Tundu Lissu ni jasiri wa kipekee

Tundu Lissu ni jasiri wa kipekee

mcoloo

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
918
Reaction score
1,402
Katika nchi hii kwa sasa hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kusimama hadharani na kukemea madhambi yanayo fanywa na watawala isipo kuwa ni Tundu Lisu pekee.

Japo kuwa anapachikwa majina mengi lkn ukweli Ni kwamba huyu jamaa ameacha Alama ambayo ni mfano Tosha kwa jamii, hasa pale wanapo ona mambo kuto kwenda sawa.

Nimejaribu kuhesabu maneno yake na nilicho kigundua Ni kwamba hakuna hata moja analo sema la uongo yote anayo yasema yametendeka.

1 : Ujenzi wa uwanja wa ndege wa chato. - BAJETI HAIKUPITISHWA NA BUNGE huu Ni uvunjifu wa Sheria za nchi.

2 : Manunuzi ya ndege.- BAJETI HAIKUPITISHWA Ni uvunjifu wa Sheria za nchi.

3: Kuminywa kwa vyama vya siasa ili viweze kufanya kazi zao kwa uhuru. - NI UVUJIFU WA KATIBA YA NCHI.

4: Kutokukemea mauwaji na kutekwa kwa watu- HUKU NI KUUNGA MKONO VITENDO VIOVU.

5: Matumizi mabaya ya fedha za Kodi za wananchi kwa kurudia chaguzi mlizozitengeneza wenyewe-HUU NI UHUJUMU UCHUMI.

6: Kuhamisha wanyama toka katika mbuga zao na kuwapeleka kwenu : HUU NI UMOBUTU SESEKO. Mbaya Sana.

7: Kujiita kuwa unaafaa kuwa kiongozi wa Malaika Mbinguni.- HAYA NI MAKUFURU.

8: Kujisifu kuwa umejenga flyover nakuona kuwa Hilo Ni Jambo la ajabu.-HUO NI USHAMBA WA KARNE.

9: Kutumia TRA Kama pembe ya kuwachomea wale wanatofautiana nawe.- HAYA NI MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA.

10: Kuziita barakoa kuwa Ni sawa na sidilia za akina mama. - HII NI KUDHARAU VAZI LA AKINA MAMA.nk.

Yapo mengi na katika hayo sijaona Tundu aliposema uongo. Tukumbuke kuwa Lisu anamshambulia jiwe kwa sababu yeye ndiye angefaa kukemea maovu lkn bila aibu amekuwa mtu wa Kwanza kubariki maovu.

Jamani kweli Tena mtu Kama huyu apewe mitano mingine ? Dunia itatucheka .
SASA BASI.
 
Naamini hii ndio inawatesa sana ccm, marisasi yote yale yamempa ujasiri zaidi. Naamini Mungu alimponyesha kwa sababu anataka kumpa kazi maalumu ktk nchi yetu. Tanzania ya haki, matumaini, usawa na utu inakuja
 
Bandiko lako kifupi yatosha kusema linachekesha
 
Hakuna kama Lissu ndugu. Huyu mtu si wa Safari hii. Ni Mungu tu anajua amemuumbaje huyu mtu
 
Back
Top Bottom