Tundu Lissu: Hizi Pikipiki zinatengenezwa China kwa Mamilioni lakini China hakuna Bodaboda hivyo Siyo Ajira

Kwa hiyo wewe unaona ni sawa kwa vijana woote wa kitanzania kutumia boda kama ajira huku wakimalizwa au kufanywa vilema watokanao na ajari za pikipiki hasa ukifikiria kwamba ajira yenyewe haina bima kama ajira zingine?
Naona ni Sawa, ajali hata kwenye magari, treni, meli na ndege zipo na watu wanaokufa, we unadhani kila kazi ina BIMA? Hao vibarua viwandani wanaolipwa laki na ishirini Wana bima? Machinga, mamantilie Wana bima? Je watu wasifanye kazi kisa wanaogopa kufa? Je wanaofanya kazi unazoona sio za laana hawafi wanaishi milele?
 
Vietname haina piki piki? Hahahaha huyu jamaa kazingua hapa. Kama kuna sehem duniani kuna boda boda zinazozid nilizoziona pale Vietnam najiuzulu aisee duu. Ukiwa kwenye mataa ni kama mita mia tano. Ni wengi kama utitiri.
Vietnam na huko kwingine watu wanatumia bodaboda zao binafsi kama mtu anavyotumia gari yake binafsi kumpeleka na kumrudisha nyumbani na sio kubebea abiria kuingiza kipato.
 
Tope topeni, akawadanganye wasioijua China, CHINA MPAKA BODABODA ZA BAISKELI ZIPO!
Hizo zinatumika kama usafiri binafsi. Yaani anayeiendesha ndio mmiliki kama wewe unavyoendesha gari yako kwenda kazini.

Binafsi rafiki yangu hawa wanaokwenda nje kufanys maonesho ya sarakasi, alivyokuwa huko China alinunua moja ya kuchaji ukawa ndio usafiri wake. Ila ilimishinda tu kurudi nayo muda wake wa kuishi kule ulivyoisha.
 
Vietnam na huko kwingine watu wanatumia bodaboda zao binafsi kama mtu anavyotumia gari yake binafsi kumpeleka na kumrudisha nyumbani na sio kubebea abiria kuingiza kipato.
Sasa hoja yako ni nini hasa? Kwani akiitumia kama ajira kumuingizia kipato ni dhambi au kuna ubaya gani akifanya hivyo?
 
Sasa hoja yako ni nini hasa? Kwani akiitumia kama ajira kumuingizia kipato ni dhambi au kuna ubaya gani akifanya hivyo?
Shida ni pale mnapojaribu kuchukua mifano ya huko kuifanya uhalalisho. Bodaboda ni kichaka cha kujibanza pale unapokuwa huna mchongo wowote na kutafutia mtaji. Ni dharura tu. Unaweza niambia mtoto wako unamsomesha aje kufanya bodaboda!?
 
Vietnam na huko kwingine watu wanatumia bodaboda zao binafsi kama mtu anavyotumia gari yake binafsi kumpeleka na kumrudisha nyumbani na sio kubebea abiria kuingiza kipato.
Bro mi nimekaa pale miez minne kila cku nilikuwa natumia boda. Thailand ndio usiseme ingawaje ndio zipo za familia. Kwa wale walioenda Bangkok wataelewa kutoka soukhmvit mpaka pratunam tulikuwa tunatumia nini sana ukikosa tax au bajaji
 
Shida ni pale mnapojaribu kuchukua mifano ya huko kuifanya uhalalisho. Bodaboda ni kichaka cha kujibanza pale unapokuwa huna mchongo wowote na kutafutia mtaji. Ni dharura tu. Unaweza niambia mtoto wako unamsomesha aje kufanya bodaboda!?
Wewe nikuulize matamanio aliyokuwa nayo Baba yako yote yalienda Vile alivotaka? Wewe binafsi mambo mazuri yote uliyotamani yalienda vile ulivyotaka? Wahenga walipata kunena "kama mataminio yangekuwa farasi basi ningeyaendesha" if wishes was horses I could drive. Kuna vijana wengi wakiwa chuo wanakuwa na wishes kibao, lkn wakimaliza chuo mtaani wanapakuta pa Moto, huyohuyo mzazi unayesema asingependa mwanae awe boda boda ndo anakuwa wa Kwanza kumnanga mbele ya wadogo zake, oneni Kaka lenu pumbavu limekaa kihasara hasara linagombea rimoti ya TV na nyie, wenzake aliomaliza nao fomu foo walijihangaisha na shuhuli ndogo ndogo kama uchinga, boda boda na uchuuzi Leo hii Wana maendeleo kuliko hata Kaka yenu mwenyewe degree, huyo mzazi unayesema asingependa mwanae afanye kazi za laana hufikia kumfuru hata Mungu Kwa kuona kama alikula hasara kumsomesha mwanae.
 
