GE2025 Tundu Lissu afikishwa tena mahakamani leo Oktoba 9, 2025, Mawakili wa Jamhuri kumuhoji shahidi namba moja wa Jamhuri

GE2025 Tundu Lissu afikishwa tena mahakamani leo Oktoba 9, 2025, Mawakili wa Jamhuri kumuhoji shahidi namba moja wa Jamhuri

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amefikishwa mahakamani katika Kesi hiyo ambayo mshtakiwa anajitetea mwenyewe, leo imekuja kwaajili ya Mawakili wa Jamhuri kumuhoji 're-examination' shahidi namba moja (1) wa Jamhuri ACP George Willbert Bagyemu baada ya mshtakiwa kumaliza kumuhoji maswali ya dodoso (cross examination) hapo jana, leo pia inatarajiwa huenda shahidi wa pili (2) wa Jamhuri akaanza kutoa ushahidi wake Mahakamani hapo.

Kutoka kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam tunakusogezea kuona namna Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu alivyofikishwa Mahakamani hapo leo, Oktoba 09.2025 kwaajili ya kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili.

Jana tuliishia sehemu ya 75 na leo tunaendelea na sehemu ya 76

Pia Soma:

Part 76
Imepigwa high court

Majaji wanaaingia Mahakamani.

Watu wamesimama na Majaji wanakaaa sasa.

Karani anasoma kesi criminal Case No. 19625 Jamhuri dhidi ya TUNDU LISSU.

Jaji anawaita Mawakili wa Serikali.

Anasimama Wakili, Naitwa Renatus Mkude wakili wa serikali mkuu, Nikisaidiana na Ajuaye Silanga, Nassoro Katuga, Winiwa Kasala, Cuthbert Mbilinge.

Mshtakiwa yuko in good health na ana afya tele tunaomba kuendelea.

Mhe. Lissu: Ndugu zangu niliowaandika na kuwaomba waje hawajaruhusiwa kuingia inaonekana kuna mamlaka makubwa zaidi ya kuzuia nani aingie na nani asiingie.

Hili wahe majaji sio jambo dogo ni jambo kubwa na ni suala la kikatiba nitalisema na nitaendelea kusema watu lazima wawe na unimpeded entrance to the doors of justice.

Akimaanisha watu inabidi waruhusiwe kuingia mahakamani bila kuzuiwa.

Ninaomba tuendelee Waheshimiwa.

Majaji wanaandika hapa alichosema Lissu.

Jaji Ndunguru anasema naomba tuendelee na hilo nitalitolea ufafanuzi baadae kidogo.

Anaitwa Katuga anasimama sasa kuanza Rejoinder.

Anasimama Katuga kwa sauti ndogo anasema Wah. Majaji nisaidie kumkumbusha kuwa yuko kwenye kiapo.

Shahidi anakumbushwa kuwa yuko chini ya kiapo.

Katuga anasema Sasa shahidi nikupe pole kwa yaliyokukuta kwa siku 3.

Tutauliza maswali yaliyo kwenye hati ya mashtaka.

Uliulizwa kuhusu kufanya uchochezi ni uhaini sasa tuelezee hapa kufanya uchochezi ni uhaini?

George anajibu: Kufanya uchochezi kwa nia ya kuitisha serikali ni uhaini.

Katuga: Shahidi ulionyeshwa hati ya mashtaka iliotumika kukuhoji kwanza uliulizwa kuhusu yale maneno yaliyokuwa quoted kwenye hayo maneno ukaulizwa neno serikali limo humu?lakini ukajibu haliko...ila kimaudhui limo.

George anaanza tena kuyarudia yale maneno ya Lissu anaishia kusema kuwa neno serikali halipo hapo ila kimaudhui limo.

Katuga: Kaulizwa pia kuzuia uchaguzi ni kosa ukatujibu kuzuia kwa njia halali sio kosa elezea majaji ni kivipi?

George: Kwenda mahakamani kuandika petition kuzuia uchaguzi sio kosa ila kuzuia uchaguzi kwa vitisho ni kosa la uhaini.

Katuga: Sasa shahidi tufafanulie kwa mujibu wa maelezo ya P nani alichapisha maneno hayo ukasema ni TAL ukaulizwa pia mimi nina password za jambo TV ukasema sio mara ya mwisho ukaulizwa nani aliechapisha ukasema ni TAL na shahid P sasa fafanua ulimaanisha nini?

George: Mwenyekiti wa CDM Kwa kuongea na waandishi wa habari wewe ulichapisha

😃😃😃😃 vituko leo.

Katuga: Pia eneo hilohilo ukaulizwa ni nani aliepeleka maneno mtandaon ukasema sio mtu wa jambo tufafanulie hayo maneno?

George: anasema nilimaanisha mtu wa jambo ni mwandishi wa habari ambae TAL aliongea nae kwa malengo hayo maandishi yachapishwe mtandaoni.

Katuga: Kuna swali hapa ulianza na kupewa somo kuwa hii ni nchi ya kidemokrasia ukaenda mbele ukaelezwa kuwa kuipinga serikali ni kosa la uhaini ukajibu kwa njia halali sio kosa wafafanulie waelewe kwa njia halali inaruhusiwaje?

George: Kama nilivoelezea kwenye maelezo ya halali kukosoa sio kosa kosa ni vitisho kwa serikali watu wanaguna kidogo..

Katuga: for the purpose ya maswali yanayohusu mashtaka sisi tunaishia hapa.

