kwenye ahadi isiyokuhusu ndugu yangu.

Baada ya kujua kuwa kufunga ndoa mjamzito ni kumhusisha mtoto wenu na matatizo yenu sasa na wewe usioe au kuolewa ukiwa mjamzito.

Unaweza shangaa mtoto anamchukia mzazi wake watu mkahisi mtoto ana laana au anavuta bangi (japo bangi haipo hivyo) kumbe ni kuwa roho yake ipo kwenye mgogoro mkubwa na ninyi wazazi wake msiotimiza ahadi mliyomshikamanisha nayo ya raha na shida.

Basi ngoja mimi niishie hapa kwa leo, uzima ukiwepo nitakuja kuwaeleza jambo lingine.

Usiku mwema wana JF
 
Na haya ndiyo baadhi ya matatizo ya walokole
Yaani ndoa wafunge baba na mama,kifungo akipate mtoto wa tumboni?

Nehiiiiiiii....!!!​
 
Kuna ukweli ndani yake.
Sio vizuri wenzi kufunga ndoa kama mwanamke Ni mjamzito.
Mnamuingiza Mtoto kwenye agano
 
Back
Top Bottom