Ama tutengeneze mfumo thabit wa vijana kurudi mashambani. Naunga mkono bodaboda sio ajira. Ajira ni kurudi mashambani ama viwandani tunapoteza nguvu kazi kubwa sana.
Ndio Mkuu, kilimo kinalipa sana, huwa ninafikiria serikali ikiwezeshe kile kidanda cha tractor cha JKT alafu igawe hizo tractor kwa mkopo au iuze bei nafuu, hii itasaidia sana
 
Hakuna hoja ambayo mtu yeyote anaweza kuleta kuhusu kuhalalisha bodaboda kama usafiri wa umma. Hoja hiyo itakuwa na mashiko, labda mbele ya watu wenye uelewa duni.

Watengenezaji wenyewe wanatoa tahadhari kuhusu matumizi ya pikipiki wanazotengeneza kuwa kwaajili ya usalama, pikipiki itumike na mtu mmoja tu kwa sababu kukiwa na abiria nyuma, mwendesha pikipiki akifunga break ghafla, abiria atamsukuma mbele dereva.
Nakubaliana naww!! Ndio maan nikasema CCM wameamua kucheza rumba la CDM!!
 
Wewe nikuulize matamanio aliyokuwa nayo Baba yako yote yalienda Vile alivotaka? Wewe binafsi mambo mazuri yote uliyotamani yalienda vile ulivyotaka? Wahenga walipata kunena "kama mataminio yangekuwa farasi basi ningeyaendesha" if wishes was horses I could drive. Kuna vijana wengi wakiwa chuo wanakuwa na wishes kibao, lkn wakimaliza chuo mtaani wanapakuta pa Moto, huyohuyo mzazi unayesema asingependa mwanae awe boda boda ndo anakuwa wa Kwanza kumnanga mbele ya wadogo zake, oneni Kaka lenu pumbavu limekaa kihasara hasara linagombea rimoti ya TV na nyie, wenzake aliomaliza nao fomu foo walijihangaisha na shuhuli ndogo ndogo kama uchinga, boda boda na uchuuzi Leo hii Wana maendeleo kuliko hata Kaka yenu mwenyewe degree, huyo mzazi unayesema asingependa mwanae afanye kazi za laana hufikia kumfuru hata Mungu Kwa kuona kama alikula hasara kumsomesha mwanae.
Ndio maana nimeandika hapo hiko ni kichaka cha kuzugia tu na labda kutafutia mtaji lakini shida ni kujaribu kuihalalisha kama ajira rasmi kwa kushindwa kwenu kuweka sera nzuri za kutengeneza ajira kwa waTanzania.
 
Hao chadema wakisema boda siyo ajira basi Watoe na alternative yao.

Ni kweli boda boda siyo jambo la Serikali kujivunia kuwa imeajiri.. Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha wanaajiriwa au wanajiajiri kwa kadiri ya fani zao..

Hivi hizi fani kama ualimu wa masomo ya sanaa si ingelikuwa heri wafute vyuo vyote.. Maana tangu jiwe aharibu mfumo mzima wa kuajiri kwa kigezo cha uhakiki... Mambo yapo hovyo hovyo.. Vijana wa 2015 wapo mtaani lakini wanaomaliza 2022.. Wanapata ajira chap "mama yupo kazini".

Matokeo yake Serikali inajificha kwenye kichaka cha ajira za bodaboda
Umenena vyema
 
Back
Top Bottom