Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 65,812
- 156,946
Kwa Watanzania wenye akili timamu mtakubaliana nami kuwa miaka 5 ya awamu hii ya 5, kimekuwa kipindi kigumu sana kilichojaa;
Hofu
Mashaka
Umasikini uliotopea
Ombwe la kiuongozi nk.
Watanzania wengi mioyo yao imejaa mashaka na kutojiamini tena.
Ni enzi za watawala wachache kuneemeka na kufanya walitakalo bila kuwajibishwa na yeyote.
Lakini baada ya Tundu Lissu kuteuliwa kuwa mgombea wa urais na kuanza kitema cheche, naona mioyo ya Watanzania ikihuishwa tena kuingia ulingoni kuipigania Tanzania yenye neema.
Wito wangu, tumuunge mkono huyu shujaa aliyejitoa Sadaka.
Kuthubutu kuyanyooshea kidole mapungufu ya huyu mfalme yahitaji moyo lakini huyu mwamba amedhamiria.
Kwa masikio yangu nimewasikia ccm wengi wakibadili gia angani na kuahidi kumpigia kura Lissu.
Shime Watanzania tuipiganie heshima ya nchi yetu nzuri ya maziwa na asali, upendo na mshikamano