Tuncel:"DNA ya Bayern Munich ni Ushindi tu"

KENGE 01

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
1,592
3,839
Na KENGE,

25 March 2023 ni siku ambayo Kocha Thomas Tuchel(TT)anasaini mkataba wa kuinoa miamba ya ujerumani Bundasliga BAYERN MUNICH baada ya kumfuta kazi Julian Nagelsmann.

Katika EXCLUSIVE Interview TT ameweka wazi sababu ya yeye kukubali kwa haraka dili la kuwanoa miamba hao wa Bayern moja wapo ikiwemo historia nzuri ya ushindi wa makombe waliyonayo miamba hao wa Ujerumani.

"Nilikubali kwa haraka kuifundisha bayern kwasababu team hii ina vinasaba (DNA) vya ushindi" Amesema TT

Licha ya kuwindwa na team nyingi kubwa ikiwemo Tottenham na R.madrid kocha TT amesema amekuwa akipokea ofa nyingi baada ya kutimuliwa CHELSEA lakini ofa ya kuinoa bayern aliipa kipaumbele na kuikubali kwa haraka zaidi.

Ameongeza
"Bayern inakikosi ambacho kinaweza kucheza EPL na kushinda back to back na naamini ndio team tishio baranu ulaya"

"Ninayo Furaha na uhakika tutashinda makombe yote yatayokatiza mbele yetu"

Ikumbukwe TT alishinda Kombe la UEFA champions dhidi ya Man.City ndani ya mwaka mmoja akiwa chelsea na kwasasa team yake mpya Bayern inashika nafasi ya pili Bundasliga ikizidiwa point moja na B.Dortmund pia Ipo hatua nzuri ya Robo fainali UEFA Champions league huku akipangiwa na mahasimu wake wababe wa wingereza MANCHESTER CITY

Je Bayern wamelamba dume kwa TT?

Pia soma>>

Tunachokijua!!
KENGE 01
20230325_155257.jpg
 
Nauhakika atawatoa city nje ndani yaani kama alishinda na Chelsea ndo ashindwe kuwafunga akiwa na Bayern? Tumekaa pale
Hawa buyern wameyakanyaga nakuambia ,Bora wasingefukuza kocha ...

Yaani huyo TT tushakuwa na hasira nae internally,ndio maana Toka atufunge final hajawahi kutufunga Tena ....na Chelsea tutaendelea kumpa kichapo cha mbwa Koko mpaka tutakapo chukua CL ndio cheslea ataweza kutufunga ....

Maana kila tukikutana na cheslea huwa tunakumbuka CL ...
 
Hawa buyern wameyakanyaga nakuambia ,Bora wasingefukuza kocha ...

Yaani huyo TT tushakuwa na hasira nae internally,ndio maana Toka atufunge final hajawahi kutufunga Tena ....na Chelsea tutaendelea kumpa kichapo cha mbwa Koko mpaka tutakapo chukua CL ndio cheslea ataweza kutufunga ....

Maana kila tukikutana na cheslea huwa tunakumbuka CL ...
Kwamba wameyakanyaga? Ngoja tuone ila kitu nauhakika nacho pale Alianza hamchomoki

Kuhusu kuifunga Chelsea ata Azam wakikaa vizuri wanaifunga hii chelsea ya G.potter
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom