Tundu Lissu: Mwigulu anahusika na mauaji ya polisi CRDB Mbande?

medsebapol

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
327
225
TUNDU LISSU, MWIGULU ANAHUSIKA NA MAUAJI YA POLISI CRDB MBANDE?

Uyu jamaa anajiskia kuongea sana angekuwa anajua angesubilia afatwe ndo aseme tunaenda kubaya,pia anajenga hali ya kuchochea kabisaa.

Tundu Lissu amesema CHADEMA wala UKUTA hawahusiki na mauaji ya askari polisi, lakini ukweli ni kwamba jeshi la polisi hawajamtaja mshukiwa wa mauji hayo na ameshangaa mauaji hayo kuhusishwa na UKUTA mapema mapema na kuanza kusema kuhusisha tukio hilo na UKUTA ni kutafuta sababu za kuhalalisha udikteta nchi hii.

Anaendelea kuhoji mara baada ya askari kuuwawa ndani ya muda wa nusu saa kwa mujibu wa vyombo vya habari Mwigulu Nchemba alifika jeshi la polisi akiwa amevalia sare rasmi za jeshi la polisi,
Mkuu wa jeshi la polisi IGP Mangu hakuwepo, mkuu wa mafunzo na operesheni hawakuepo ma OCD hawakuepo wala RPC wa Dar hawakuepo lakini waziri wa mambo ya ndani, ndani ya nusu saa alikuwepo

Anahoji huyo aliyempa taarifa Mwigulu asiwape taarifa wakuu wa jeshi la polisi badala kuwapa maafisa wa jeshi la polisi wanaotakiwa kumsahuri na wataalamu wa mambo ya uhalifu kwenye tukio naya kama lile?

Na ndani ya nusu saa alikuwa na sare za jeshi la polisi anahoji sare hizo alizitoa wapi ndani ya muda huo mfupi?

Amesema mambo hayo sio mageni sana kwa kuwa matukio kama hayo ndio yaliyopelekea Hitler kuwa mtawala wa Ujerumani

Amesefananisha na tukio la moto wa kuchoma moto bunge la ujerumani kisha tukio hilo kuhusishwa na chama cha upinzani ujerumani na shughuli za siasa zikapigwa marufuku, na ndani ya siku moja Hitler akapiga marufuku katiba ya Ujerumani na kuanza kutawala kidikteta
Tukio hilo Hitler aliliita ni ishara kutoka kwa Mungu kuwa yeye ndio anatakiwa kuwa mtawala na mkombozi wa Ujerumani

Amesema tukio la jana la polisi kuuwawa jana ndio imekuwa ishara kwa Magufuli kama ilivyokuwa ishara kwa Hitler na kuanza kutawala kidikteta




Source
 
Mie huyu huwa hata simsikilizi! Njaa kali njia zote zimezibwa muache apige kelele tu.. Huyu milembe kunamuhusu!! Eti nae ni kiongozi?? Akaongoze punda huko kwao Puma!
Njaa inamsumbua huyu atavaa sana suti.. Hapa kazi tu.

Ila hili aliloongea linaingia akilini, hasa ukizingatia alichoongea kiko wazi na huyo anayemtaja watu wana mashaka na mwenendo wake. Ametufungua wengi pamoja na ukichaa wake. Kwa maneno marahisi tz inatakiwa kuwa na vichaa wengi wa aina hii.
 
Ila hili aliloongea linaingia akilini, hasa ukizingatia alichoongea kiko wazi na huyo anayemtaja watu wana mashaka na mwenendo wake. Ametufungua wengi pamoja na ukichaa wake. Kwa maneno marahisi tz inatakiwa kuwa na vichaa wengi wa sina hii.
Ila tukumbuke pale unapokuwa unadai haki au Uhuru lazima uwe msili ili at end of the time unafanya kitu chenye uhaki hasa nambie mfano kwa hivi alivyosema ni kama anawapnguzia wenzake speed
 
Back
Top Bottom