TAL anateta na mawakili hapa wanaonekana wakicheka sana 😆

Naona Mawakili wa Serikali wamekosa maswali ya kumuuliza shahidi wake, ukiona mpaka Mawakili wa Serikali wanakosa maswali ya kumuuliza Shahidi wao basi ujue Mshitakiwa alimshona Bwana George kisawa sawa wanaona wakiuliza maswali mengi kwenye Rejoinder yao Shahidi ataharibu zaidi.

Wanasema wanae Shahidi Mwingine ambae ni yule Kaaya.

Tunasubiri aitwe.

Part 77
Renatus Mkude, Wakili Mkuu wa Serikali anasimama anasema tuendelee na shahidi mwengine naona yuko hapa.

Jaji anauliza mshtakiwa uko sawa tuendelee?

Mhe. Lissu anajibu niko sawa naona tunaenda vizuri.

Watu wanacheka.😀😀😀

Jaji Nduguru : Unaitwa nani shahidi?naitwa Insp. John Kaaya. umri: miaka 45 ila hafananii hii miaka🤣kachoka sana sijui ndo shughuli za polisi.

Dini yako: Mkristo Anaapishwa hapa.

Renatus Mkude: Anasema kuwa shahidi wa pili ataongozwa na Job Mrema wakili wa Serikali Mkuu.

Anasimama hapa Job Mrema anasema kabla ya kuanza kuuliza maswali ufahamu kuna amri ya mahakama kuu iliotolewa ya kulinda mashahidi haitakiwi kutaja majina ya baadhi ya mashahidi pia uongee kwa sauti.

Eleza mahakama hii umeajiriwa lini? Nimeajiriwa 2006 baada ya kuhitimu mafunzo ya ukuruta nilioanza mwez wa 8 2005 na kuhitimu February 2006

Eleza mahakama mafunzo ulipata wapi? Nilipata chuo cha polisi zanzibar.

Anarudia tena kuuliza kapata mafunzo wapi eleza katika mafunzo hayo ulijifunza nini?

Anasema nilijifunza mbinu mbalimbali za kivita, sheria mbalimbal mathalani sheria ya ushahidi, criminal procedure, kazi za polisi, investigation skills na First aid

Baada ya kumaliza mafunzo haya ulipata nini?nilitunukiwa certificate of competence

Baada ya kumaliza mafunzo hayo ilikuwaje? anajibu Nilipangwa makao makuu ofisi ya upelelezi.

Unaposema makao makuu unamanisha nini? Makao Makuu ya Polisi Mkurugenzi wa upelelezi.

Ilipofika 2020 ilitokea nini?

Anajibu nilihamishiwa kitengo cha Cybercrime dawati la doria mtandaoni.

Eleza Mahakama hii ulikuwa unafanya nini?

Ins. Kaaya anajibu Kupeleleza makosa ya jinai, kukamata watuhumiwa, kufikisha watuhumiwa mahakamani pamoja na kutoa ushahidi.

Shahidi unaeleza Mahakama ulihamishwa kwenye kitengo cha makosa ya mtandao hebu eleza kiko chini ya nani?

Ins. Kaaya anajibu Kitengo cha dawati la doria mtandaon kiko chini ya DCI

Eleza ofisi ya DCI ilikuwa wapi?

Ins. Kaaya; Kwanzia mwaka 2006 ofisi ya DCI ilikuwa jengo la Police Hq Dar baadae Serikali kuhamia Dodoma na ofisi zikahamia huko.

Wewe kwa sasa majukumu yako unatekeleza ukiwa wapi?

Ins. Kaaya : Ililokuwa Police HQ Dar es salaam.

Anaendelea Job Mrema kuuliza.

Shahidi ulieleza Mahakama ulihitimu mafunzo yako 2006 ulivyohitimu mafunzo hayo ulikuwa na Cheo gani?

Ins. Kaaya ; Baada ya kuhitimu 2006 nilipewa cheti cha Polisi na kuwa na cheo cha Constable.

Shahdi cheo hiko cha constable ulikaa mda gani?

Ins. Kaaya : Nilitumikia hadi 2021

Na baada ya cheo hiko ulipanda cheo gani?

Ins. Kaaya : Niliteuliwa kuhudhuria mafunzo ya special seargent katika chuo cha polisi moshi (CCP)

ILIKUWA LINI?

Ins. Kaaya ; mwezi wa tano 2021 hadi mwezi wa 8, 2021.

Katika mafunzo hayo nini ulijifunza?

Ins. Kaaya : Nilijifunza military and safety training, police duties, investigation skills, elimu ya msingi ya sheria ya ushahidi, criminal procedure.

Kuna jambo lIngine tena?

; Gbv Na lingine ni drill and parade, cybercrime investigation skills.

Kuhitimu mafunzo hayo kuna kitu ulijifunza hujakitaja?embu ieleze mahakama mafunzo hayo ilikuwa mda gani?

Ins. Kaaya : Miezi 3

Ulieleza mafunzo haya ulipata moshi huko moshi ni wapi?

Ins. Kaaya : Moshi iko mkoa wa Kilimanjaro

Ebu eleza mahakama matokeo ya mafunzo hayo ulipata nini?

Ins. Kaaya : nilihitimu cheti cha mahudhurio Certificate of attendance

Cheti hicho kilikuja na nini?

Ins. Kaaya : kiliambatana na cheo cha Special seargent

Eleza mahakama chet hiko ulitunukiwa lini?

Ins. Kaaya : nilipaata mwezi wa 8, 2021

Baada ya kuhitimu chet hiko ulienda wapi?

Ins. Kaaya : nilirudi kwenye kituo changu cha kazi Dar es salaam

Shahidi ilikuwa lini hio?

