Watanzania tuna upeo mdogo sana wa kutafsiri mambo. Tunatafsiri mambo mengi kwa vey narrow premises.Mtu akihoji mamlaka makubwa ya kikatiba ya Rais ya kuteua watu wengi kwenye nafasi tofauti za uongozi anaambiwa anahoji mamlaka ya JK wakati urais ni taasisi ya kushikwa na mtanzania yeyote mwenye sifa kwa nyakati tofauti chini ya katiba ile ile.
Hoja ya Mheshimiwa Tindu Lissu ilikuwa kuhoji kitendo cha hadhi na mamlaka ya Bunge kuingiliwa na mtu kutoka nje ambaye ni wa mhimili mwingine wa dola. Hoja hii ina uzito wa kulifanya Bunge lihalalishwe kuahirisha kujadili hoja iliyopo na kujiadili hoja hiyo ya kulirudishia Bunge heshima yake.
Kuna wajinga wame-construe hoja hiyo very narrowly kwamba inamhusu Mheshimiwa Tindu Lissu personally wakati inaihusu taasisi nzima ya Bunge. Kwa bahati mbaya sana miongoni mwa wajinga hao ni kiongozi mwenywe mkuu wa taasisi iliyodharauliwa, yaani Spika wa Bunge! Kwa mwendo huu Watanzania tunahitaji elimu bora kwani tuko dull kichizi.