Tuongee Asubuhi Live Ijumaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuongee Asubuhi Live Ijumaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Paul Mabuga, Jan 20, 2012.

 1. P

  Paul Mabuga Verified User

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gharama za Umeme nchini zimepanda tangu tarehe 15 Januari, 2012. Tanesco walitaka kupandisha kwa asilimia 155 kwa hati ya dharula lakini EWURA wamepitisha zaidi ya asilimia 40 kama ongezeko. Je kuna justification ya kupandisha gharama hizi? Je baada ya kupanda --- nini athari kwa mlala hoi --- Tanesco watafikia malengo yao ya kufuta mgao na kuongeza wateja wapya? ........ na Je hakuna mbinu zozote mbadala za kukabiliana na changamoto za Tanesco zaidi ya kuongeza ankara kila Mara.

  Tutakuwa nma wageni kutoka EWURA hapa Star TV ; Tafadhali changia Mada hii
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Watuambie kwanza wamepokea sababu zipi za kuhalalisha maombi hayo ya TANESCO?

  Je, TANESCO hawakuwa na njia nyingine ya kukabiliana na matatizo ya kifedha?
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,676
  Trophy Points: 280
  Ewura hawana faida kwa watanzania maskini ambao ndio asilimia kubwa.taasisi kama Ewura kwa bajeti yake na utendaji wake ni hasara kubwa.wana negotiate price kwa kubase kwenye economics indicators ambazo hazimgusi mtu wa kawaida.kama mlo tu tabu tutaweza kulipia ongezeko la hizo gharama? Mashirika ya umma yanapaswa kupewa ruzuku ya kutosha na serikali ili kusaidia walalahoi.
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,676
  Trophy Points: 280
  Hatuoni Ewura ikitoa mapendekezo kwa serikali kulingana na hali halisi ya wananchi kukabili maongezeko kama haya.hatujakomaa kiasi cha kuweza kupangiwa bei za ajabu kwa kisingizio za gharama kupanda.EWURA mnao mwongozo wa utendaji lakini mnapaswa kuishauri serikali hatua za kuchukua.
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,676
  Trophy Points: 280
  EWURA wanapopanga bei wanachambua sababu ya kutaka kupandisha kwa kupima na hali halisi prevailing in the particular industry lakini hawaangalii yule mkulima wa mboga mboga Mbulu ataweza? Mbona hatusikii wakiiambia serikali waongeze ruzuku kwa mashirika haya ili kufidia hilo ongezeko? Mbona hawawabani mashirika husika kama Tanesco waboreshe utendaji ili waweze kujimudu? Uzembe wa watendaji tulipe sisi wananchi? Kabla hamjakubaliana bei huwa mnachambua mbinu wanazotumia kuongeza mapato kwa kupunguza uzembe? Je huwa mnawapa recommendation ambazo wasipozifanyia kazi hawataruhusiwa kupandisha bei tena?
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,676
  Trophy Points: 280
  Siamini kama EWURA kazi yao ni ku regulate price tu bali na kuyashauri mashirika husika pamoja na serikali.EWURA jicho lenu liwe kwa maskini jamani!
   
 7. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  EWURA wala sijui faida ya kuwepo kwake,ni ama hawajui wajibu wao,ama wanafanya ujinga uliozoeleka wa kuwafurahisha wana_siasa kwenye mambo ya kiutendaji,.....wanafuja pesa ya walipa kodi bila tija yoyote,...i wish msingewaalika kwenye mjadala kabisa..............hawana meno hao.
   
 8. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mabuga wengine tulibanwa a waajiri, vipi kipindi kimeishaje? Ufafanuzi wa EWURA umewaridhisha wafuatiliaji?
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nasikitika sana kwani kwa kupandisha bei za nishati za umeme atakayeathirika ni mlaji au mlalahoi wa kawaida. Kiuchumi naweza kusema kuwa litaua kabisa viwanda vidogo vidigo vyote kwani bidhaa zake zitashindwa kuingizwa katika ushindani na hivyo kudoda.

  Kumbukeni kuwa Tz mnafuata soko huria. Bila serikali kutumia a kulinda viwanda vyake basi vitu vya nje vitauzwa saaana.
  Lazima muwe makini sana kukuza uchumi wenu wa ndani na sio kuwa soko la bidhaa za nje.
   
 10. P

  Paul Mabuga Verified User

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kombo
  Re: Tuongee Asubuhi Live Ijumaa
  Mkuu Mabuga wengine tulibanwa a waajiri, vipi kipindi kimeishaje? Ufafanuzi wa EWURA umewaridhisha wafuatiliaji?

  Kombo, tuliwaachia wadau zaidi kuamua kutokana na kile kilichoelezwa na kuchangiwa. Pengine ni vema walioangalia kipindi wakatoa hitimisho! Lakini kimsingi suala bado linahitaji mjadala, hasa baada ya wachangiaji kuonesha njia mbadala za kukabiliana na changamoto za TANESCO badala ya kupandisha bei ya ankara za umeme.

  Nawashukuru Waungwana wote waliochangia na hata kusoma thread. Heshima mbele na Wiki end njema.
   
Loading...