Ins. Kaaya : Mwaka 2021 mwezi wa nane

Kitengo chako kiko wapi tena?

Ins. Kaaya : ilikokuwa Makao Makuu ya Polisi, Dar es salaam.

Kitengo ulichorejea ni kipi?

Kaaya: kitengo cha makosa ya mtandao dawati la doria mtandaon

Part 78

Wakili wa Serikali Job Mrema anaendelea kumuongoza Shahidi namba 2 wa Jamhuri huyu wakuitwa Ins. Kaaya, Mzee wa doria mitandaoni.

Huyu kazi yake kufuatilia pages za watu ambao wanakosoa Serikali humu kwenye mitandao na kuwachoma kwa mabosi zake.

Eniwei tuendelee

Shahidi eleza mahakama baada ya cheo hiko cha seargent ulipanda cheo gani?

Ins. Kaaya: mwezi wa 10 2021 niliteuliwa na mwajiri wangu Jeshi la Polisi Tanzania kuhudhuria mafunzo ya mkaguzi msaidizi wa Polisi..katika chuo cha Polisi Moshi.

Ilikuwa lini hio?

Ins. Kaaya : Mwezi wa 10, 2021

Shahidi baada ya uteuzi huo nini kilifuata?

Ins. Kaaya : nilienda hudhuria mafunzo CCP Moshi

Ilikuwa lini?

Ins. Kaaya : Mwezi wa 10, 2021

Ieleze Mahakama mambo gani ulijifunza au mafunzo yalihusu nini?

Ins. Kaaya . miongon mwa mafunzo ni Police duties, sheria ya makosa ya jinai, cybercrime, majukumu ya mkaguzi, Crime prevention, Community police,Military training, Human rights

Embu ieleze mahakama mafunzo hayo yalichukua mda gani?

Kaaya : yalichukua muda wa takribani miezi 4

Baada ya miezi 4 ulipata nini?

Kaaya : nilipata cheti cha Certificate of Attendance na Assistant Inspector of Police

Ilikuwa mwaka gani?

Kaaya : mwezi wa 2, 2022

Baada ya kutunukiwa cheti na kumaliza mafunzo ulirudi wapi?

Kaaya : nilirudi kwenye kituo changu cha kazi Dar es salaam

Shahidi uliporejea kituo cha kazi ulifanya kwenye kitengo gani?

Kaaya : makosa ya jinai dawati la doria mtandaon

Shahidi umejitambulisha kama insp John kaaya eleza cheo cha insp ulipata lini?

Kaaya : cheo hiko nilipewa mwaka 2025 mwezi wa 6, nilipewa kutokana na utendaji kazi mzuri kazini.

Nani alikupa hicho cheo?

Kaaya; Nilipatiwa na Jeshi la Polisi Muajiri wangu.

Mbali na Mafunzo nje ya Kipolisi yapo mengine?

Kaaya; Nimejifunza pia Forensic Cyber Crime in Modern Investigation niliyapatia Chuo cha Polisi Dar es salaam.

Pia nimeweza kujifunza Cyber Crime Management, digital forensic, Basic Computer Skills in Cyber Crime Investigation, pamoja na Cyber Ivestigation Skills. Haya yote nilihitimu 2020 na nikapata Cheti.

Je kuna mafunzo mengine mbali na hayo?

Kaaya ; Ndio, Sisco Certified Support Technician in Cyber Security. Mafunzo haya nilisoma chuo cha JR institute of Information Technology kilichopo Kisutu Dar es salaam na ilikuwa mwaka 2024.

Mambo muhimu uliyojifunza kupitia course hiyo?

Kaaya; Ulinzi wa Data nilijifunza, Networking, Computer hacking aahhh sio hiyo ni Ethical Hacking. Mafunzo ni ya miezi mitatu yalikuwa na haya yalikuwa mwaka 2024 ambapo nilipata cheti pamoja na ujuzi pia.

Je kuna mafunzo mengine tena?

Kaaya; Pia nilisoma Computer Hacking Forensic Investigation. (CHFI) Nilijipatia katika mafunzo ya Unique Academy pale Upanga Dar es salaam na yalikuwa ni mafunzo ya miezi miwili. Mambo niliyojifunza ni upelelezi wa kisayansi katika mifumo mbalimbali ya Computer.

Ulisema unafanya kazi wapi hivi?

Kaaya ; Kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandao online patrol desk na sasa majukumu yangu ni kufanya doria katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kumbuka anayeuliza Maswali ni Job Mrema na anayejibu maswali ni John Kaaya ambae ni Inspector wa Polisi.

Anamuuliza Doria mtandaoni ni nini?

Kaaya :ni kwamba tunaperuzi mitandaoni kwa ajili ya kung'amua makosa mbalimbali ya kijinai yanayofanywa na watumiaji wa mitandao hiyo na mitandao yenyewe ni instagram, tiktok, X na kadhalika.

Hiyo Doria inafanyikaje?

Kaaya: Doria tunafanya kwa kuperuzi katika mitandao hiyo niliyosema baada ya kung'amua kama kuna kosa la jinai nawasilisha kwa wakubwa wangu kama kuna kosa basi hatua stahiki zinachukuliwa.

Mitandao inatumikaje na watu?

Kaaya: Ni lazima wawe na account yaani kujisajili kuweka taarifa zako katika uwanja wa mtandao husika na ukishaandika basi taarifa hizo zitaonekana kwa watumiaji wengine wa mitandao hiyo.

Part 79
Wakili wa Serikali Job Mrema anaendelea kumuongoza Mzee wa Doria Mitandaoni kujibu maswali.

