Tungekuwa mbali leo bila Rais Samia

Ofisi gani yenye bil 57 tena? Mie kapuku.

Report tunatoa sisi wenyewe wananchi kupitia serekali yetu. Sasa ukisoma Dira 2025, FYDP 1 & 2 huoni wapi mnapotushika pabaya?

Na bado bungeni mnasema nchi haiwezi kuendelea hii haina dira😂😂😂😂.

hapana mzee gdp ya kenya ni 300b au unasemaje binti salum?
 
Jitahidi ufunguke kiakili ili ondokane na imani ya kipekee unayompa JPM hata baada ya kuaga dunia karibu mwaka umeshapita. Vyote vimo ndani ya ilani, wanasema kujenga madaraja wakimaanisha yote, liwe la ubungo liwe la kule rusahunga Ngara.

Wanasema watatoa ajira milioni nane, hawawezi kuziweka wazi, zipo njia nyingi za kufanikisha upatikanaji wa ajira hizo.

Ilani huongea vitu vya jumla, utendaji hutegemea na upatikanaji wa pesa kutokana na vyanzo mbalimbali.

kwahio ile 27 ya umeme iliandikwa wap? na mbna imekuja kubadilika ama walibadilisha ilani?
 
Je,Tanzania ingekuwa wapi kama ingepata kiongozi mzalendo?

1: Uchumi wa Tanzania ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu Rais S.S.H aingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21 ; Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22 ; Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
 
Hivi hii mikataba aliosaini Mwigulu jana na yule DG wa TADB, zimepitia kwa Professor Aidan John Mwaluko?
 
Tulia dawa ikuingie wewe
Mambo hayako upande wako ndio maana kelele nyingi acha mama afanye kazi. Ana miezi kadhaa mnaanza kuleta gubu
 
  • Thanks
Reactions: Tui
kwahio ile 27 ya umeme iliandikwa wap? na mbna imekuja kubadilika ama walibadilisha ilani?
Ufafanuzi uliwekwa hadharani. TANESCO wakimtoza kila mteja tshs 27,000 ya umeme shirika litafilisika, wamebaki wateja wapya wa vijijini tu ndio wanaotozwa pesa hiyo.
 
Ufafanuzi uliwekwa hadharani. TANESCO wakimtoza kila mteja tshs 27,000 ya umeme shirika litafilisika, wamebaki wateja wapya wa vijijini tu ndio wanaotozwa pesa hiyo.

kidogo akili inakujia sasa, uelewe navyokwambia ubora wa kiongozi sku ingine
 
Huu ujinga unaweka hapa mbona huweki na madarasa yaliyojengw akila mkoa binadamu hamueleweki mnataka nini alikuwepo JPM mkawa hamumtaki sijui mantaka muongozwe na nani.
Labda pale alipoweka TOZO ndo angeendelezea.
 
Wewe ni msukule tu na hauna uelewa. Magufuli ameharibu uchumi wetu na kuturudisha nyuma miaka 20. Kukopa kuna limit yake ila Magufuli alikopa kiasi kwamba makusanyo ya ndani yaliishia kulipa riba na deni na ndiyo Lisa wafanyakazi wakakosa ongezeko la mishahara kwa miaka 5 mfululizo.

Task Force kinadharia uko sawa lakini kiuhalisia wa Magufuli likikuwa ni genge la unyang'anyi. Kuna fedha zilikwenda Serikalini lakini kuna zingine waligawana wenyewe including Magufuli
Asiyejua au asiyefahamu na mbaya zaidi akiwa na CHUKI BINAFSI, siyo rahisi kuelewa kuwa HAJUI kwani amegubikwa na ushabiki wa kisiasa uliojaa na unaoongozwa na hizo chuki binafsi ambazo msingi wake ni chuki za kisiasa. Sina cha kukusaidia zaidi ya kusema POLE SANA!
 
Back
Top Bottom