Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu leo Jumatatu, Oktoba 6, 2025, amefikishwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam ambapo kesi yake ya uhaini inayomkabili itaanza usikilizwaji kamili wa kesi hiyo.
Soma: CHADEMA: Polisi wawatawanya Wananchi waliofika Mahakamani kufuatilia Kesi ya uhaini ya Lissu, kadhaa wajeruhiwa
Kwa mujibu wa hati ya wito wa kufika mahakamani iliyopelekwa kwa pande zote, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mfululizo kuanzia leo, mpaka Oktoba 24, 2025.
Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, kwa tuhuma za kutamka maneno kuhusiana na kuzuia kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.