Tundu Lissu: Rais Magufuli anapotosha kuhusu "Magwangala", ajifunze kwa Rais wa Bolivia

Mkuu uwe unaelewa, tatizo sio mgodi au wamiliki wa migodi, tatizo ni nemc waliowakataza wamiliki wa migodi kugawa hayo maweukoko, kwanza hayana hata dhahabu sanasana wananchi watatumia kujengea nyumba tu.
Kwa hiyo unataka kusema kuwa migodi inasafirisha mawe ukoko kwenda Japan!? Ili iweje hasa!?
 
mgodi unaosafirisha mawe uko singida unamilikiwa na mtanzania, huko geita hawasafirishi mawe.
 
Inashangza kusoma andiko la Tundu Lissu likitoa hitimisho kwa suala ambalo kila siku anatuambia hafahamu mkataba wake.

Kwa hiyo anachotaka kutuambia Tundu Lissu, serikali isiende hata mahakamani kupata tafsiri za kisheria.

Mbaya zaidi, eti anaishauri serikali ifanye kama ilivyofanya Bolivia ambapo kimsingi, kitendo hicho ni kuondoa mazingira rafiki ya wawekezaji wote nchini. Serikali ikifanya hivyo, huyu huyu Tundu Lissu atajitokeza tena na kuanza kusema, serikali imekosa wawekezaji kwa sababu imeondoa mazingira bora ya uwekezaji.

Unafahamu kuna baadhi ya wanasiasa kama Tundu Lissu wamefahamu udhaifu wa baadhi ya watanzania na kwa msingi huo, wanatumia udhaifu huo kujinufaisha kisiasa.
Kuna shida kubwa upande wako!. Hebu tulia halafu utenganishe "concept" ya Tundu Lissu (kusomea na kujua sheria za mikataba ya madini) Na ya kwako (kuisoma mikataba ya madini). Ukielewa mnapotofautiana Na Lissu utaelewa uncle Magu alipoteleza, vinginevyo unaelewa ila unafanya makusudi
 
mgodi unaosafirisha mawe uko singida unamilikiwa na mtanzania, huko geita hawasafirishi mawe.
Magwangala ni waste rock na ni tofauti na mchanga unaopelekwa Japan. Huu mchanga unatoka Bulyanhulu na kwa siku ni semi trela zaidi ya 20 zinaelekea bandari kavu ya Isaka. Nime research hiyo area
 
Ila msikilizeni Tundu kwa hili. Ukiwa tayari ndani ya tundu, usiendelee kuchimba!
Magufuli anachimba.
 
Richard,

..nadhani hujamuelewa Tundu Lissu "TL" hoja yake.

..hoja ya TL ina sehemu mbili. Mchango unaosafirishwa nje (suala la mkataba)na magwangala (thamani yake).

..TL ameeleza njia za kufuata ili tuweze kuyabana kisheria makampuni yanayosafirisha nje mchanga wenye madini. Amependekeza hatua na utaratibu uliofuatwa na Evo Morales.

..kuhusu magwangala TL ameeleza kwamba yale ni mabaki yasiyo na thamani kwa mwekezaji. Ameyabeza kwamba ni sawa na kula makombo.

..tungelisaidia jukwaa kama tungejadili FAIDA vs HASARA za MAGWANGALA. Au njia bora na salama ya kuvuna magwangala.

..mimi nadhani hoja ya TL imesheheni " madini ". Labda kilichowakwaza ni vijembe vya kisiasa vya hapa na pale.

NB.

..TL ni mwanaharakati wa masuala ya madini na rasilimali tangu alipomaliza chuo kikuu.

..amesha-deal(kashfa ya bulyankulu) na makampuni makubwa ya madini mpaka huko yanakopata fedha za kuja kuwekeza hapa Tz.

..pia amefanya kazi ya utafiti kuhusu masuala ya madini na rasilimali ndani na nje ya nchi.

Cc MsemajiUkweli ,

Mkuu Joka Kuu,

Mchanga unaosafirishwa nje umekuwa unasafirishwa bila uangalizi hivyo kuanza sasa kuuangalia mchanga na kuupima hilo ni jambo safi kabisa.

Kama ni mkataba basi hata Evo Morales ambae Tundu Lissu anamtumia kama mfano aliwaambia wachimba madini kuwa take upya tuandike mikataba mipya inayoweka bayana nani anafuata sheria na kanuni.

Hakuna nchi yoyote ile duniani hata hizo wanakotoka hao wawezekezaji wataruhusiwa kusafirisha mchanga kienyeji bila kufuata taratibu na wao wanafahamu hivyo.

