Tundu Lissu avurugwa.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
HALI ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, juzi ilikuwa tete baada ya wabunge kuamua kumtolea uvivu kutokana na kauli zake za uwongo zilizodaiwa kuwa zina lengo la kupotosha umma.

Huku wakionyesha mifano, wabunge wengi waliosimama walimshambulia Lissu kwa kupotosha umma kuhusu masuala mbalimbali ya Muungano huku mengi yakidaiwa kuwa hayana tija wala ushahidi wa kutosha.

Hali hiyo ilijitokeza juzi wakati wa kujadili Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), awali, Lissu, aliwasilisha taarifa ya Kambi ya Upinzani.

Naibu wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ndiye aliyekuwa mwiba kwa Lissu, ambapo alisema mbunge huyo amezoea kusema mambo ambayo hayafahamu wala kuwa na uhakika nayo.

Mwigulu, ambaye alikuwa akijibu baadhi ya hoja zilizohusu wizara yake, alisema fedha za misaada kwa kawaida wafadhili hutoa maelekezo ambapo katika hilo, kiasi cha usawa wa asilimia 4.5 hutengwa kabla ya kufanya mgawo husika.
"Naomba tu kwanza niweke kumbukumbu sawa. Fedha wanazopaswa kupata Zanzibar, zimekuwa zikitolewa kwa miaka yote mfululizo kama kawaida.

"Unajua kama mambo huyajui, ni vyema ukauliza. Hata ndugu zangu wa Zanzibar, ni kwa nini msiwaulize viongozi wenu. Bahati nzuri kuna kitengo kinachohusu masuala ya fedha, kuliko kufanya mambo yasiyo na ushahidi.

"Kwa kwaida, fedha za wafadhili ambazo zitatolewa ndivyo mgawo utakavyofanywa. Sasa kama hii iliyoelezwa kwenye hotuba ya kambi ya upinzani kwamba zilitakiwa kiasi cha sh. Bilioni 32. Tulizozipata, tumetafuta uwiano wa 4.5, kiasi kilichobaki tutapeleka Zanzibar," alisema Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM).

Alishauri kuwepo kwa utaratibu wa kutoa takwimu zinazohusu fedha ili kuwezesha akina Lissu kuelewa kabla ya kuzungumza ndani ya bunge.
Pia, aliwahadharisha wabunge wa Zanzibar kuwa, mambo yaliyozungumzwa na Lissu katika hotuba yake, hayaonyeshi kuwa ana mapenzi ya dhati kwa wananchi wa visiwa hivyo.

"Unajua mtu huyo baada ya kuona chuki aliyoipandikiza Tanzania Bara imekosa mashiko, ameamua kuhamia Zanzibar. Mkivurugana yeye atabaki Singida.

Akinukuu maneno ya Lissu aliyoyatoa mwaka jana kuwa kero za Muungano si mali binafsi ya wabunge, alisema hata watanzania wanakerwa na ubaguzi unaofanywa na Wazanzibari, jambo ambalo ni kinyume cha anayoyasema sasa.
Katika kuonyesha Lissu ni kigeugeu, Mwigulu alisema aliwahi kusema kwamba, Wazanzibari walikuwa wakipendelewa kinyume na jinsi hotuba yake inavyoeleza kwa sasa.

"Yaani wakati mwingine napata shida kuamini kama Lissu ametokea Singida kule ninakotoka mie," alisema.
Awali, wakichangia hoja hiyo, Mohamed Amour Chombo, alimshangaa Lissu kuwa na mapenzi na watu wa Zanzibar huku awali alikuwa akiwapinga na kuwatolea maneno ya karaha na yenye kukera.

Chiombo, alisema muungano wa sasa baina ya CHADEMA na CUF ni sawa na kuchepuka na kwamba, CUF wanapaswa kuwa macho na Lissu.
"Ndugu zangu acheni mchepuko, rudini njia kuu, hawa wanawapenda leo wana nia yao si bure wenzenu ni sisi,'' alisema Chombo.

Chombo alisema hotuba ya Lissu ni ya uchochezi na kuwataka watanzani kutokubali kuingizwa katika uchochezi.
"Wewe unaposema muungano hauna maana ujue fedha za uwanja wa ndege zimetokana na nini, acheni michepuko rudini njia kuu.

"Kuna baadhi ya watu wakishapata wimbo Fulani, basi kila wakati atauimba huo huo wakati akienda kula, akienda wapi, sasa ni sawa na Lissu amepata wimbo wa muungano ni huo huo,'' alisema.
Aidha, kwa upande wake Steven Masele, aliweka rekodi sawa aliposema Wizara ya Mambo ya Nje imewahi kuwa na Waziri kutoka upande wa Zanzibar.

Masele, alisema hayo baada ya kuzuka hoja kwamba Muungano uliopo una upendeleo kwa viongozi wanaotoka Tanzania Bara.
"Jamani niwakumbushe tu kwamba Ahmed Hassan Diria (Marehemu), aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa," alifafanua Masele.

Wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge waliochangia ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri Samia Suluhu Hassan, aliahidi kushughulikia changamoto hizo na kuzipatia ufumbuzi wenye tija.
 
