Kumbe haya mambo yameota mizizi nimemsikiza Mh.Tundu Lisu(jembe)akiwataja aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya Zanzibar Kassim Hanga na wengine Abdulla Twalla,Mbungi Ussi na Othman Sheriff (kama nitakuwa nimekosea majina )kuwa walitoweka kufuatia kuhoji kwako kuhusu uhalali wa muungano,TL anasema hakuna anayeweza kueleza hawa watu walienda wapi lakini wote walikuwa viongozi ktk serikali ya mapinduzi Zanzibar!
Tumeshuhudia hata hivi leo watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari wanatekwa, wanauwawa na wenye roho za paka wanazindukia ktk chumba cha wagonjwa mahututi.Mifano ni kama Amran Kombe,Mwangosi,Kolimba,Dr...... na wengine wengi,hivi imefika wakati tuamini serikali inahusika?