Tunawafanya Wananchi Wajinga: Kuwaambia Rais katoa pesa wakati Bunge ndio limeidhinisha?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,798
71,218
Acheni kabisa kuwa fanya Watanzania ni wajinga na kuwa hawaelewi ya kuwa fedha ni zao lakini Bunge ndio linaidhinisha fedha zijenge Zahanati, barabara, madaraja, mikopo ya elimu nk nk.

Sasa hivi speed hiyo imekuwa kubwa "Rais JPM katoa fedha kuwajengea hospitali, katoa fedha kununua madawa ya mahospitali nk" kisha makofi mengi na vigelegele vya kufa MTU. Jee ni kutokuelewa hata hao wasemao au wametumwa kusema hivyo na wanahofu wasiposema watakosa kazi? Kwa nini watu na heshima zao mnasimama hadharani na kuwa puppet bila ya aibu?

La ajabu hawasemi huko vichochoroni bali hata mbele za wasomi ikiwamo hata ndani ya Bunge ambako ndio waliko idhinisha fedha hizo na mbele ya puppet namba moja Job Ndugai. Huyu ni mmoja ya maspika wanaoongoza kwa kutojifahamu Afrika, hakuna mfano wake kabisa.

Watanzania wanapaswa kuelimishwa kuwa fedha zote ni zao na zinaidhinishwa na Bunge na hata mshahara wa JPM anapangiwa alipwe nini sasa ayawezaje kutoa fedha za kujenga hospitali?
 
Hata kama Bunge limeidhinishwa hicho ndio kipaumbele cha Serikali ya JPM?


lakini mbona suala la ndege mnamlaumu JPM na siyo Bunge?
 
Msigwa jana ilibidi akimbie Twitter, alikuja na swaga zake za kitoto hahahaaa pumbavu kabisa
 
Je kama sio Rais Magufuli pesa zingetoka?

Tusione aibu kumpongeza Mzalendo Magufuli anafanya kazi kubwa
Pongezi nyingine ni za kipumbavu. Lakini tunapaswa kuwazia akili yahuyo anaepongezwa kwa mambo ambayo ni utaratibu wa serikali na anafurahia.

Kuna siku mtampongeza Magufuli kwa mvua za masika kunyesha Dodoma
 
Kama hawezi kupitisha fedha bila bunge, basi Chakaza eh, acha zile mada za tuhuma ya matumizi ya pesa bila idhini ya bunge. Hiyo itakuwa ni matumizi ya mazuri ya common sense kwa upande wako.
 
Hapa unacholalamikia wewe ni nini sasa?

Maana huwa mnalalamika Magufuli anatoa hela kiholela leo tena unalalamika kwanini waseme anatoa rais badala ya bunge?
Kugawa milioni kadhaa barabarani na miradi ya maendeleo iliyo zungumzwa bungeni ni vitu viwili tofauti
 
Watanzania tujifunze kuwa na shukurani. Bunge huwa linapanga bajeti kwa makisio ambayo yatakusanywa.

Serikali kupitia wizara ya fedha wanakusanya kupitia vyanzo mbalimbali kama mishahara na tozo.

Pasipo utawala (Executive Branch) kukusanya kilichokisiwa na Legislature hata nini kifanyike Fedha haziwezi kuwepo.

Nchi zi kifalme kama UAE ua Saudia, wafalme wanafanya kila kitu bila idhini ya bunge na maisha yanakwenda.

JPM mwenyewe wakati anafungua Hospitali ya Mloganzila (Muhas) alimshukuru JK kama Rais alieanzisha mchakato kuanzia kutafuta kiwanja mpaka kuidhinisha fedha kutoka.

Mara ngapi huko nyuma bunge lilitoa idhini ya hapakua na kilichofanyika au fedha zikaliwa.

Heri mtu/utawala unaotekeleza kwa vitendo yale yaliyoidhinishwa na BUNGE.

Mungu ibariki Tanzania.
Utekelezaji wa vitendo ukifanyika tunafaidi sote.
 
Kwa kasi hii ya maendeleo anayoifanya Rais wetu hata bunge lisitaarifiwe kuhusu allocation ya pesa flani mm shega tu

Mnakwama wapi nyie mang'ombe?...

Kwani miaka yote tokea uhuru mbona bunge liliifanya hiyo kazi unayoitaka wewe ila hakuna lililofanyika?

Au unataka kua kama wananchi wa gadafi waliokua wanakula kulala , kusaza na kuoleana bure kisha baadae "wakaambiwa" huyo anayewafanyia yote hayo ni dikteta et hawafai!!!!!

Wakakubali....leo wapo chini kati ya walio chini
 
Pongezi nyingine ni za kipumbavu. Lakini tunapaswa kuwazia akili yahuyo anaepongezwa kwa mambo ambayo ni utaratibu wa serikali na anafurahia.

Kuna siku mtampongeza Magufuli kwa mvua za masika kunyesha Dodoma
Yaani wamezidi ningekua mimi Magufuli ningeona aibu
 
Kwa kasi hii ya maendeleo anayoifanya Rais wetu hata bunge lisitaarifiwe kuhusu allocation ya pesa flani mm shega tu

Mnakwama wapi nyie mang'ombe?...

Kwani miaka yote tokea uhuru mbona bunge liliifanya hiyo kazi unayoitaka wewe ila hakuna lililofanyika?

Au unataka kua kama wananchi wa gadafi waliokua wanakula kulala , kusaza na kuoleana bure kisha baadae "wakaambiwa" huyo anayewafanyia yote hayo ni dikteta et hawafai!!!!!

Wakakubali....leo wapo chini kati ya walio chini
Nani kakudanganya? You have been brain washed kiasi ukilambishwa pipi unaona mambo safi kabisa.
Kwa hiyo kwako serikali kuwa na uwazi na check and balance havina maana kwa vile unanunuliwa ndege nakuambiwa ni USD 200 na kitu kumbe ni USD 100 na kitu?
Kuamsha maiti halisi ni kazi ngumu hata Gwajima haiwezi.
 
Yaani wamezidi ningekua mimi Magufuli ningeona aibu
Hawezi kuona hata aibu kwani akili zake na za hao waimbao pambio zinarandana kwa ubora wao!
Kuna watu, na wako humu wanajiita GT lakini ukiangalia wanacho kiandika ni akili ambazo hata 1960's watu hawakuwa nazo.
 
Back
Top Bottom