Tatizo hapa ni ubunge au uanachama? Kama chama hakikutaki kwa nini ulazimishe uwe mwanachama wake? Anaweza kuhamia kule ACT na still akatetea ubunge wake na si lazima agombee kupitia Chadema. Nashangaa watu wengine ndiyo wanapiga kelele kwa niaba ya Zitto wakati yeye mwenye anatua Mwandiga kesho kuujulisha umma kuwa anahamia kwenye chama ambacho ameshiriki kukiasisi akiwa Chadema? Kelele hizi haziwezi kubadilisha maamuzi ya Chadema....period.
Hata kwenye ajira, mtu huwa anapewa masharti kabla ya kuanza kazi. Kama hukubaliani na masharti au policy hakuna anayekulazimisha kuchukuwa hiyo kazi. Lakini ukisaini kuchukuwa kazi inamaanisha kuwa unakubaliana na policy na taasisi ina-expect u-comply na kile ulichosaini. Na ili policy iwe relevant, inatakiwa kuwa updated mara kwa mara kutokana na mabadiliko au mahitaji kwa kipindi hicho. Na policy inapokuwa updated kila mhusika mpaka mfanyakazi wa chini anapewa na anaulizwa kama anakubaliana nayo, kama hukubaliani nayo..RUKSA KUMATA NJIA. Tatizo liko wapi?
Kama kweli mko concerned na katiba ya Chadema, kwa nini msiende mnakokuhafamu (haki inapopatikana) mka-file petition ili hilo tatizo lishughulikiwe? Maana nina uhakika hakuna maamuzi ambayo yanaweza kufanyika hapa JF dhidi ya katiba ya Chadema juu ya adhabu ya Zitto. Badala ya kupoteza muda, watu kadhaa wakae, wa-draft na ku-file petition au kwenda kufungua kesi mahakamani juu ya ukandamizaji wa Katiba ya Chadema dhidi ya wanachama wake. Na hakikisha wewe ni mwananchama wa Chadema kabla hujaenda kufungua kesi ili ueleze ni jinsi gani unaathirika na katiba hiyo. Ila upitie ngazi zote za chama before hujaenda mahakamani maana yanaweza kukuta kama haya haya.
Good luck.