Tununua bidhaa kutoka wa wamachinga pia.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tununua bidhaa kutoka wa wamachinga pia....

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Madevu, Apr 19, 2010.

 1. M

  Madevu Member

  #1
  Apr 19, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuwashauri ndugu zangu tuwe na utamaduni wa kununua bidhaa kutoka kwa Wamachinga au vijana wa mitaani, sababu kubwa ni kama ifuatavyo;
  1. kuunga mkono kazi zao ili wasikate tamaa ya maisha
  2. kuwawezesha kiuchumi,
  3. kuleta usalama katika jamii, kwa kuepusha wezi na majambazi
  4. kuwatengenezea ajira maana hatuwezi kuwawezesha wote, basi hawa wanaojitoa na vibishara vya mkononi tuwaunge nao mkono...
  5. ni Uzalendo pia.....

  vijana wengi ni wenye afya na nguvukazi kwa taifa kama kungekuwa na shughuli ya kuwapa wafanye lakini tunawaona wanauza maji,chewing gums,magazeti...nk...unaweza kujiuliza kijana mpaka auze chewing gum ngapi apate pesa ya kula kwa siku, au chupa ngapi za maji lakini ameona inamtosha kufanya hivyo, kwahiyo tunapaswa kuwapa pia matumaini kwa njia tofauti za kuonyesha tunawajari na hata kama serikali ina kitu inaweza kusaidia au kuwatumia vijana hawa basi wawakusanye na kuwasaidia.

  pia suala la watoto wa mtaani limeongezeka kwa kasi sana, linabidi tuliangalie, watoto wanaokaa kwenye trafik light na kujifanya wanaosha magari wameongezeka sana hasa pale ubungo, kwakuwa hatuna msaada wa kuwapa basi kama unachochote wape tu na kama kuna sehemu unajuwa wanaweza kupelekwa basi toa ushauri, mimi niliwahi kuchukua mmoja lakini akanitoroka baada ya kuanza kufuatilia utaratibu wa kutaka kupata kibali cha ustawi wa jamii ili niishi nae akaona labda nawatafuta wazazi wake ili arudi kwao.....

  saidia maskini, Piga vita umaskini kwa vitendo...
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huo ni uzembe wa serikali kwani nchi zingine wanafanyaje kupunguza watoto wa mitaani?? Unasema tununue vitu kwa wamachinga....ndiyo watu wananunua lakini ukshauziwa maji ya mtaroni kwa kuchukua chupa na kuiziba kwa moto halafu ukiharisha hutarudia kununua maji yao na ndo maana wengi wameacha kwani vijana wale wengi siyo waaminifu.

  kuhusu omba omba pale ubungo nadhani jamii ikiamua kutowapa cho chote na kwa chapa bakora hutaona mtu pale ni kwa sababu tu Tanzania mambo ni tambarare...mtu anazaa mtoto akitegemea ataomba na atapewa.
   
Loading...