Binafsi ninawamba TWAWEZA wafanye utafiti kwenye Halmashauri zetu kama Watumishi wa ujumla wanafanya kazi kwa kuwahudumia wananchi. Nashauri waangalie vigezo vifuatavyo:-
- Muda wa kuingia na kutoka kazini.
- Upatikanaji wa nyenzo za kufanyia kazi mfano:- stationaries,magari, mafuta nk.
- Upatikanaji wa bajeti kama ilivyopitishwa na Bunge.Je fedha zote zinateremshwa?.
- Asilimia ya miradi iliyotekelezwa na inayotekelezwa.
- Upungufu/ziada ya watumishi wanaotakiwa.
- Ajira mpya kama ipo.
- Upandishwaji wa vyeo kwa watumishi.
- Madai ya haki kwa watumishi kama wanalipwa.
- Motisha kwa watumishi kama yanalipwa.
- Ubora wa miradi inayotekelezwa kwenye Halmashauri.
- Ubadhirifu kwenye Halmashauri zetu.
- Ufuatiliaji wa miradi kama inafanyika mfano:- Kilimo, mifugo,maji,elimu, ujenzi nk.
- Utawala Bora kama ipo. Kwa maana kuwa Vikao vya vijiji vinafanyika na kwa ratiba.
- Morali ya watumishi.
- Ulipaji wa posho ya haki.