Tunawezaje kuamini mabadiliko ya salamu?

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,829
Hili ni swali kwa wote UKAWA ASILIA na UKAWA Mabadiliko.

UKAWA ilianza kama muungano usio rasmi wa wananchi wanaotaka rasimu ya katiba ya judge Warioba.

Hapa UKAWA ilikuwa hot kweli kweli na ilikuwa serious.

Ukawa hii ilijumuisha watu mbalimbali kutokea kwenye vyama vya siasa na asasi za kiraia.

Baadae tukaona mchujo wa kimyakimya ukianza kushika kasi na hatimaye tukafika hatua ya kubaki na viongozi wa vyama vinne vya kisiasa.Baadaye zaidi tukaona ajenda ya katiba mpya inatulizwa pembeni na kukawekwa makubaliano ya Kusimamisha mgombea urais kupitia UKAWA.

UKAWA ukatoka kuwa umoja wa katiba ya wananchi na kuwa umoja wa vyama vinne.

Hapa tukaanza kusikia Badiliko la kwanza la Salamu yaani badala ya salamu moja ya Peoplez(kumbuka koti hili la UKAWA lilikuwa na rangi ya kakh) tukapata salamu nne...yaani peoplezz,Nccr,Haki na Motomoto.

Hata kwenye ufunguzi wa kampeni za urais tulizisikia.

Muda haukupita Salamu tatu zikaanza kufifia huku ile ya peoplezz ikirudi kwenye chati kabla ya mwenyekiti kuja na salamu mpya yaani mabadiliko yote yataitwa lowassa.

Kampeni zikashika kasi lakini kukawa na ukakasi wa watu kuikubali au kuizoea hii salamu ya mabadiliko ...sasa leo naona ile salamu ya asili imerejeshwa tena yaani peoplezzz!!

Sasa mimi najiuliza je mabadiliko ni salamu au?

Watanzania wanajiuliza mabadiliko ni salamu?

Wale wa vyama vitatu yaani CUF,NCCR na NLD wanajiuliza mabadiliko ni kwenye salamu tu?

Tunaendelea kukumbushwa kuwa hatuendi kuchagua Genge la kishikaji kuingia ikulu bali taasisi yenye ukamilifu wa kimaono,kimipango,kirasilimali,kimiongozo na yenye kila sifa ya kuitwa taasisi.

Tunaenda kuchagua taasisi yenye utambulisho kutokana na muundo wake,sera zake na misimamo yake.

Mimi siamini katika mabadiliko ya salamu hata kidogo kwani siko tayari kubadilishiwa salamu baada ya kupiga kura.

TUPINGANE KWA HOJA!
 
Kwa akili yako huwezi kuelewa hata kidogo, labda muuluza kwanza Magufuli kwanini kaziiga zote mpaka kukataa Mdahalo
 
Jipambanue ww ni wa mrengo upi kati ya hiyo maana sisi wa cuf kitambo tulishaona pale ni usanii na ubabaishaji tukaamua kukacha coalition ya kinafiki isiyo na makubaliano rasmi.
 
Hili ni swali kwa wote UKAWA ASILIA na UKAWA Mabadiliko.

UKAWA ilianza kama muungano usio rasmi wa wananchi wanaotaka rasimu ya katiba ya judge Warioba.

Hapa UKAWA ilikuwa hot kweli kweli na ilikuwa serious.

Ukawa hii ilijumuisha watu mbalimbali kutokea kwenye vyama vya siasa na asasi za kiraia.

Baadae tukaona mchujo wa kimyakimya ukianza kushika kasi na hatimaye tukafika hatua ya kubaki na viongozi wa vyama vinne vya kisiasa.Baadaye zaidi tukaona ajenda ya katiba mpya inatulizwa pembeni na kukawekwa makubaliano ya Kusimamisha mgombea urais kupitia UKAWA.

UKAWA ukatoka kuwa umoja wa katiba ya wananchi na kuwa umoja wa vyama vinne.

Hapa tukaanza kusikia Badiliko la kwanza la Salamu yaani badala ya salamu moja ya Peoplez(kumbuka koti hili la UKAWA lilikuwa na rangi ya kakh) tukapata salamu nne...yaani peoplezz,Nccr,Haki na Motomoto.

Hata kwenye ufunguzi wa kampeni za urais tulizisikia.

Muda haukupita Salamu tatu zikaanza kufifia huku ile ya peoplezz ikirudi kwenye chati kabla ya mwenyekiti kuja na salamu mpya yaani mabadiliko yote yataitwa lowassa.

Kampeni zikashika kasi lakini kukawa na ukakasi wa watu kuikubali au kuizoea hii salamu ya mabadiliko ...sasa leo naona ile salamu ya asili imerejeshwa tena yaani peoplezzz!!

Sasa mimi najiuliza je mabadiliko ni salamu au?

Watanzania wanajiuliza mabadiliko ni salamu?

Wale wa vyama vitatu yaani CUF,NCCR na NLD wanajiuliza mabadiliko ni kwenye salamu tu?

Tunaendelea kukumbushwa kuwa hatuendi kuchagua Genge la kishikaji kuingia ikulu bali taasisi yenye ukamilifu wa kimaono,kimipango,kirasilimali,kimiongozo na yenye kila sifa ya kuitwa taasisi.

Tunaenda kuchagua taasisi yenye utambulisho kutokana na muundo wake,sera zake na misimamo yake.