Kuhusu Magwangala kwanza, watu wa STAMICO na baadhi ya viongozi huko nyuma walikuwa wakiwafukuza wananchi kwenye maeneo yote ambayo hao viongozi walihisi kuna magwangala yenye thamani hivyo kuwepo uwezekano wa kupata madini kadhaa katika magwangala hayo.

wachimbaji.jpg

Kuna uwezekano mkubwa wa kupata chochote kutoka kwenye Magwangala.

Na walipopata madini hayo walifanya biashara ya madini na kusahau kwamba maeneo yote yenye Magwangala mengi ni ya wananchi wanaozunguka eneo la mgodi wa Geita pamoja na wale wachimbaji wadogowadogo ambao wanamiliki machimbo madogomadogo.

Mwisho ni kwamba Tundu Lissu na kundi lake wanapotosha watanzania kwa hoja ya magwangala. Hoja hapa ni kwamba mgodi wa Geita unatakiwa usichukue mabaki ya mawe ya dhahabu ambayo hubakia baada ya shughuli ya upasuaji wa miamba.

Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatafutia wakazi hao na wafanyabiashara wadogo wa madini sehemu maalum ya kuchekecha mawe hayo ili kupata dhahabu wanayotafuta na wakipata wanakwenda ofisi ya madini na kupima halafu kisha kuiuza kwa madalali.

Hawa wachimbaji wadogo na wenye kupata hayo magwangala kabla ya kuanza shughuli za uchenguaji inabidi wawe na leseni za kuchimba na pia namba ya VAT.

Lakini katika karne hii ya 21, hatuwezi kuendelea kumruhusu mgeni kuja kuchimba madini nchini mwetu halafu pia abebe mamilioni ya tani ya mabaki ya mchanga kuyasafirisha nje ya nchi nasi tubaki kama tulivyo.

Hivyo vituko alifanyiwa hayati Chifu Mangungo wa Mzovero kwenye karne ya 19.
 
Kama ni suala la kisheria, Tundu Lissu anafahamu mkataba wa serikali na wawekezaji?

Kwa nini asiweke wazi ili na sisi tuusome na kuuelewa badala ya kujaribu kutuaminisha kwa maneno.

Hata tukikubaliana na maneno ya Tundu Lissu, kumbuka kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na kwa maana hiyo anaposema serikali itashindwa haina maana kweli serikali itashindwa. Kuna kesi nyingi tu ambazo hata yeye kama wakili ameshindwa mahakamani.

Kumbuka pia, siyo huyu huyu Tundu Lissu alikuwa anapiga kelele akisema hafahamu mikataba yaTanzania na wawekezaji na kwa maana hiyo anaitaka serikali iweke wazi mikataba.

Mikataba kutokuwekwa wazi haimaanishi Lisu hajaiona, ameiona kwa njia ya panya. Yote tisa, kuvunja mkataba mahala popote ulimwenguni, uliyevunja utashindwa tu, huhitaji kuwa mwanasheria kujua hili. Lisu ameshauri njia ya kufanya ambayo itaondoa nchi kulipa fidia na kuwa black listed kama taifa lisiloheshimu mikataba. Kumbuka tunawahitaji sana wawekezaji makini, na watu wa namna hiyo wanatilia maanani sana utawala wa sheria, na siyo amri za majukwaani zinazotegemea rais kaamkaje siku hiyo. Ndiyo maana wawekezaji makini wanaangalia sana shereia za uwekezaji, kodi, n.k kabla ya kufanya maamuzi
 
Kwani mikataba ya madini ya Botswana na Tz inafanana!? Botswana madini yao ndio roho ya uchumi. Wao mikataba yao inawapa nguvu hiyo. Je, mikataba yako wewe Tz inakupa jeuri hiyo!?

Mikataba iliyosainiwa na mawaziri waliopita ambayo haikuwa sahihi yote inaweza kufanana na ya Botswana kwa kuzingatia kwamba hata sisi Tanzania tunayo madini mengi tu yenye kuweza kutufanya tuyategemee.
 
U
Mkuu Joka Kuu,

Mchanga unaosafirishwa nje umekuwa unasafirishwa bila uangalizi hivyo kuanza sasa kuuangalia mchanga na kuupima hilo ni jambo safi kabisa.

Kama ni mkataba basi hata Evo Morales ambae Tundu Lissu anamtumia kama mfano aliwaambia wachimba madini kuwa take upya tuandike mikataba mipya inayoweka bayana nani anafuata sheria na kanuni.

Hakuna nchi yoyote ile duniani hata hizo wanakotoka hao wawezekezaji wataruhusiwa kusafirisha mchanga kienyeji bila kufuata taratibu na wao wanafahamu hivyo.

Kuhusu Magwangala kwanza, watu wa STAMICO na baadhi ya viongozi huko nyuma walikuwa wakiwafukuza wananchi kwenye maeneo yote ambayo hao viongozi walihisi kuna magwangala yenye thamani hivyo kuwepo uwezekano wa kupata madini kadhaa katika magwangala hayo.

wachimbaji.jpg

Kuna uwezekano mkubwa wa kupata chochote kutoka kwenye Magwangala.

Na walipopata madini hayo walifanya biashara ya madini na kusahau kwamba maeneo yote yenye Magwangala mengi ni ya wananchi wanaozunguka eneo la mgodi wa Geita pamoja na wale wachimbaji wadogowadogo ambao wanamiliki machimbo madogomadogo.

Mwisho ni kwamba Tundu Lissu na kundi lake wanapotosha watanzania kwa hoja ya magwangala. Hoja hapa ni kwamba mgodi wa Geita unatakiwa usichukue mabaki ya mawe ya dhahabu ambayo hubakia baada ya shughuli ya upasuaji wa miamba.

Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatafutia wakazi hao na wafanyabiashara wadogo wa madini sehemu maalum ya kuchekecha mawe hayo ili kupata dhahabu wanayotafuta na wakipata wanakwenda ofisi ya madini na kupima halafu kisha kuiuza kwa madalali.

Hawa wachimbaji wadogo na wenye kupata hayo magwangala kabla ya kuanza shughuli za uchenguaji inabidi wawe na leseni za kuchimba na pia namba ya VAT.

Lakini katika karne hii ya 21, hatuwezi kuendelea kumruhusu mgeni kuja kuchimba madini nchini mwetu halafu pia abebe mamilioni ya tani ya mabaki ya mchanga kuyasafirisha nje ya nchi nasi tubaki kama tulivyo.

Hivyo vituko alifanyiwa hayati Chifu Mangungo wa Mzovero kwenye karne ya 19.
unachanganya stori GGM hawasafirishi magwangala na wala hawana shida nayo zaidi ya concern ya usalama wa mali zao watu na mazingira. Wanaosafirisha mchanga ( na si magwangala) ni BGM
 
BGM ni underground mine wala wananchi hawaoni na kutamani huo mchanga wao zaidi ya kuibiwa ukiwa njiani kwenda Isaka
 
JPM akifanya hayo anayotaka Tundu Lisu, amuige Rais wa Bolivia, wawekezaji wakianza kuondoka mtakuja tena kulaumu, Kuna kipindi walilaum kua utalii unaingiza Fedha kidogo kuliko sigara, imewekwa kodi katika utalii, mmepiga kelele hapa

Kuna kipindi Mwaka 2014 wapinzani walipiga kelele juu ya vibali vya sukari kua inaua viwanda vya ndani, visitishwe, vimesitishwa, mlikuja kupiga kelele tena .

USHAHURI WA KINAFIKI HAUNA NAFASI TENA KATIKA SERIKALI HII
Wamepiga kelele mafisadi wanaimaliza nchi, haya wameshughulikiwa! Hao hao waliokuwa wanapiga kelele wameanza kulia lia maisha magumu. Yote hayo ni unafiki tu.
 
Mkuu Joka Kuu,

Mchanga unaosafirishwa nje umekuwa unasafirishwa bila uangalizi hivyo kuanza sasa kuuangalia mchanga na kuupima hilo ni jambo safi kabisa.

Kama ni mkataba basi hata Evo Morales ambae Tundu Lissu anamtumia kama mfano aliwaambia wachimba madini kuwa take upya tuandike mikataba mipya inayoweka bayana nani anafuata sheria na kanuni.

Hakuna nchi yoyote ile duniani hata hizo wanakotoka hao wawezekezaji wataruhusiwa kusafirisha mchanga kienyeji bila kufuata taratibu na wao wanafahamu hivyo.

Kuhusu Magwangala kwanza, watu wa STAMICO na baadhi ya viongozi huko nyuma walikuwa wakiwafukuza wananchi kwenye maeneo yote ambayo hao viongozi walihisi kuna magwangala yenye thamani hivyo kuwepo uwezekano wa kupata madini kadhaa katika magwangala hayo.

wachimbaji.jpg

Kuna uwezekano mkubwa wa kupata chochote kutoka kwenye Magwangala.