Mwaka 2010, Mh. Tundu Lissu aliibuka na tuhuma nzito kuhusu CUF na sababu ambazo zilikifanya CHADEMA kukaa mbali sana na "uchafu wa CUF" ndani ya mstakabali wa taifa pale aliposema,

Forward mpaka wednesday, 30th April utakutana na hotuba ya Mh. Lissu akiwasifiwa CUF na viongozi aliwashutumu na kusema,

 
MwanaDiwani,

Mbona hujagusia hoja za akina Kassim Hanga na wenzake aliowataja Tundu Lissu kwa majina? wako wapi?
Zamani wapinga muungano kama alivyo Tundu Lissu walikuwa wanashughulikiwa ipasavyo. Tumshukuru Mungu kwa kutuletea Rais mvumilivu sana kwa sasa
 
Ndugu, FaizaFoxy unaweza kunisaidia katika hoja utakazo changia ili kuboresha kile ambacho unadhani nilitakiwa nikiweke na sikuweka!.

Sijaona hizo hoja zinazowahusu akina Kassim Hanga kujibiwa, Jee, ni kweli waliuliwa na kuzikwa kwenye handaki moja na Nyerere na Karume?

Itakuwa ni kutetea maovu kama CCM na Serikali haijajibu hoja hizo na kuusema ukweli. Hazifai kupuuzwa hata kidogo.
 
Hapo ndipo utakapoona ulaghai wa Tundu Lissu
 
Hoja ya Kassimu Hanga ilishajibiwa jana na mtoto wa Hanga. Alisema kuwa baba yake alikufa kifo cha kawaida na alizikwa kwa mujibu wa taratibu zote za dini ya kiislam. Anasema pia kaburi la baba yake lipo
 
Unaweza kurejea kwenye mjadala wa jana hapa chini juu ya kifo cha Kassim Hanga

Yamemkuta Lissu: Kushtakiwa na mtoto wa Hanga kwa udanganyifu!
WanaJF,


Mtoto wa aliyekuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar, bwana Juma Abdallah Hanga, ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kumpeleka Tundu Lissu mahakamani kufuatia kauli za mwanasheria huyo wa CHADEMA kuwa za uongo, uchochezi na udanganyifu.


Mtoto huyo wa kwanza wa hayati Hanga, ambae pia ni mwanachama wa CCM, amesema baba yake alifariki kifo cha kawaida na kuzikwa kwa kufuata taratibu zote za dini ya kiislamu kwenye makaburi ya familia. Kwa maana hiyo maneno ya mwanasiasa Tundu Lissu kuhusu chanzo cha kifo cha baba yake ni ya kuokoteza na hayana ukweli wowote. Aliliambia gazeti la Zanzibar Leo.


Pia Juma Hanga amesema amepanga kwenda mahakamani kumshtaki mwanasiasa Tundu Lissu kwa upotoshaji wake kwa umma juu ya kifo cha baba yake kwa kuwa ana amini akiacha maneno hayo ya uongo yaendelee kusemwa yanaweza kuzua uchochezi utakao vuruga amani.


My take,


Ni wakati sasa kwa Lissu kuandaa ushahidi wake juu ya kauli yake ya kuuwawa kwa mwasisi huyo na kuonyesha kaburi hilo la pamoja analodai mwanasiasa huyo pamoja na wenzake wamezikwa. Hili suala halitaki porojo.
 
Hoja ya Kassimu Hanga ilishajibiwa jana na mtoto wa Hanga. Alisema kuwa baba yake alikufa kifo cha kawaida na alizikwa kwa mujibu wa taratibu zote za dini ya kiislam. Anasema pia kaburi la baba yake lipo

mtoto wa hanga ndio serikali ya CCM?.
 
zamani wapinga muungano kama alivyo tundu lissu walikuwa wanashughulikiwa ipasavyo. Tumshukuru mungu kwa kutuletea rais mvumilivu sana kwa sasa

zaifu..... Ndo mana hana maamuzi
 
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini huyo anayesema wamezikwa kwenye handaki asiwapeleke kwenye hilo handaki.

Yaani haya maswali yako nje ya mantiki . Hiyo hiyo serikali inadaiwa iliua halafu hiyo hiyo serikali inaulizwa tena kama iliua.

Mind you. The burden of proof rested with the accuser rather than the accused.
 
Hoja za lissu hazijawahi kujibiwa kamwe na mainterahamwe, zaidi ya kumshambulia yeye binafsi! Lissu bado ni mwiba mkali umagambani na interahamwe kiujumla!
 
Miaka 50 ya Muungano, mnzazibar mmoja ameshakuwa Waziri wa Mambo ya nje (Masele, 2014) safi sana muungano wa kipekee duniani (Mizengo, 2014) udumu milele.
 

Kumbuka kuwa hapa hatuongelei "proof", tunaongelea hoja ya watu waliosemekana wamepotezwa kwa kuupinga muungano wa Nyerere na Karume kwa namna moja au nyingine.

Hili suala si jepesi kama unavyolichukulia, na hizi ndio baadhi ya kero kuu za Muungano, wanaoongelewa ni watu na si vitu.

Serikali inatakiwa ije na majibu ya kuridhisha wananchi na si kuja na maswali mbadala. Kama walikufa walipokuwa chini ya mikono ya Serikali inabidi serikali ieleze na walipozikwa ni wapi na kwanini waliwekwa kizuizini.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…