TUNAWASHUKURU YANGA KWA USHINDI WA SIMBA

ZINDAGI

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
1,117
1,426
Kwanza kabisa naipongeza Timu ya Simba Sport Club na Watanzania wote kwa namna mmoja ama nyingine kwa michango yao ya hali na mali mpaka kuiwezesha Simba kufanya vema katika kuiwakilisha East Africa na Kusini yote katika mashindano haya makubwa barani Africa.
Lakini mchango mkubwa sana umetolewa na timu ya Yanga kwa Simba, pressure kubwa iliyokua nyuma yetu kutoka kwa mashabiki wakubwa wa Yanga kutoka kada mbali mbali kuanzia viongozi wa serukali, kocha wa Yanga, viongozi nq wanahabari wapenzi wa Yanga, na bila kusahau mashabiki woote wa Yanga waliokua wanaandika kuhusu matokeo ya Simba.
Ama kwa hakika zile dua zao za sisi tufungwe ndio zilizotufanya tusilale na tujipange zaidi katika kuhakikisha tunafanikiwa ili tusiwape cha kusema.
Mwisho kabisa tunawapa pole upande wa pili kwa kupoteza mchezo wenu wa jana dhidi ya lipuli.

"Huku wanashinda, kule wanapoteza kwa taabu sana"

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom