MAGUFULI AKAHUTUBIE KISWAHILI UN.
Lugha rasmi zinazotambulika UN ni sita (Arabic, Chinese, English, French,Russian, Spanish,) Lakini anaruhusiwa kiongozi kutumia lugha yoyote ili mradi lugha hiyo itafsiriwe kwenye moja kati ya hizo sita rasmi.Nchi kadhaa zimeomba lugha zao zikubalike kuwa rasmi,HAZIJAFANIKIWA HADI SASA.HATA WAKOLONI WA KIRENO LUGHA YAO SI RASMI !!!
SISI watumizi wa Kiswahili kwa sasa tusijiingize katika mlolongo wa kutaka lugha yetu iwe moja katika hizo rasmi.TUGOMBANIE TU RAIS MAGUFULI(au Kiongozi yeyote wa Afrika mashariki)AKATOE HUTUBA KWA KISWAHILI.
Ataehoji kwa nini tunahangaikia kutumia Kiswahili wakati tuna matatizo mengine muhimu ya kuyazungumzia jibu lake ni kuwa “UTUMWA WA KILUGHA UNAATHIRI NYANJA NYINGINE”
Viongozi wengi wanatumia lugha za kwao pamoja na kuwa wanajua kiingereza, kwa nini na sisi tusitumie Kiswahili chetu?
Umefika wakati wa kujinasua na “UTUMWA WA KILUGHA”