JAPUONY
JF-Expert Member
- Jul 16, 2010
- 383
- 186
Wadau wa JF,
Kwa muda wa siku tatu nimepiga kambi hapa katika jimbo la Mhe. Tundu A. Lissu, Wananchi wa Jimbo hili wanadai HAWATOMRUDISHA Mhe. Lissu Bungeni kwa sababu zifuatazo:
1. Wanadai toka apate Ubunge hajawahi kupeleka maendeleo yoyote Jimboni kwake
2. Toka apate Ubunge amekuwa akipiga kelele Dodoma; kelele amabazo haziwasaidii wao wa jimbo lake
3. Kali zaidi, Wanadai Lissu hana adabu kuwa alimtukana Mzee Nyerere na Karume Bungeni na kuwa wao hao wazee wanawaheshimu kuliko hata yeye Tundu Lissu
4. Wanadai amekuwa DALALI wa kutembea na FISADI ambaye yeye mwenyewe aliwaaminisha kuwa ni fisadi. Nakuwa, alivyogundua kuwa Lowassa siyo fisadi hakuwahi kurudi kwa Wananchi wake na Watanzania kwa ujumla kuwaambia kuwa Lowassa siyo fisadi. Wanahoji, kuwa, Lissu kagundua lini kuwa Lowassa siyo mwizi kama alivyowaaminisha? Je, yeye anamfahamu Lowassa kuliko wana-CCM walioamua kumkata pamoja na umaarufu wake?
Wana UKAWA, Mie nimewaletea hayo ili mjue namna ya kwenda kukomboa jimbo hilo na muwe na majibu ya hoja hizo za Wananchi.
Kwaherini kwa leo.