Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,100
- 136,721
Zile kamata kamata zisizo na kichwa wala miguu dhidi ya Tundu Lissu na zile kesi uchwara zote zilizofunguliwa dhidi yake naamini ndizo zilizompandisha chati huyo bwana katika huu utawala wa awamu ya tano.
Mara nyingi kama si zote hizo kamata kamata zilitokea baada ya yeye kutoa maneno makali dhidi ya serikali na Rais.
Kuna nyakati alikuwa yupo sahihi na nyakati zingine alikuwa mzushi tu. Kwa mfano, aliposema nchi inaendeshwa kwa misingi ya kikabila na kikanda, huo ulikuwa ni uzushi tu. Zilikuwa ni propaganda tu.
Uzushi na propaganda kwenye siasa ni jambo la kawaida sana na la kutegemewa kuwepo. Mwanasiasa asiyezusha, asiyetia chumvi na asiyepiga propaganda atakuwa kakosea fani.
Sasa mimi naamini hii serikali inafanya makosa sana katika kuwakamata na kuwafungulia mashitaka watu wanaoipinga na kuikosoa. Hizo kesi wanazofunguliwa ni vichekesho mtupu.
Katika kukosea kwao huko, naamini serikali imeunda lidubwana [monster] ambalo kuanzia sasa kwenda mbele itakuwa vigumu kulidhibiti. Lidubwana hili nalifananisha na lile lidubwana la kwenye filamu ya Frankenstein.
Lidubwana hilo ndo Tundu Lissu. Hebu fikiria haya:
Jamaa keshaonyesha kuwa haogopi kuikosoa serikali wala kumsema vibaya Rais [mambo ambayo ni ya kawaida sana kwenye demokrasia na ambayo yanahimizwa kufanyika].
Uthubutu na ujasiri wake huo ndio umepelekea yeye kukamatwa kamatwa na kufunguliwa vikesi uchwara.
Uthubutu na ujasiri huo huo ndo si ajabu umepelekea yeye kushambuliwa kwa risasi kwa lengo la kutaka kumuua. Sijui kwa uhakika ni nani anayehusika na hilo shambulio.
Sasa pata picha atapopona na kurejea tena nchini na kuendelea na harakati zake pale alipoishia!
Serikali itamfanya nini huyu mtu? Wataendelea kumsumbua na hizo kamata kamata zao na kumfungulia hivyo vi kesi uchwara mtu ambaye tayari ana huruma za umma kwa ujumla wake kutokana na yale yaliyomtokea?
Sioni utamkamataje na kumfunga mtu ambaye kanusurika kuuwawa namna ile. Akili yangu inaniambia hata dhamiri yako, kama ni safi, basi itakusuta tu.
Hakika hii serikali ya awamu ya tano ilibugi stepu katika namna ya kumkabili Lissu na sasa amekuwa lidubwana ambaye anaweza asidhibitike tena.
Ni muda tu ndo utaotueleza.....