Je unajua utaratibu wa kusajili mtandao wa YouTube?

Mzee wa Doria Mitandaoni: Ndio mtumiaji unapaswa kuwa umeandaa taarifa zako binafsi kama Username, email address pamoja na passwords utakayoitumia baada ya hapo utaingia uwanja wa YouTube na kuandika taarifa hizo kadri zitakavyokuwa zinahitajika. Ukishakamilisha watakupa terms and condition na baadae watakupa channel URL.

Job Mrema anamuuliza hiyo Channel URL ni nini?

Kaaya: yaani uniform resource locater ni unique ID yaani utambuzi wako binafsi ambayo inakuwezesha kuendelea kutumia mtandao huo wa YOUTUBE ama hiyo Account yako.

Hiyo unique ID unamanisha nini?

Kaaya; Maana yake ni utambuzi wa mtumiaji wa Mtandao wa YOUTUBE ambao haufanani na mtu mwingine.

Ili mtu aingie anapaswa kufanya nini kwenye huo mtandao?

Kaaya; utaingia kwenye ukurasa wa YouTube kwa kutumia username yako na password uliyokwisha umeandaa baada ya hapo utakuwa unaweza kuona maudhui mbalimbali yaliyochapishwa na watumiaji mbalimbali wa mtandao huo.

Job Mrema huwa ana mbwembwe sana na makelele na kipara chake utadhani ana kitu cha maana tutakiona, anarudia swali moja mara tatu tatu, kutupotezea muda tu.

Huyu Shahidi wa leo anaonekana ni muoga sana muda wote anajibu maswali akiwa ameinama

Unaweza kudhan kama amelazimishwa kuja hapa Mahakamani na hapa bado hajaingia kwenye 18 za Mhe. Lissu.😀

Haya tuendelee

Insp. John kaaya anasema jambo lingine muhimu kuhusu mtandao wa YOUTUBE unaweza kuweka maudhui na baadae ukafuta na unaweza kutumia kuona maudhui ya watu wengine waliyoyaweka.

Live stream ni nini shahidi nasikia uliitaja?

Insp John Kaaya : Live streaming ni kitendo cha kurusha ama kuchapisha tukio katika mtandao wakati tukio hilo likiwa linatendeka moja kwa moja.

Huwa unafanya maandalizi gani unapoingia kazini kabla hujafanya majukumu yako?

Insp John Kaaya ; Huwa ninaandaa vitendea kazi vyangu ambavyo ni Computer maalumu ya Jeshi la Polisi, Police notebook na Internet access. Kingine huwa naandaa umeme ni muhimu nihakikishe umeme upo.

Mashahidi wa Jamhuri Bwana eti naandaa Umeme, utadhan anakampuni ya kufua umeme.😀

Taratibu binafsi zingine ni zipi huwa mnachukua?

Insp John Kaaya : Huwa nahakikisha chumba kinakuwa salama kwa maana mtu ambae hahusiki asiingie.

Baada ya kuandaa hivyo vyote huwa unafanya nini?

Insp John Kaaya : Nawasha Computer kwa kutumia username yangu binafsi na password na baada ya kuingia nafanya ukaguzi wa Computer kama inafanya kazi na pia natumia anti virus ku scan kama virus wapo na pia nakagua Internet access ili kuniwezesha kufanya kazi.

Je hiyo Computer unayizungumza ni ya namna gani na ina vitu gan?

Insp John Kaaya : Hii ni software na ina program maalumu zinazotuwezesha kufanya doria mtandaoni.

Hizo programu maalumu zinaweza kufanya mambo gani?

Insp John Kaaya : Zinatusaidia kwa ajili ya ku monitor mitandao mbalimbali niliyoitaja. Zinatuwezesha kupakua maudhui yenye ujinai. Doria mtandaoni huwa tunafanya kwa muda wa saa 24 za siku na pale katika dawati tunaingia kwa zamu.

Sasa SHAHIDI tuambie tarehe 04/04/2025 ulikuwa shift gani?

Insp John Kaaya : Majira ya saa 12 asubuhi nilikuwa Zamu kazini.

Huko kote ilikuwa mbwembwe kujifanya anajua kazi yake hapa sasa ndio anaingia kwenye kesi.😀

Ieleze Mahakama tarehe hiyo jambo gani lilitokea kuhusu hii kesi?

Insp John Kaaya : Wahe. Majaji mnamo tar. 04/04/2025 niliingia zamu saa 12 asubuhi baada ya kufika ofisini niliandaa vitendea kazi vyangu kama kawaida.

Niliweza kuwasha Computer mali ya jeshi la Polisi kwa kutumia username na password baada ya kuwaka nikaweza kuikagua na kugundua iko katika hali nzuri ya kufanya kazi.

Part 80
Job Mrema: ukawa unafanya nini?

Inspector Kaaya: nikawa naperuzi na niliingia YouTube. Nilivyoingia YouTube nilibaini machapisho mbalimbali ya video. Mojawapo ya Chapisho ni katika ukurasa uliosajiliwa kwa majina ya JAMBO TV na niliona picha iliyokuwa imeambatana na maneno TUNDU LISSU USO KWA USO NA WATIA NIA MAJIMBONI. NO REFORMS NO ELECTION NJIA PANDA.

Baada ya kuona picha mjongeo hiyo niliweza kuchezesha picha mjongeo hiyo ili niweze kuona maudhui yaliyochapishwa.

Lengo la kuchezesha lilikuwa ni nini?

