Tundu Lissu amjibu Magufuli juu ya yeye kugombea TLS

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Anaandika #Tundu_Lissu

Mimi nina misimamo thabiti ya kutetea utawala wa sheria, utawala wa kikatiba na utawala bora. Ni mpinzani wa CCM kwa sababu hiyo. Kazi yangu bungeni imejengeka katika misingi hiyo. Kama nikichaguliwa Rais wa TLS huo ndio utakuwa msimamo wangu. Kwa bahati nzuri, misingi ninayoisimamia ndio pia ni malengo ya kisheria ya TLS kwa mujibu wa Sheria iliyoianzisha, yaani Sheria ya Chama cha Mawakili wa Tanganyika, Sura ya 307.

Kwa miaka mingi, TLS imeacha kusimamia misingi hii kwa hofu ya kuwaudhi watawala. Kumekuwa na dhana kwamba tukiwa wapole basi mambo yetu yataenda vizuri. Mambo ya nchi yetu hayajaenda vizuri kwa sababu ya ukimya wa TLS.

Na wala mambo wa mawakili walio wengi hayajaenda vizuri licha ya ukimya huu. Nikiwa Rais wa TLS ukimya huu utaisha. Wanaotaka kuendesha nchi yetu kama mali yao binafsi, bila kujali sheria na Katiba yetu; wanaotaka kutawala bila vizingiti vya sheria na katiba, hao ndio wanaoogopa kugombea kwangu. Je, ubunge wangu na Uanasheria Mkuu wangu wa CHADEMA utakuwaje???

Kazi ya Rais wa TLS sio full-time job, ni kazi ya muda tu. Sidhani kama Rais wa TLS ana ofisi ya kudumu pale Makao Makuu. Hata kazi ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA sio full-time job. Sina ofisi Makao Makuu ya CHADEMA. Kazi ya ubunge ni full-time lakini ina flexibility kubwa sana.

Nje ya vikao vya Bunge na Kamati, mimi ndiye ninayepanga ratiba yangu. Kwa sababu hiyo, licha ya majukumu mengi niliyo nayo, ninaamini nitapata muda wa kutekeleza majukumu ya Rais wa TLS. Wanaopiga kelele, akina Mwakyembe na Magufuli, wanaogopa sio CHADEMA bali wanaogopa TLS yenye nguvu na inayojitambua.

Hofu yao sio hofu ya CHADEMA, ni hofu kwamba wanasheria wakiamka katika umoja wao wana nguvu kubwa ajabu kwa sababu ya unique position waliyonayo kisiasa na kijamii. Kwa hiyo, kwenye uchaguzi huu wa TLS, choice iliyopo mbele ya wapiga kura sio choice ya CHADEMA au CCM bali ni choice kati ya TLS inayotambua wajibu wake na TLS inayoogopa wajibu huo. It's between change or status quo.
 
Hongera Tundu Lissu kwa kuamua kugombea nafasi hiyo ndani ya TLS.

Ila ufahamu jambo moja ktk hii nchi shida si watu kujua sheria,tuna wana sheria wazuri sana Tanzania nachokiona Mimi unaweza kuwa Rais mzuri sana wa TLS lakini unaweza ukajikuta unabaki peke yako ktk kupambana na Viongozi wasiofuata sheria za nchi.

Tumeona mfano wa vita vya madawa ya kulevya hapa juzi Makonda kupiga kelele tu tumeona upinzani ulivyojitokeza dhidi yake kila kona ya nchi utafikiri hatujui vijana wanavyoangamia na drugs.

Kwa hiyo Mh Tundu Lissu watanzania ni wazuri sana kwa kuongea sana lakini utekelezaji ni zero take care wanasheria wenzako wasije wakakutelekeza na uongozi wako pale utakapo lianzisha jambo.
 
Lissu yupo sahihi. Hoja yake ina mashiko. Kazi ya ubunge ipo very flexible muda mwingi wabunge wanakuwa huru na hii inamaanisha anaweza kupanga muda wake vizuri kutekeleza kazi zake zote zinazomuhusu. Kusema kwamba ataingiza mambo ya siasa na kuitetea Chadema kwa mgongo wa TLS si sahihi. Nadhani zipo kanuni zinamzuia kufanya hivyo. Nashangaa taharuki na woga wa Magufuli unatoka wapi.

President Magu acha kufuatilia mambo yasiyokuhusu. Wewe ni kiongozi mkuu wa nchi jikite kwenye agenda za kuwaletea wananchi maendeleo.
 
kwa mtizamo wangu binafsi, ninaunga mkono wanasiasa wakereketwa kutogombea katika mambo ya kitaaluma.

binafsi sitazami vyama vya wanataaluma kama vyama vya kupambana na serikali bali vyama hivi vinatakiwa kuwa katika position ya kutetea taaluma yao kufanya kazi.

pale walipopewa nafasi watasifia lakini kwa mwanasiasa mkereketwa hawezi kusifia jambo lililofanywa na siasa anazozipinga hivyo hapo kutakuwa tatizo.

kuna mambo vyama vya wanataaluma vinatakiwa kukaa chini na kuandaa ushauri lakini wanasiasa hawako tayari kushauri bali kukimbilia kwa wananchi kushitaki na hata mambo yaliyo ya kweli kuyapotosha ili kupata sapoti ya wananchi katika siasa zao.

tunachokitegemea kutoka TLS ni chama hiki kuwa neutral hakilalii upande wowote wa siasa au kundi lolote bali wao kuegemea upande wa haki kwa mujibu wa sheria tu.

ni kwa bahati mbaya sana wanasiasa wengi wako blinded na itikadi zao, wanaamini itikadi zao ndizo sahihi na za wengine zote ni makosa. wanasiasa wetu ni mashabiki na sio watu wa kusimamia ukweli wa kumsaidia mtanzania.

TLS inahitaji mtu mwenye busara, asiye na njaa kwa maana mkiweka mtu mwenye njaa anatumia nafasi hiyo kujifanyia promosheni za kuganga njaa zake, inahitajika mtu asiye na ushabiki wa kundi lolote bali awe ni mtu anayeweza kukiongoza chama kusimamia haki.

serikali ikifanya mambo ya kukiuka haki waseme wazi, wanasiasa wasio madarakani wakifanya mambo ya kukiuka haki waseme wazi, penye kuhitaji kukaa na serikali kushauriana wafanye hivyo.
 
Back
Top Bottom