Tundu Lissu kutogombea tena ubunge?

Tundu Lissu kutogombea tena ubunge?

Katika maisha kinachoangaliwa siyo pesa tu, kuna mambo mengine kama vile sifa, mchango wako kwa nchi yako, kutakuwa katika nafsi fulani nk. Kama anasema ubunge umemtia umasikini inategemea tafsiri yake binafsi (operatinal definition) ya umasikini kwa sababu sote tunajua kipato cha wabunge kuwa ni kikubwa kuliko mtumishi wa umma mwingine yeyote. Kuwa masikini hakutokani tu na kipato kuwa kidogo, bali pia matumizi. Lakini pengine analinganisha na kipato ambacho angekipata kama angeendelea na kazi yake ya uwakili, hii ni opportunity cost. Inakubidi ifikirie mara mbili kuacha hiki ili kupata kingine unachoona kinafaida zaidi. Unapochagua kati ya vitu viwili vyote vyenye faida, unapaswa kuchagua kile chenye faida kubwa ila unapochagua kati ya vitu viwili vyote vyenye hasara basi unachagua chenye hasara ndogo. Lakini unapaswa kuangalia muda wa malengo. Kuna malengo ya muda mfupi na muda mrefu. Kazi ya siasa inalipa sana ila haitabiriki. inaweza kukulipa baada ya miaka mingi kupita. Tazama JK aliacha kuajiriwa kama mchumi miaka ya 1980 akawekeza kwenye siasa akaja apata mapato yasiyomithirika mwaka 2005 baada ya miaka 20 kupita. Ni mapema mno kwa Lisu kukata tamaa. Huu ni uwekezaji wake binafsi sisi kama wananchi haituhusu. Asipokuwa yeye tutapata mwingine atakayefaa pengine kumzidi yeye. Kubadilishana uongozi ndiyo kunakotupa nafasi ya kumjua mwingine bora zaidi. Tanzania ina watu 45 mln.
Wasalaam wana jamvi!
Wakati wengine wakifurahia kupata ubunge kwa upande wa Mh Tundu Lissu imekuwa ni matatizo makubwa kwani ubunge umemsababishia umasikini kabisa!

Wana jamvi waswahili wanasema ukiona mtu mzima ana lia hadharani ujue kuna jambo.....Mh Tundu Lissu alikaririwa akisema ubunge umemsababishia umasikini na hivyo ana hitaji zile pesa 230+ walizo kuwa wametengewa!

Kwakweli mimi nilisikitishwa sana na kukuguswa sana na kilio chake na niliamini kabisa Lissu ni mtu makini sana anaposema ubunge umemsababishia umaskini ana maanisha kabisa na pengine tusije tukashangazwa kama hatogombea tena maana mtu makini kama Mh Tundu Lissu awezi kuendelea na kitu kinacho mtia umasikini!

Hivyo ndio maana nimepata wasi wasi kama kweli Lissu atagombea ubunge tena lasivyo ni vyema Chadema wakamfikiria zaidi Mh Lissu kwa kumpa hata mshahara wa ziada ili kumuondoa kwenye umasikini alio upata baada ya kuwa mbunge!

Kama kweli Dr.W.Slaa aliweza kusikilizwa na kuwa ana lipwa kama mbunge kutokana na umuhimu wake ni vyema na Mh Lissu akapewa mshahara wa ziada kutoka kwenye chama kutokana na kazi anayo ifanya!

Bado najiuliza kweli Mh Lissu atagombea ubunge tena ikiwa huu ubunge umemletea umasikini hadi ana tangaza hadharani?

Ni vyema ili jambo likatazamwa vyema ili Mh Lissu asije akagomea kugombea ubunge kutokana na umasikini!

Karibuni wana jamvi!
 
Wewe ni mmoja wa wapuuzi na wajinga sijawahi kuwaona duniani.nasema wajinga maana ningesema wapumbavu ningekushusha kwa kuwa angalau unajua kusoma na kuandika.hivi na wewe umeona umeletA mada ili watu wasiovaa nepi wajadili?
 
Wewe kichwa wengine hawana muda wa kufikiri zaid ya matusi...
 
Back
Top Bottom