Kaaya; Ili nione maudhui yaliyopo humo ni nini?

Sasa ili iweje ukishaona hayo maudhui?

Kaaya: Lengo ni kubaini kilichozungumzwa.

Kwanini uliingia sasa?

Kaaya: Nilishangaa kuona video ile ina watizamaji wengi elfu na 39 nikaona ngoja na mimi niingie kuona kuna nini na watizamaji 300 niliona wamecomment.

Sasa shahidi unaweza kueleza mahakama majukumu yako ni yapi?

Kaaya: Majukumu yangu ni kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii kubaini makosa yanayofanywa.

Sasa ieleze mahakama hiyo sjju ya tarehe 04/04 uliingia kule kufanya nini?

Anasimama Lissu kuwa hilo swali lilishajibiwa alishasema aliingia kuwa video ile ilikuwa imetizamwa na watu wengi na waliocomment nikashawishika ni maudhui gani yamechapishwa humo.

Baada ya kuingia ulibaini nini humo ndani shahidi?

Kaaya anajibu nilivyotizama niliweza kubaini baadhi ya matamshi yenye viashiria vya jinai.

Viashiria hivyo ni vipi?

Shahidi anasema viashiria ni aliposema kuwa kwa kuwa hatuna access na hizo server za tume na Mapolisi ndo hao mnawaona na vibegi vya kura feki.

Mhe. Lissu anasema haya mambo ya vibegi feki yalishakataliwa na Mahakama siku ya juzi hauwezi kuletwa leo tena unahusiana na kesi iliyopo kisutu.

Naona Majaji wanajadili kidogo.

Job Mrema anajibu kwamba kwa upande wa Jamhuri tunapinga hilo pingamizi kwasababu kesi ya Mukisa Biscuits imeeleza pingamizi lazima liwe na sheria iliyotajwa.

Kuibuka ubishani wa kisheria hapa kati ya Mawakili wa Serikali na Mhe. Lissu

Sasa anasimama Mh. Lissu kuwajibu mawakili wa Serikali kuhusu hilo pingamizi dogo la namna ya kutoa ushahidi.

Waheshimiwa majaji nimesikiliza majibu marefu ya hawa wenzangu: nilidhani wasingebisha.

Cha ajabu wamemuachia anijibu huyu Job Mrema wakati yeye hakuwepo sasa mkimkubalia huyu na mlikataa kwa yule PW1 ambae ni George.

With all due respect nafikiri Mrema alikuwa anaongea jambo ambalo halifahamu.

Unaleta kesi ya Mukisa ambayo yenyewe inahusu mapingamizi ya mamlaka ya Mahakama.

Sasa hiyo kesi unatutajia leo ya nini kwenye hatua hii ambayo tupo sasa?

Waheshimiwa Majaji naomba mlikubalie ombi langu.

Majaji wanajadiliana hapa

Kwenye chuma cha Mahakama kuna ukimya fulani hivi nakumbuka tukiwa watoto mkiwa darasani mnapiga kelele ghafla mnajikuta wote mpo kimyaaaaa, tulikuwa tunasema shetani kapita ndo kama huo sasa.😀

Tunasubiri Majaji wamalize kujadiliana then watoe uamuzi kuhusu ombi la Mhe. Lissu.

Part 81

Mahakama imeanza muda huu.

Majaji wameingia.

Mheshimiwa Lissu alivyoingia kabla ya Majaji amewaambia Mawakili anzeni kuandaa submission ya No Case to Answer maana hakuna kitu hapa.

Mawakili wa Serikali wanacheka.

Anasema Jaji Ndunguru kuwa sasa kabla hatujaahirisha kulikuwa na suala hapa la kulitolea uamuzi mdogo atasoma mwenzangu hapa Jaji Kiwonde.

Anaanza hapa Jaji Kiwonde. Shahidi alisema habari za vibegi vya kura feki na mshitakiwa alipinga hapa.

Baada ya sisi kutafakari swali la msingi tulijiuliza kama mahakama hii ilishatoa amri ya kuzuia maudhui yaliyoonwa yasitolewe ushahidi.

Mahakama siku ya Jumatatu ilisema masuala yanayohusu vibegi vya polisi na utendaji kazi wa mahakama ya Tanzania.

Hicho ndio tulichokizuia siku ya Jumatatu.

Kwenye kesi hii tumeona shahidi namba mbili anasema alichokiona kwenye mtandao wa Kijamii.

Lakini yule wa kwanza yeye alikuwa anatoa ushahidi kama anafahamu mambo hayo.

Huyu anaeleza alichokiona na sisi tunamwambia asifike mbali aishie kwenye kusema alichoona.

Pingamizi halina mashiko.

Shahidi aendelee kutoa ushahidi wake.

Hiyo ndo ruling mtaelewa wenyewe maana binafsi nimejitaidi kuelewa lakini naona Jaji ananivuruga tu hapa ila ndo Mahakama zetu tutafanyaje.

Haya tuendelee

Job Mrema: Sasa shahidi endelea

Kaaya: Lissu alisema hawa mapolisi mnawaona wana vibegi vya kura

Maneno mengine alisema.. kwakuwa majaji nao ni watu wa Rais na wao ni MACCM. Wanataka wapandishwe vyeo kwenda kwenye mahakama za rufani kuteuliwa kwenye commissions na kwenye tume ndiko kuna hela.

Hayo maneno niliona akisema Mshitakiwa.

Akaeleza tena kwahiyo MAHAKAMANI HAKUENDEKI.

