Tunauza matikiti maji

Tinywax

Member
Joined
May 17, 2014
Posts
7
Reaction score
1
Kwa wale wenye kuhitaji kununua matikiti kwa jumla, tunawakaribisha kufanya biashara nasi.

Tunayo mashamba makubwa ya matikiti yanayozalishwa kisasa kutumia njia ya umwagiliaji wa matone. Kwa sasa tuna mzigo wa tani 10 uliotayari kuingia sokoni.

Naambatanisha picha za maendeleo ya zao msimu huu. Pia waweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa facebook kwa jina la Tinywax au kupitia akaunti ya facebook Tiny Wax.

Kwa mawasiliano ya kibiashara ni PM, mnakaribishwa.


 
safi sana, mmeyalimia wapi hayo matikiti......jaribuni kutafuta wanunuzi toka kenya hao ndiyo mtapata bei nzuri mimi pia nikipata contacts zao ntaku pm...ushauri wangu tu msifanye biashara na wanunuzi roka soko la temeke stereo au wa soko la buguruni mtaliaaaaa
 
safi sana kazi nzuri unaweza kuwatembelea soko la mahakama ya ndizi last time nilipeleka hapo ila ikiwezekana kama shamba lako liko kuzunguka Dar ni vizuri ukupaliane shambani maana ukiyaleta halafu wanayakagua kama kitu gani huwezi tena kupandisha kwenye gari wanakulalia hapo ni kazi. Kila la heri kitu kinaonekana kimekaa vizuri huo ugreen nimeukubali
 

Mkuu wana nini hao wa Stereo na Buguruni?
Tujuze Mkuu!!
 
Tunauza mzigo wa kuanzia tani na kuendelea.
 
Mkuu wana nini hao wa Stereo na Buguruni?
Tujuze Mkuu!!

mimi nilikuwa nalimaga matikikiti mbele ya mkuranga panaitwa mwarusembe unaingia ndani kidogo..basi wakati wa kutaka kuuza wakawa wanakuja wanunuzi toka ktk masoko hayo wao wanakadiria bei ya shamba zima ulilo lima...ni walaliaji kiamaa, hawataki uwape bei ya kila tikiti moja wao wanataka nunua kwakukadiria...nkajitusu kulima pia matango hali ikawa hiyo hiyo kutoka kwao, ila ukipata wanunuzi toka kenya ah utapiga bao.....
 
Nitafute kupitia anuani ya tinywax.investments@gmail.com

Nimejaribu kujibu PM zote lakini zinagoma, sharti kwanza niwe nimefikisha post 5.

Kumradhi kwa wale waliotuma PM na hawajaona majibu
 
Ukipata mteja makini, mkuu Tinywax usisahau kutupa mrejesho.
 
Last edited by a moderator:
kila biashara inachangamoto zake. Nna miaka mitatu kwenye uzalishaji wa tikiti
 
soko langu kubwa ni ndugu jamaa na marafiki nna nnalikuza taratibu kama hapa jamiiforums naamini wapo wanajamiiforums zaidi ya elfu 4000 katika jiji la Dar peke yake. Ukiwa na mahitaji ya tikiti, wewe nitafute kupitia anuani ya tinywax.investments@gmail.com. Hapo tutapeana mawasiliano na namna ya kuja kuchukua tunda ulilonunua kwetu au namna waweza kutufikia ili upate mzigo.
 
Ujasema unalimia wapi mkuu wangu
 
Mkuu Tinywax mbona kimya, ama unakula pesa kimya kimya.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…