Tundu Lissu rudi Shule

Tundu lisu arudi shule tu aache kukurupuka mpaka wenzake wanamshangaa
 

Attachments

  • 1426298563481.jpg
    59.4 KB · Views: 127
Wewe ndiyo unajiita msomi? Wewe nadhani ni kanjanja +++.

Hakuna msomi anayeweza kusema go go tupo nyuma yako. Msomi hawezi kumfuata mtu ambaye hajui anaenda wapi. Wewe inaonekana upo tayari kumfuata Zito kokote anakokwenda hata kama ni chooni. Hakuna msomi yeyote Duniani ambaye huwa na falsafa ya kijinga namna hiyo, ya kumfuata mtu fulani kokote aendako.

 
Last edited by a moderator:
Katiba yao inasema ukipeleka swala linalohisu chama mahakamani na kesi hiyo ukashindwa basi utakuwa umejifukuzisha

Iko hivyo ukienda na ukashindwa hapo elewa umeshindwa maana nyingine uliyemshtaki amekushinda sasa apo si umeshindwa
Kwanza umepoteza muda wa uliyemshtaki
Umemdhalilisha
Basi mlipe fidia
 

Ewe wakili msomi kama unavyojiita, naona kimsingi ungetakiwa ujishangae wewe na sio wananchi. Ujishangae wewe kwa kutaka kupotosha wananchi kwa kuwaaminisha kuwa alichokiongea Tundu Lissu ni kuwa mahakama imeongelea kuhusu uanachama wa Zitto kabwe pale Chadema, Tundu Lissu alisema kuwa kesi ya Zitto imetupiliwa mbali na kwa vile moja ya ibara za katiba yao ni kuwa mtu akikishtaki chama mahakamani na akashindwa basi anakua amepoteza uanachama wake automatikali (acha procedure nyingine za kupewa taarifa rasmi nk), hivyo basi jishangae wewe kwa kutaka kupotosha umma ilhali wengi wanajua kuwa kilichomfukuzisha Zitto Chadema kwa sasa ni kushindwa kwa kesi yake aliyoipeleka mahakamani kuwa chama kisijadili lolote kuhusu uanachama wake (hapa hata chama hakijajadili kuhusu uanachama wake wala madudu yake japo kingetaka kingeweza pia kujadili uanachama wake na kumpiga chini).

Unamshauri Zitto aende mahakama ya rufaa kuomba tafsiri ya uamuzi wa mahakama kuu, unamshauri vibaya jamaa yako (Comrade), bora ungemshauri akate rufaa kuwa amekasirishwa na maamuzi ya mahakama kuu kwa sababu anaamini alifungua kesi yake kwa usahihi ili wapitie jalada na wao (mahakama ya rufaa) watoe uamuzi kuhusu hiyo rufaa yake (nadhani lengo lako kuu ni kutaka jamaa aendelee kuwa mbunge, basi kwa delay Technic hii anaweza kuendelea kuwa mbunge mpaka bunge litakapovunjwa hapo Julai 2015). Kuomba tafsiri tu bila kukata Rufaa hakutamsaidia.

Kwa maelezo ya Tundu Lissu tarehe ya juzi ile ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa uamuzi japo Zitto ansema kesi ilikuwa inaitwa kutajwa, nashangaa lakini leo ni almost wiki bado hawajua tu kama ilikuwa inaitwa kutajwa, kusikilizwa au kutolewa uamuzi (Zitto alisema wakili wake anafuatilia kujua hilo) badala yake nasikia Zitto anaomba wanajimbo wake wamuunge mkono katika maamuzi atayofanya (obvious ni kuwa anajua tarehe 10 Machi ilikuwa ni day for rulling ambapo angekuwepo au asingekuwepo mahakamani, isingeathiri chochote kwa maana ya kubadili uamuzi wa mahakama).Mwisho, mzee Mahakama kwani huwa inatafuta kesi? Zitto kapeleka kesi ya kuzuia asijadiliwe uanachama, leo unasema kuwa mahakama ya Rufaa itatoa maelekezo kuhusu katiba mbovu kama za Chadema, sasa mahakama sijui itaanza vipi kujadili kuhusu katiba wakati hakuna mtu aliyelalamika kuhusu katiba hiyo!! 'Wakili Msomi' hapo nadhani haupo sahihi kabisa na utafanya watu wazidi kukutilia shaka kwa hayo majina unayojiita..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…