Nyamizi
Platinum Member
- Feb 19, 2009
- 9,192
- 13,737
Anaishi mbali na nchi anaonekana yuko ndotoni, anasahau jambo moja la msingi kuwa kati ya wale waliojitokeza kuchangia matibabu yake, ndio wale waliojitokeza kumpokea uwanja wa ndege alivyokuja kwa ajili ya uchaguzi mkuu uliopita.
Huruma ya hao watu ndio hiyo hiyo iliyowasukuma kujitokeza kwa wingi barabarani kumuaga Magufuli baada ya kufariki, chuki yake kwa Magufuli asilazimishe kuirithisha kwa watanzania wote, sawa alipigwa akaumizwa, lakini huruma ya watanzania huwa haichagui, na wala asijidanganye ana hatimiliki ya kupendwa na watanzania.
Kwa hii move yake sisemi uongo na wala sitaki kumliwaza yeyote, Lissu is disappointing big time, kuipiga mateke maiti sio ujanja ni ushamba, na hili litamfanya aonekane mropokaji, like it or not.
Atarudi Tz watampokea tena kwa wingi, after that, that will be it, nothing lasts forever.
Hunizidi Mimi Mkuu,kanidissapoint sana. Sijui akili yake inawaza nini? Ile huruma niliyokuwa nayo imeondoka kabisa. Huyu kama ndiyo ana ndoto ya kuja kugombea ndiyo atawajua Watanzania vizuri. Wenzie kina Mbowe wamekaa kimya anadhani wao ni wajinga?