adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 15,479
- 33,510
Moja kwa moja.
Mimi ni muumini wa ushahidi, habari zozote bila ushahidi wa uhakika na wa kuamika huwa nazikataa moja kwa Moja au naiweka katika kundi la tetesi na kuzifanyia uchunguzi ili kujua ukweli na uhalisia wa habari yenyewe kwa uhakika.
Siku za karibuni kumekuwa na wimbi la watu wengine ni kama wakosoaji wa serikali na wengine kama wafuaji wa yale ya ndani yaliyojificha yaliyotokea na yanayoendelea , sasa tukija kwenye Mada husika binafsi nimesoma nyuzi kadhaa za Britanicca haswa hizi episode mbili za jana ila sikuona solid evidence katika nyuzi zake zote zaidi kujikita katika masimulizi na tuhuma tu.
Swala la ushahidi nalitilia umakini mkubwa sababu katika ulimwengu huu mtu ni rahisi sana kupelekwa na upepo wa propaganda au kusuka vizuri habari ya uwongo na ikaonekana ukweli au kutia chumvi kwenye ukweli wenyewe kutoka na uadui , chuki , maslahi nk #EvidenceIsAPower
Sasa kama ushahidi wa kuaminika katika habari na tuhuma ukawa unapuuzwa tunaweza kutenganisha vipi habari tuzazoziamini zinazoletwa na watu na zile stori maarufu za kutunga na soga za vijiwe vya kahawa ? tukipuuza Hilo na tusihoji mtu yeyote anaweza kuwa source of information akaamka na habari yeyote anayoiona ya sawa na tukamuamini pia.
Nyongeza ;
Mhusika ana historia ya kutoa tabiri feki na mikeka yake mingine kuchanika vibaya . Pamoja na hiyo baadhi ya members wamekuwa wakimtuhumu kutoa taarifa za uongo na kukurupuka katika majambo , hapo inatia mashaka kidogo kumuamini Moja kwa moja.
Hii Screenshot nimetoa katika comment ya uzi wake mmoja wa codes ambao umefeli vilevile kuleta matokeo tarajiwa.