Maudhui mengine aliyotamka ni kwamba NA MIMI NATAKA NITEULIWE KWENYE KACHEO FULANI NCHI HII,

UKisema na mimi unamaanisha nini shahidi?

Jaji anaingilia sasa ndugu MREMA Shahidi anasema hayo maneno aliyasema Lissu wewe ukisema anamaanisha nini akisema NA MIMI unamuuliza hilo swali kwani ni yeye ndio ameyasema huyo si ana quote tu?

Job Mrema: Sawa Mheshimiwa Jaji naomba nisamehewe nilidhani ni maneno yake anasema.

Anaendelea Kaaya: anaanza kusema maneno mengine lissu alisema "Mkutano wetu unasema NO REFORMS NO ELECTION, Wamesema Kitu kimoja sahihi hapa kwamba tunapanga kufanya uasi, ni kweli tunaashiria uasi.

Tutakinukisha vibaya sana, tutakinukisha sana sana.

Kitu nimegundua ni kwamba haya Mapolisi yamekaa huko kituoni kukariri Hotuba ya Mh. Tundu Lissu ambayo yeye hata hakatai hayo maneno wa kila siku ya Mungu wanayarudi tu kama Sara ya Baba yetu.😀

Nafikiri hawana kitu cha kukitolea ushahidi.

Eniwei tuendelee

Job Mrema: Ulivyomaliza kusikiliza Video ulibaini nini?

John Kaaya: Nilibaini matamshi yale yana viashiria vya jinai.

Job Mrema: Shida gani?

John Kaaya: Maneno yavibegi niliona yanapotosha umma.

Jaji Kiwonde: sasa mnaona huko mnaanza kuelekea tena kwenye vibegi.

Mhe. Lissu: Mhe. Jaji huu ushahidi aachwe aendelee kuutoa tu maana nilipinga mkasema ni sahihi aendelee sasa nafikiri asikatazwe acha aseme tu. 😂

Jaji Ndunguru: Basi aendelee hakuna shida.

Job Mrema: Ieleze Mahakama Shahidi ulikuwa unaelezea viashiria vya makosa kwenye maneno hayo.

John kaaya: Waheshimiwa Majaji pamoja na hayo matamshi niliyosema, pale aliposema kuwa mahakamani hakuendeki kwasababu majaji ni watu wa Rais na ni MACCM niliona taarifa hiyo ina viashiria vya jinai. 😂😂

Anaendelea pia shahidi kusema kanuni za utumishi wa umma zinakataa watumishi kuwa wafuasi wa vyama vya siasa.

Yani Job Mrema na John Kaaya wamekutana hapa ni pipa na mfuniko. Wanzingua sana yani wanapa uvivu kuandika maana kuna muda wanaongea hivi havieleweki

Kaaya kuna muda anaongea sauti ya chini hadi Jaji anamwambia ongeza sauti ni muoga muoga sijui Polisi wa wapi huyu au ndio mjanja akiwa anapiga doria mtandaoni.

Part 82

John Kaaya: Pia aliposema Mahakamani hakuendeki ila Mahakama ni chombo cha kutoa haki na kutoa maamuzi ya mambo mbalimbali yanayobishaniwa.

Hivyo anavyojulisha umma kwamba hakuendeki ni kutoa taarifa ya uongo kwa umma na kuitishia serikali 😂

Kaaya ana akili hata kidogo huyu yani Mahakamani hakuendeki eti ni kuitishia serikali.😀😀😀

Job Mrema: Baada ya kuitizama hiyo video nini kingine ulikisikia.

John Kaaya: Lissu alisema Tutaenda kuzuia uchaguzi, tutazuia uchaguzi kwasababu wanasema tunahamasisha uasi na tutaenda kuuvuruga sana sana.

Natamani mngekuwa mnamuona huyu shahidi aiseee, kituko cha mwaka.😀

John Kaaya anaendelea: Kwa matamshi hayo niliyosema waheshimiwa majaji niliona kuna viashiria vya jinai.

Uchaguzi huandaliwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria hivyo kuzuia uchaguzi kwa kuhamasisha uasi bila kufuata utaratibu ni kosa.

Haya yote aliyafanya lengo lake ni kuitisha serikali ambayo ndio msimamizi mkuu wa Sheria na kulinda amani.

Nilichogundua TANZANIA haitakuja kushinda kesi yoyote kimataifa kama mashahidi wetu ndio hawa na Mawakili wetu wa serikali ndio hawa akina Job Mrema kama nchi tunasafari ndefu.🥹

Anaendelea hapa John Kaaya: Baada ya kuona hayo maudhui nilichukua POLICE NOTEBOOK yangu na ku note maudhui hayo niliyosema na nilinote link ambayo hayo maudhui yanahusika.

Hapa namaanisha ni ukurasa wa Jambo TV pamoja na mtoa maudhui ndugu Tundu Lissu.

Job Mrema: Kila muda unasema Tundu Antipas Lissu unamfahamu yuko wapi?

John Kaaya: anasema namfahamu na yupo hapa mahakamani.

Job Mrema: Yuko wapi?

John Kaaya: Yule pale anampungia.

Majaji wanasema ukipunga mkono maana yake umemuonesha nani?

Watu wanacheka. 😀😀😀

Shahidi ananona aibu kumuonesha Lissu kwa kidole.

Hawa watu wanawasababishia watu watende dhambi wasizotaka.

Huyu shahidi kiukweli usikute hajataka kabisa kuja kufanya hii kazi maana namuona kama hana amani😂

John Kaaya anaendelea: Baada ya kuona hayo nilimjulisha mkuu wangu wa kazi ambae ni mkuu wa kitengo cha doria mtandaoni.

