Tunduma kwawaka moto

Tunduma kwawaka moto

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,945
Reaction score
4,499
Yametokea mapigano makali kati ya polisi na raia mji mdogo wa Tunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia mida hii chanzo cha vurugu hizo kainzi ketu bado kanadodosa.
 
Last edited:
Du mkuu huko kuna jamaa zangu kibao wanapiga dili pale mpakani...ngoja nimpigie moja wao!
 
Du mkuu huko kuna jamaa zangu kibao wanapiga dili pale mpakani...ngoja nimpigie moja wao!

Dah mkuu maduka yamefungwa na watu wanakimbia kimbia ovyo.
Chanzo ni kwamba polisi wamemuua mfanyabiashara usiku kwa kumpiga risasi wakijua jambazi alikuwa anarejea toka kuangalia mpira.
 
Inaelekea hapo Tunduma kuna matatizo, kwa vile hii siyo mara ya kwanza kutokea vurumai. Pafanywe utafiti kujua chanzo cha matatizo hayo ili kupata fumbuzi wa kudumu.
 
Magari ya mbio za Mwenge yamehifadhiwa kwenye soko la kimataifa wanasubili vurugu zitulie naona watakuwa wanasubili kikosi kazi toka Mbeya. Magari ya serikali yamekimbizwa eneo la tukio hakuna lililo pasuliwa kioo.
 
Shughuli zote za kibiashara zimesimama maduka,hoteli,migahawa,guest house vyote vimefungwa watu wanarejea majumbani kusubili khali iwe shwari.
 
Nasikia chanzo vurugu hizo ni wananchi kuvamia kituo cha polisi baada ya mfanyabiashara mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi, wenye habari zaidi kuhusu kinachoendelea huko waendelee kutujulisha
 
Jamani utaratibu na mbinu za kumukabiri jambazi kwa polisi wetu siku hizi zimebadilika? Mbona siku hizi haya matukio ya raia kuuwawa kwa kudhaniwa ni majambazi yameongezeka? Mlio na taarifa kuhusu hili tujulishane ili kujihami mapema hata kwa kurudi majumbani mapema.

Je hakuna utaratibu kwa polisi wetu ni wakati gani watumie silaha wakati wa kumkakata mtu au mtuhumiwa? Tusaidiane manake sasa hili nalo linatakuwa jambo la kawaida tu, kusikia mtu kauwawa kwa kudhaniwa ni jambazi, mbaya zaidi na polisi wetu, au kuna jambo nyuma ya hilo tukio kati ya polisi muhusika na muhanga wa tukio hilo, manake polisi nao tumijichanganya mno nao huku mitaani kwetu.
 
Bado Watanganyika hamjaweza kupambana na polisi kama WaPemba ila kwa kuwakumbusha ndugu zangu wa Polisi tu kuwa kuna msemo wa zamani usemao Ngoma au tarumbeta ikipulizwa Zanzibar basi walioko huko Mwanza na kwengineko hucheza.
 


Mkuu kwa leo hali ya amani imerejea.
Lakini cha kushangaza polisi wametoa report yao wanadai yule mfanyabiashara alikuwa miongoni mwa majambazi ambapo sio kweli jamaa alikuwa bar anaangalia mpira baada ya kusikia milio ya risasi akachukua gari lake akaanza kukimbia kunusuru maisha yake. Majambazi walivamia karibu na eneo alipo kuwepo huyu marehemu akiangalia mpira.
 
Hakika hayo yote ni matatizo ya polisi kukosa umakini na kutokuwa waadilifu ka jamii.

Poleni sana tunduma

Nasriyah.
Mapumzikoni Mwera. Znz
 
Askari adaiwa kuua mfanyabiashara
*Barabara Tunduma zafungwa kwa saa 9
*Wananchi wavunja magari JWTZ,ofisi RC
*Mbio za Mwenge wa Uhuru zasitishwa
* Risasi zarindima, kituo chazingirwa

MJI Mdogo wa Tunduma uliopo mpakani wa Tanzania na Zambia jana uligeuka uwanja wa vita baada ya mamia ya wananchi kuandamana, kurusha mawe na kushambulia magari kushinikiza Jeshi la Polisi kuwajibika baada ya mmoja wa askari kudaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mfanyabiashara wa kitongoji cha Sogea Bw. Frank Mwachembe (34).

