Tunatimiza hii ahadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunatimiza hii ahadi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The great R, Oct 9, 2011.

 1. The great R

  The great R Senior Member

  #1
  Oct 9, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Mimi TGR ninakuchukua wewe SSS kuwa mke wangu wa ndoa nina ahidi kukupenda na kukuheshimu,nitakufanyia fadhila na kukujali.nitakua pamoja na wewe katika shida na raha,magonjwa na afya,hadi kifo kitutenganishe,eeh mwenyezi Mungu nisaidie."
  Vigelegele vikapigwa ,makofi matarumbeta yani full shangwe,lakini leo hii huyu aliye apa hapo mbele za Mungu na binadamu anafanya kama si yote basi mawili au matatu ya yafuatayo:

  1. Uzinzi na uasherati
  2. Yuko bize na marafiki kila weekend
  3. Anachelewa kurudi home kila siku
  4. Anakunywa pombe akirudi hana hata dk moja na mkewe
  5. Tendo a ndoa hadi mkewe aombe
  6. Hasali nyumbani,kanisani wala msikitini
  7. Hana hata dk 2 na familia yake ili mradii kaacha matumizi basi
  8. Kila analofanya kwa ajili ya familia ni yeye labda na watu baki ila si mkewe
  9. Kutoa siri za ndani mwao
  10. Kumteta na kumsengenya mwenzake kwa ndugu,jamaa na marafiki.

  Hivi tunamchezea Mungu au?tunaona kuwa tupo duniani nakusahau kuwa ndoa ni mpango wa MUNGU na heshima inatakiwa iwepo ili tusihukumiwe adhabu.Jamani wenye ndoa tuheshimu ndoa zetu na wasiokua nayo tutakapoipata tufanye inavyopasa,tuuhurumiane.
   
 2. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,639
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  watu wengi wanaishi ktk ndoa kwa uzoefu tu kama ndoa zilizo salama basi ni chache sana mwana Jf
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Oct 9, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mimi mwenyewe ni muathirika wa hayo uliyoyataja hapo juu, nimevunja hizo amri sijui mara 1000.
   
Loading...