Tundu Lissu:Ya Tarime yanukia singida mashariki.

The Emils

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
568
124
Migogoro ya madini kati ya wawekezaji na wachimbaji wadogo wadogo yaendelea kushika kasi..vijiji vya Mang'onyi, Taru na Londoni ni baadhi ya vijiji vyenye utajiri mkubwa wa madini aina ya dhahabu..kuna hii kampuni ya shanta mining iliyotumwa na serikali kufanya upembuzi yakinifu na badae kutoa ripoti kuwa kweli kuna hazina kubwa ya madini baada ya kuona wachimbaji wadogowadogo wakichimba.Yakatokea yafuatayo:1. wananchi hawaruhusi kuchimba mashimo makubwa kwenye mashamba yao2. shanta mining wakati wakifanya upembuzi mwaka jana walikanyaga mazao ya wakulima bila kuwalipa chochote.3. Mwezi uliopita wananchi walifukuzwa baada ya kuchimba shimo kwenye shamba linalosadikiwa kuwa na dhahabu nyingi.4. Kama vile haitoshi, polisi kutoka singida mjini wameletwa kuja kulinda hilo shamba usiku na mchana.5. Hakuna mwanakijiji yeyote alielipwa stahili zake hata kama anamiliki shamba kihalaliMbunge wangu Tundu Lissu mimi nikiwa mmoja wa mwanakijiji wa Mang'onyi tunaomba sana msaada wako kwani tuna imani sana kwako ndio maana hawa magamba wanataka kutumia nguvu zao kutunyang'anya haki yetu..mfano:Alichofanya Chiligati katika machimbo ya londoni na manyoni tunayafahamu..vinginevyo singida mashariki itageuka kuwa nyamongo part 2.
 
Back
Top Bottom