Tunawaomba TWAWEZA wafanye utafiti kwenye halmashauri zetu kama kazi zinafanyika

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Binafsi ninawamba TWAWEZA wafanye utafiti kwenye Halmashauri zetu kama Watumishi wa ujumla wanafanya kazi kwa kuwahudumia wananchi. Nashauri waangalie vigezo vifuatavyo:-

  • Muda wa kuingia na kutoka kazini.
  • Upatikanaji wa nyenzo za kufanyia kazi mfano:- stationaries,magari, mafuta nk.
  • Upatikanaji wa bajeti kama ilivyopitishwa na Bunge.Je fedha zote zinateremshwa?.
  • Asilimia ya miradi iliyotekelezwa na inayotekelezwa.
  • Upungufu/ziada ya watumishi wanaotakiwa.
  • Ajira mpya kama ipo.
  • Upandishwaji wa vyeo kwa watumishi.
  • Madai ya haki kwa watumishi kama wanalipwa.
  • Motisha kwa watumishi kama yanalipwa.
  • Ubora wa miradi inayotekelezwa kwenye Halmashauri.
  • Ubadhirifu kwenye Halmashauri zetu.
  • Ufuatiliaji wa miradi kama inafanyika mfano:- Kilimo, mifugo,maji,elimu, ujenzi nk.
  • Utawala Bora kama ipo. Kwa maana kuwa Vikao vya vijiji vinafanyika na kwa ratiba.
  • Morali ya watumishi.
  • Ulipaji wa posho ya haki.
Baada ya kufanya utafiti huo basi muishauri Serikali njia mwafaka ya kufanya.
 
Back
Top Bottom