Na walipopata madini hayo walifanya biashara ya madini na kusahau kwamba maeneo yote yenye Magwangala mengi ni ya wananchi wanaozunguka eneo la mgodi wa Geita pamoja na wale wachimbaji wadogowadogo ambao wanamiliki machimbo madogomadogo.

Mwisho ni kwamba Tundu Lissu na kundi lake wanapotosha watanzania kwa hoja ya magwangala. Hoja hapa ni kwamba mgodi wa Geita unatakiwa usichukue mabaki ya mawe ya dhahabu ambayo hubakia baada ya shughuli ya upasuaji wa miamba.

Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatafutia wakazi hao na wafanyabiashara wadogo wa madini sehemu maalum ya kuchekecha mawe hayo ili kupata dhahabu wanayotafuta na wakipata wanakwenda ofisi ya madini na kupima halafu kisha kuiuza kwa madalali.

Hawa wachimbaji wadogo na wenye kupata hayo magwangala kabla ya kuanza shughuli za uchenguaji inabidi wawe na leseni za kuchimba na pia namba ya VAT.

Lakini katika karne hii ya 21, hatuwezi kuendelea kumruhusu mgeni kuja kuchimba madini nchini mwetu halafu pia abebe mamilioni ya tani ya mabaki ya mchanga kuyasafirisha nje ya nchi nasi tubaki kama tulivyo.

Hivyo vituko alifanyiwa hayati Chifu Mangungo wa Mzovero kwenye karne ya 19.

..thank.

..nakubaliana na maoni yako pamoja na ya TUNDU LISSU.
 
Lakini zamani watu wote,, paka hao kina lisu walikua wanasema wananchi wanaonewa inakuaje watu wachukue gold na mchanga? Paka mikutano walienda kufanya. Vp leo kuwe na sheria halali apo...mbona mwanzo hawakuwaambia watu kwamba ni halali kisheria?
Mbona mnashindwa kuelewa? Watu walikuwa wanapiga kelele sheria ibadilishwe sio kulipuka na kusema hakuna kuchukua Mchanga.
Ni kama walipokuwa wanasema watumishi wabovu waondolewe, hawakumaanisha wafukuzwe bila kufuata sheria zilizopo. Ndio maana mnashangaa wakipinga style ya kufukuzwa.
Hata jambo baya lazima liondolewe kisheria na sio kwa kauli ya mtu mmoja kisha ikigeuka kesi inakuwa hasara tena ya serikali
 
Sina Cha kuongeza HATE THAT BUT HUO NI USHAURI WABURE WA KISHERIA ...
BY THE WAY ...hivi MAGUFULI ni kiongozi anayeamini mrengo gani ????

Kama anaamini KWA Hisia kuwa ni mteule wa Mungu KWA hiyo hakosolewi BASI Tutakuwa NA Bahati Mbaya Sana watanzania
Kipo kikundi cha ushangiliaji ambacho, siku malaika atakapokwa kisiki watasema hizo ndio style zake, ni POSE.
 
U

unachanganya stori GGM hawasafirishi magwangala na wala hawana shida nayo zaidi ya concern ya usalama wa mali zao watu na mazingira. Wanaosafirisha mchanga ( na si magwangala) ni BGM

Wenye migodi iwe GGM au BGM na wale wengine waanze sasa kufuata taratibu, sheria na kanuni zinazowekwa na serikali.

Si umesikia kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania mwezi uliopita Kampuni ya Barrick Gold imetoa taarifa yake ya mapato na faida?

Halafu kama unakumbuka Mahakama ya masuala ya kodi mapema mwaka huu waliwaambia Barrick Gold kwamba walikwepa kulipa "corporate tax" kwa muda wa miaka minne kati ya 2011-2014.

Pia haohao Barrick Gold mwaka huu wameanza kulipa hiyo kodi ya USD milioni 20 sawa na tshs bilioni 40 au fwedha za madafu na hiyo itakuwa kila mwaka.

Nao Acacia kila baada ya miezi 3 watatakiwa kuwalipa TRA kasi cha dola za marekani milioni 3 sawa na shilingi bilioni 10 zikiwa fwedha za madafu.

Sasa fedha hizo zote kwanini tulikuwa tukizipoteza baada ya watu kuchekacheka na kulipiwa kulala kwenye 4 star hotels London na Paris halafu mtu anasaini mkataba feki?

Tuifuate serikali mpya kwenye "New Direction" ambayo itamfaidia kila mtanzania, hiyo ndiyo "the way forward".

Ukiangalia nyuma utageuka jiwe.

Hapa kazi tu.
 
Back
Top Bottom