Mimi siamini katika mabadiliko ya salamu hata kidogo kwani siko tayari kubadilishiwa salamu baada ya kupiga kura.

TUPINGANE KWA HOJA!

Jaribu kushirikisha na ubongo wako kwanza kabla ya kupost hizi ngonjera zako, Ukawa asilia na Ukawa mabadiliko ulizianzisha lini na wapi maana sisi tunatambua UKAWA ni moja ndio maana tupo wamoja na adui yetu mkubwa ni MKOLONI MWEUSI ccm. TUTOKOMEZE HIKI KIRUSI FISIEM. Umbea mwingine peleka lumumba waliko waimba mipasho na umbea wa kila rangi.
 
Hahaha....gia ya angani sitoisahau aisee ....hadi mwanasiasa niliyekuwa naapa mbele za watu kwa kumuamini kama Tundu Lissu anakaa meza moja na EL,Masha, Sumaye etc kisa ndio njia pekee ya kuiua CCM? sitosahau huu mzaha wa kihistoria kwenye siasa zetu .....
 
Wewe utakuwa umeisikia ukawa mwezi wa saba.
Acha wanaoelewa waje na hoja
 
Yaani hawa walioshindwa hata kutikisa hata mkutano mkuu huko CCM pamoja na kuapa kutachimbika? ...Leo kuchimbike wakiwa upande wa pili ? ....hoja hakuna, zaidi ya mbwembwe za bendera na mafuriko ambayo kama una akili japo za chekechea utajua si kura .....
 
Hahaha....gia ya angani sitoisahau aisee ....hadi mwanasiasa niliyekuwa naapa mbele za watu kwa kumuamini kama Tundu Lissu anakaa meza moja na EL,Masha, Sumaye etc kisa ndio njia pekee ya kuiua CCM? sitosahau huu mzaha wa kihistoria kwenye siasa zetu .....
Ni mzaha wa kihistoria kwa kweli!
Lakini wanasema malipo ni hapa hapa duniani...kumbuka kuna waliomwaga damu kwa ajili ya mwaka huu lakini ndio hivyo tena.

Ni mwendo wa kubadili salamu na ishara tu.
 
Mtoa mada naomba nikupongeze kwa kutambua kuwa ukawa ni wabunifu sababu hata nagufuli pia hupenda kuiga walivyovibuni. Mwisho hueleweki unatakaje kwa nani na faida yake ni nini
 
Sina hiyana kupongeza ubunifu wa salamu na ishara...lakini hoja yangu ni moja tu hayo ndiyo mabadiliko yanayotakiwa??
 
Ni mzaha wa kihistoria kwa kweli!
Lakini wanasema malipo ni hapa hapa duniani...kumbuka kuna waliomwaga damu kwa ajili ya mwaka huu lakini ndio hivyo tena.

Ni mwendo wa kubadili salamu na ishara tu.

Kama wanaweza kubinafsisha mabadiliko ya kweli yaliyopangwa kwa miaka zaidi ya ishirini na kuishia kuja na vijisababu rahisi ambavyo kwa kujua wanao majuha watakaounga mkono watashindwa kubinafsisha hadi ikulu kwa hekaya hizi hizi?
 
Yaani hawa walioshindwa hata kutikisa hata mkutano mkuu huko CCM pamoja na kuapa kutachimbika? ...Leo kuchimbike wakiwa upande wa pili ? ....hoja hakuna, zaidi ya mbwembwe za bendera na mafuriko ambayo kama una akili japo za chekechea utajua si kura .....
Oktoba 26 ndio mwisho wa kuwasikia halafu shughuli itarudi kwa mwenyekiti kwani hata wabunge na madiwani kutakuwa na pigo kubwa sana nje ya matarajio.

Na hapo salamu zitakua hazieleweki tena.
 
Du la KUKU...........
 
Oh! my god! kwani salam ni mabadili? hapana isipokuwa msemo huo unaanza ivo kwa sababu mlengwa wa uraisi ndie mleta mabadiliko na mabadiliko yenyewe yanaanza na katiba mpya ambayo ni yawananchi na ndo msingi wa kila kitu na ndomaana huwezi sema magufuli mabadiliko sababu yeye ni ataendeleza pale walipoishia wenzie na si vinginevyo, ko ukisema mabadiliko lowasa ndo mfumo mzima kuanzia hata kumtambulisha kwa community nzima itaelewa lowasa ni nani
 
Huu muungano wa UKAWA walau basi ungekuwa base ya kupata wabunge wengi wa upinzani ....lakini ni kama walioungana ni viongozi while huku chini wanahujumiana kimya kimya ....kuna kila dalili CCM wakatuumiza kuliko hata 2010 tofauti na matarajio ya wengi .....ndio maana wengine tunashindwa kuvumilia huu uhuni ....
 
Mtoa mada hapo umeelewa kama bado niulize tena
 
Huu muungano wa UKAWA walau basi ungekuwa base ya kupata wabunge wengi wa upinzani ....lakini ni kama walioungana ni viongozi while huku chini wanahujumiana kimya kimya ....kuna kila dalili CCM wakatuumiza kuliko hata 2010 tofauti na matarajio ya wengi .....ndio maana wengine tunashindwa kuvumilia huu uhuni ....

Acha wajaze mafuriko ya guinea bissau halafu ccm itachukua itaweka waaa
 
Back
Top Bottom