Job Mrema: Hiki kitengo kipo ofisi gani?

Kaaya: Kipo ofisi ya DCI.

Job Mrema: Hiyo picha mjongeo alimaliza kuitizama muda gani?

John Kaaya: Nilimaliza kuyatizama kwenye majira ya saa nne asubuhi siku ya tarehe 04/04/2025.

Job Mrema: Ulitoa taarifa kwa mkuu wako wa kazi ulitoa taarifa saa ngapi?

Jibu: Nilipomaliza kuitizama ndio nilitoa taarifa kwa mkuu wangu wa kazi.

Job Mrema: ulivyotoa taarifa ulipata matokeo gani?

John Kaaya: Nilielekezwa kwenda Polisi kanda maalumu Dar es salaam kwa ajili ya kwenda kumjulisha Afande SSP George. Juu ya maudhui yale.

Job Mrema: Utekelezaji wa majukumu yako ikawaje?

Kaaya: Nilisimama kutekeleza majukumu mengine nilienda kuonana na Afande George ambae kwa siku ile alikuwa ni Naibu Kamanda wa Upelelezi Kanda ya Dar es salaam na ilikuwa tarehe hiyo hiyo Tar. 04/04/2025.

Job Mrema: Ikawaje?

John Kaaya: Nilivyofika nikamkuta Afande George na kumjulisha dhumuni la ujio wangu kwake.

Nilimwambia nimeelekezwa na mkuu wa kitengo cha makosa ya mtandao kuwa nije kukupa taarifa ya nilichokiona huko mtandaoani.

Baada ya kumjulisha alinielekeza, nimuonyeshe picha mjongeo zile na nilimuonyesha kupitia simu janja yake kwa kuingia kwenye ukurasa wa Jambo TV.

Job Mrema: Ikawaje tena?

John Kaaya: Basi nilichezesha picha mjongea ile kwa kumuonyesha baadhi ya vipande nilivyobaini vina viashiria vya jinai.

Hapa nazungumzia ile video ya tundu lissu uso kwa uso na watia nia majimboni No reforms, no election.

Job Mrema: Nini kikafuata?

John Kaaya: Afande George alichukua Police Notebook yake na kujaza taarifa kuhusiana na picha mjongeo ile na baada ya kuchukua baadhi ya taarifa muhimu, aliniamuru kurudi eneo langu la kazi kuendelea na majukumu mengine.

Ikawa iviiii.....

"Anzeni kuandaa submission za no case to answer, hakuna kesi hapa" Mhe. Tundu Lissu Akiongea na Mawakili wake mara baada ya break fupi.



Part 83
Job Mrema: Tarehe 07/04/2025 nini kilitokea?

John Kaaya: Nakumbuka nilikuwa zamu kazini. Wakati naendelea na majukumu ya kila siku. Alinipigia afande SSP George majira ya asubuhi akinielekeza niende Ofisini kwake.

Ulivyofika ofisini ikawaje?

Kaaya : Alinikumbusha kuhusu ile taarifa niliyompelekea aliniamuru nirudi Ofisini ninapofanyia kazi za doria mtandaoni na kupakua video ile katika ukurasa wa Jambo TV niipakue na baadae nimpelekee.

Nilivyopokea amri ile nilirudi ofisini kuifanyia kazi.

Nilipofika ofisini niliandaa vitendea kazi vyangu kama vile computer na notebook. Nilikagua utendaji kazi wa computer yangu na nilichukua police notebook yangu na kuchukua ile link na kuinakili kwenye program maalumu kwa ajili ya kupakua yale maudhui.

Job Mrema: Halafu ikawaje?

John Kaaya: Niliandaa Flash mpya aina ya XIOXIA yenye ukubwa wa GB 8 niliiweka kwenye computer na kuifanyia virus scanning na baadae nikaifanyia formating ili kuondoa data yoyote iliyomo mle kwenye flash.

Ndipo nikaichukua ile video na kuihifadhi katika flash hiyo.

Job Mrema: wakati unaipakua hiyo video ilikuwa na muonekano gani?

John Kaaya: ilikuwa na watizamaji elfu 52 na waliocomment mia tatu.

Kingine nilibaini ile video ilichapishwa tar. 03/04/2025 kwenye ukurasa wa Jambo TV.

Job Mrema: Kuhusu maudhui yake ulifanya nini?

John Kaaya: Niliweza kuisecure flash ile kwa ku encrypt na password.

Nilichukua pia PF 145 ambayo ni Exhibit label na niliilabel kile kielelezo na kukipa alama DM.

Radio call la askari limeanza kuita humu ndani mahakama imesimama kidogo.

Majaji hawajasema kitu wanasema haya tuendeleeee. 😂😂

Kuna mambo majaji wanakausha ila Katuga huwa ni mnoko sana angekuwepo angeweza msingizia hata Chadema yeyote hapa maana anatuchukia sana.😀

Job Mrema: Baada ya kufanya labelling uliendelea na hatua gani nyingine?

John Kaaya: Niliondoka ofisini na kuonana na afande SSP GEORGE na kwamba nimeshapakua na kuyahifadhi.

Hiyo ilikuwa ni tarehe 07/04 majira ya saa 9 mchana baada ya kufika ofisini kwa George nilionana nae na kumjulisha kwamba maelezo aliyonipa nimekamilisha.

Baada ya kumjulisha afande George alichukua diary yake na kunijulisha kuwa ameshafungua kesi ambayo ina Reference No. DSMZ/CID/PE.101/2025

Pia aliniambia niorodheshe hiyo kesi namba kwenye kile kielelezo ambacho niko nacho yaani flash aliniambia niandike maelezo yangu nimpatie.

