Kama viongozi mbali mbali katika idara mbali mbali wangekuwa na dhamira ya kweli kuongeza ufanisi na kupunguza rushwa kwa nini wasingetoa namba zao za simu ili mtu anayehitaji huduma akizungushwa zaidi ya mara mbili basi aweze kupiga simu kwake ili kuingilia kati.tunaona urasimu mwingi katika idara mbali mbali kama hapa nchini kama vile tanesco,mashirika ya hifadhi ya jamii kama vile NCCF,mahakamani,mawizarani,wilayani,halmashauri,hazina,na sehemu nyingine.pia mtu akiona na kuwa na ushahidi wa wizi na rushwa aweze kutoa taarifa kama wananchi wanavyofanya katika jeshi la polis.madhalani,wizi wa rasilimali za taifa,meno ya tembo nk.leo kama ingeahidiwa ahadi ya bakshishi kwa atakayetoa taarifa ya majangili nadhani wengi sana wangekamatwa tena wakiwa kwenye ujangili au hata wakiwa na meno ya tembo.naomba wakubwa watoe mamba zao za simu na ahadi ya pesa kiasi fulani ili wananchi watoe taarifa za uzembe,wizi,rushwa na urasimu katika serikali na maeneo mengine.kama hakuna ushirika katika ujangili huu watatoa namba zao ili tusaidiane kazi,na pia kama wanataka ufanisi.