Mfanyabiashara huyo aliuawa kwa kupigwa risasi ubavuni saa nne usiku wa kuamkia jana na askari aliyefahamika kwa jina la PC Justin, mita chache kutoka nyumbani kwake.

Wananchi hao wakiwemo wafanyabiashara wa mji huo wa Tunduma, walikuwa wakiandamana kuelekea kituo cha Polisi wakiwa na mawe kwa nia ya kumuua askari anayedaiwa kusababisha mauaji hayo huku wakisema jeshi hilo limekuwa
likiacha majambazi na kuwaua raia wasio na hatia.

Hata hivyo askari huyo baada ya tukio hilo alitoweka na hajulikani alipo hadi sasa.

Hatua hiyo ilisababisha barabara kuu ya Tunduma kufungwa kwa takribani saa tisa kutokana na vurugu hizo ambapo mbio za Mwenge wa Uhuru uliokuwa ukimbizwe eneo hilo zilisitishwa.

Inadaiwa kuwa askari huyo alikuwa akifuatilia tukio la ujambazi ulitokea Tunduma hivi karibuni na mara alipoona gari la mfanyabiashara huyo lenye namba za usajili T 888 AEA, Toyota Cheaser ambalo alikuwa akiendesha mfanyabishara huyo alianza kulifukuzia kwa nia ya kulikamata.

Taarifa zimeelezwa kuwa wakati askari huyo akilifukuza gari hilo akiwa ndani ya gari Suzuki Escudo, namba T 559 AFA, marehemu naye aliongeza mwendo akidhani kuwa alikuwa akifukuzwa na majambazi ndipo, alipoanza kumfyatulia risasi.

Hali hiyo ilisababisha marehemu aongeze mwendo zaidi kwa kuhofia usalama wake na baadaye gari lake kukutwa na gari hilo ambalo lilikuwa ni la kiraia na askari huyo kumuua mfanyabishara huyo mita 50 kutoka nyumbani kwake.

Mara baada ya kufanya mauaji hayo inadaiwa kuwa askari huyo aliliondosha gari lake kwa mwendo kasi na kuelekea Tunduma na kudondosha bastola eneo
ambalo marehemu aliuawa.

Muda mfupi baada ya kufanya mauaji hayo baadaye lilikuja gari ya Polisi Landrover Defender likiwa na machela ndani na kuuchukua mwili wa marehemu kwa nia ya kuupeleka katika kituo cha Afya cha Tunduma.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Sogea, Bw. Ali Mwafongo alisema kuwa yeye alipata taarifa za kutokea kwa tukio hilo saa nne za usiku aliposikia milio ya bunduki.

Bw. Mwafongo alisema asubuhi kulipopambazuka waliletewa taarifa kuwa kuna mtu ameuawa na baadaye walipofika eneo la tukio walielezwa kuwa jirani yao ameuawa na askari Polisi na baadaye kufuatilia kituo cha afya ndipo walipobaini kuwa aliyefariki ni jirani yao Bw. Frank.

Tukio hilo lilisababisha wananchi hao kufanya maandamano ambapo kikosi cha Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) walianza kurusha mabomu ya machozi pamoja na risasi za moto
kwa nia ya kuwatawanya wananchi waliokuwa wakifanya maandamano hayo.

Hali ambayo ilisababisha hasira kwa wananchi ambao walianza kurusha mawe na kuvunja vioo vya magari.

Magari mawili moja la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa lilivunjwa
vioo vya mbele.

Mmoja wa ndugu wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Joseph Mwasote, ametaka iundwe tume kuchunguza kifo hicho.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Bw. Advocate Nyombi alisema alikuwa kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru na kuona mawe yamepangwa barabarani ndipo kusitisha mbio hizo na kwamba wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.


SOURCE: MAJIRA
 
Unajua Wasafwa wanaushirikiano sana tena wa hali ya juu.
Hakuna haja ya kuunda TUME tumechoka hii ni wazi polisi wamefanya makosa hawakuwasha king'ora mfanyabiashara alijua ni majambazi maana polisi walikuwa wanamfukuza kimya kimya.
 
Na hilo gari ambalo askari huyo alilitumia kumkimbiza marehemu aina ya Vitara Escudo mmiliki ni huyo huyo askari aliefanya mauaji.
 
Back
Top Bottom