Samwel Sitta atofautiana na CCM wenzake bungeni kuhusu Polisi kutumika na wanasiasa. Amesema hoja hiyo haipaswi kupingwa ila kupewa muda wa kutosha kujadiliwa kama hoja binafsi.
Sina tatizo na hoja yako lakini naomba jaribu kuwa considerate kwa maana ya kujua kuwa rais ni amiri jeshi mkuu na pili polisi si watumishi wa umma na pili polisi wanatumia sheria zenu mbovu mlizoweka wabunge kupitia bunge lenu. Kama una hoja ni vizuri peleka hoja kwanza ya kufuta sheria.
MaCCM wanmtetea Nchimbi, ila ki ukweli polisi wanatumika kisiasa, ndio maana wanaccm wanamtetea, nimefurahi aliposema Nchimbi kajiita Dr kabla ya kupata PhD.
Samwel Sitta atofautiana na CCM wenzake bungeni kuhusu Polisi kutumika na wanasiasa. Amesema hoja hiyo haipaswi kupingwa ila kupewa muda wa kutosha kujadiliwa kama hoja binafsi.
Bunge hili linanichosha Sana wanakandamiza demokrasia waziwazi bora wabaki peke Yao wafurahi na kura yangu 2015 zitameza kura hamsini za wanaonizunguka kuhakikisha wabana demokrasia hawaingii bungeni
Kwa kweli Samweli Sitta ni mzalendo wa kweli.kamshauri Tundu Lissu apeleke hoja binafsi bungeni kwenye mkutano ujao wa bunge kuhusu jeshi la police kutumiwa na viongozi wa ccm.Lisu kakubali na nampongeza sana mzee SITTA.
Watake wasitake watakubali tu, hali halisi inajidhihirisha kwamba wanasiasa wanalitumia jeshi la polisi tena waziwazi kabisa, ukipingana na reality ujue iko siku utasutwa na aibu itakupata. Sitta hataki kusutwa!
Tumeshuhudia viongozi wa juu kabisa wa upinzani kama mbowe anakamatwa na polisi na kulala mahabusu na kuna makada wa kawaida tu wa CCM hata watuhumiwe vipi hata hawaguswi kabisa. Tena usishangae hivyo vyombo vya dola vikawatetea kabisa. Huo ndio utumikaji wenyewe. Mifano iko mingi.