Tundu Lissu atoboa siri

Tundu Lissu atoboa siri

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alisema kuwa Makinda na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge chini ya Mwenyekiti wake, Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi, walikuwa wameleta hukumu bungeni ya kuwasimamisha ubunge wabunge wanne wa CHADEMA kwa miezi sita.
Lissu alisema kuwa waligundua wananchi wataandamana hivyo Spika alimwita na kumshauri Ngwilizi aache kusoma hukumu hiyo.
“Walikuwa wameleta hukumu kutushtaki eti Lissu, Pauline Gekul, Joshua Nassari na John Mnyika tufungiwe kwa miezi sita lakini wakagundua mitaani hapatakalika wakaamua kuahirisha kuisoma.
“Tutumie nguvu ya umma kulazimisha utaratibu wa kupata Katiba mpya. Haki isipotendeka tuingie barabarani, tuikomboe nchi yetu kwa miguu yetu na mikono yetu,” alisema Lissu.
Katika mkutano huo, Lissu pia amesema kuna njama za kuchakachua maoni ya Katiba kutokana na idadi ya wabunge wa CCM, na muundo wa mabaraza uliotangazwa wa sasa, ambao wajumbe watateuliwa na kupitishwa na vikao vya maendeleo vya kata, ambavyo wenyeviti wengi ni wa CCM.
 
Jembe Lissu usijali waache waweke kuni kwenye jiko wamwage mafuta wenyewe wajifungie jikoni kisha watupe funguo chooni,wajimwagie mafuta miili yao alafu wawashe huo moto ndani ya jiko...Usiwastue maana hawa ni wachawi wamewanga usiku wamejisahau kama kumekucha na wanaonekana sura na uchi zao...hadharani
 
Back
Top Bottom