Tungo: Ua langu jamani...

nentewene

Senior Member
Jun 9, 2017
144
94
Ua langu limechumwa- bila mimi kujua..
Moyo wangu unauma- natamani kujiua..
Amekosa huruma- ua langu kunyakua..
Hivi nan kamtuma- leo hii naugua....

Ua lilinawairi- kila mtu alidata..
Haikua tena siri- ua lilitakata..
Uzuri wake wamwili- vigogo walimtaka.
Utamu wake samsuri- watu wakamteka..

Leo hii nalia -ua limenitoka..
Bora lingejifia- kuliko kutoweka..
Nakosa wa kukumbatia- toka ua kuondoka
Ua limekimbia nimebaki nimechoka..

Nilinyunyizia maji ua langu la thamani
Likapata walaji wanaokula hadi ndani..
Nimekua mfamaji cjui nakosa nin..
Hawa watu wauwaji cjui wataisha lini?

Kila mtu anawake- niachieni ua langu..
Msifanye niteseke kweny huu ulimwengu..
Kila mtu ale chake tusije tiana pingu..
Ua langu ua langu tena nalia kwa uchungu...
 
Back
Top Bottom