Job Mrema: nini kikafuata?

John Kaaya: Aliniambia nikipeleke kielelezo kwa ACP Malugala mtunza vielelezo. Nilijaza namba ya jalada kwenye kielelezo. Nilichukua kielelezo DM na kukipelekea kwa ACP Malugala.

Job Mrema: Tar. 08/04 kilitokea nini sasa?

John Kaaya: Nilikuwa zamu kazini na nikiwa naendelea na majukumu yangu.

Alinipigia afande SSP George akiniamuru niende Ofisini kwake, nilisitisha shughuli zangu na kwenda kuonana na Afande George.

Job Mrema: Nini kiliendeleaa ulipofika?

John Kaaya: Nilimkuta yupo na Mpelelezi.
alinikumbusha kuhusu tukio la Tarehe 07/04/2025 kuhusu uwasilishaji wa kielelezo kwake.

Aliniambia nimpatie yule mpelelezi password katika kielelezo DM.

Nilichukua POLICE NOTEBOOK yangu kwa ajili ya kujikumbusha password yangu na kuinakili kwenye notebook ya mpelelezi niliyoamuriwa nimpatie.

Job Mrema: Je hiyo video ya tarehe 04/04/2025 utaitambuaje ukiiona?

John Kaaya: Hiyo video naweza kuitambua kwa maudhui yanayotamkwa, mzungumzaji amevaa kombati ya Kaki, nyuma ya mzungumzaji kuna rangi za Bendera ya Taifa pia itakuwa kwenye flash disk.

Job Mrema: Kwani Maudhui yaliyokuwepo kwenye hiyo video ni yapi?

Hawa watu wanatupotezea muda kabisa wanaulizana maswali yale yale yani, Wanakera sana.

John Kaaya: Anaanza kusema yale maudhui ya Lissu.

Part 84

Job Mrema: Hiyo Flash utaitambuaje pia?

Kaaya: Nitaitambua ina GB 8 na ina rangi nyeupe.

Job Mrema: Waheshimiwa Majaji ni hayo tu kwa shahidi huyu.

Vituko sana. Muda wote shahidi anatusumbua nitaitambua video, nikiona kitu fulani na kitu fulani. 😂

Mwisho wa siku kumbe video yenyewe na flash hiyo italetwa na shahidi mwingine sio yeye.

Makaratasi mengi wanatumalizia misitu tu bila sababu ya msingi.😂

Ngoja sasa aanze kusokotwa.

Kinachofuata sasa ni CROSS EXAMINATION yaani maswali ya DODOSO kutoka kwa CRISTIANO RONALDO AU MESSI wa Sheria Mh. Lissu.

Jaji anasema Mshitakiwa unasemaje?

Mhe. Lissu: Mh. Jaji huyu Shahidi asiende hivi hivi naomba mnipatie nusu saa nianze nae leo leo au hata kama mkiniruhusu niendelee nae hadi saa mbili usiku niko tayari.

Jambo lingine off record jana niliwaahidi nitawaleteeni kitabu nilichoandika miaka mitano iliyopita kinaitwa "Remaining in the Shadow" kuhusu mambo ya Uchaguzi pia.

Nimebeba copy tatu hapa naomba niwape na Mawakili wa Serikali Copy moja nao wakasome ili wajue mambo mengi wasidhani mimi ni mtu wa mchezomchezo na waache kutumika tu.

Majaji pia nawapatieni copy moja.

Jaji Ndunguru anasema sasa unatupatia copy moja tunasomaje si bora ungetoa copy mbili?

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji nikiwapa mbili mtagombana sana maana mko watatu.

Watu wanacheka.

Jaji Ndunguru: Sasa wewe ugomvi wetu haukuhusu, tupe hizo copy mbili sisi tutajua cha kufanya.

Watu wanacheka. 😂😂😂

Mhe. Lissu: Basi nyie Vijana anawanyooshea Wakili Kisabo na Mahinyila kuwa hakikisheni kesho mnaongeza copy zingine 4 zije hapa.

Jaji Ndunguru anasema sasa jamani tutaendelea kesho.

Muda umeshakwenda.

Shahidi kapumzike na Mshitakiwa na wewe kajiandae na kesho tuendelee na Cross Examination saa tatu kamili asubuhi.

Inapigwa Courttttttt kubwa sana.

Majaji wanasimama na kutoka.

Kesi imeahirishwa hadi kesho asubuhi saa tatu.

Tukutane kesho wandugu.

 
[Mbishi @bizy94 / @X]
20251009_162027.jpg
20251007_191606.jpg
20251007_191610.jpg


🚨 #UPDATES_KESI_YA_UHAINI 🚨 Tundu Lissu's treason case in Tanzania is a SHAM! Witnesses like Insp. Kaaya fumble, recycle weak claims of "incitement" from a YouTube video, alleging Lissu’s words threaten the state. Tanzania’s laws (Penal Code, Cap 16, S.39) define treason as acts like waging war or aiding enemies📌NOT criticizing elections or police! The prosecution’s case is crumbling; they’re grasping at straws with no solid evidence. Lissu’s right to free speech is under attack! @BBCWorld CNN Aljazeera Reuters @HRW, expose this injustice! #FreeTunduLissu
#FreePolepoleNow #wakeupTanzania #riseupTanzania #STRUGGLE_FOR_AFRICA #AFRICA_UNITED #PAN_AFRICANISM #SamiaMustGo ⚡
 
Back
Top Bottom